Kamanda Sirro kushika mikoba ya Tossi Oparesheni maalum

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
374
509
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Simon Sirro amehamishiwa makao Makuu ya jeshi hilo kushika nafasi ya aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Oparesheni Maalum Venance Tossi ambaye amestaafu.

Katika uhamisho huo nafasi yake itashikiliwa na kamanda wa mkoa wa Tabora Barow Lyimo. Hata hivyo inasemekana uhamisho huu unamsukumo na mkono wa CCM kutokana na madai kuwa hakukisaidia chama wakati wa uchaguzi.
DSC06764.JPG
 
Mhmm kwani hapo kapanda cheo au kashuka? Nyie wafanyakazi wa serikali mawazo yenu ni sehemu za rushwa tu!
 
Kwa hakika kamanda sirro wakimtoa mwanza itakua tabu,sirro amedhibiti uhalifu mwanza kwa asilimia 80,anapambana na majambazi kwa upeo wa hali yajuu,mpk sasa mwanza kumekua na nafuu kubwa kwa kupungua uhalifu,NI PIGO KUBWA KWA WAKAAZI WA MWANZA, KWA HAKIKA WATAMKUMBUKA SANA KAMANDA SIRRO.
 
Huyo ndiyo kiboko ya MAGWANDA, sasa jaribuni muone moto wake he he he he he heeeee
 
CCM they will always create fear kwa wananchi ili wapate kura na ndiyo janja yao kubwa .Hawaangalii usalama wa Nchi na wananchi wao ni madaraka tu .Wacha tuone
 
Sirro kamanda wa ukweli,ngoja akafanye mambo Operesheni maalum..namkubali sana kwa kazi anayoifanya anaiweza,habahatishi na wala hashurutishwi katika kutoa maamuzi,ukitaka kuamini rejea kumbukumbu za matukio wakati wa uchaguzi Mwanza jinsi alivyokabiliana nayo.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Simon Sirro amehamishiwa makao Makuu ya jeshi hilo kushika nafasi ya aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Oparesheni Maalum Venance Tossi ambaye amestaafu.
Katika uhamisho huo nafasi yake itashikiliwa na kamanda wa mkoa wa Tabora Barow Lyimo. Hata hivyo inasemekana uhamisho huu unamsukumo na mkono wa CCM kutokana na madai kuwa hakukisaidia chama wakati wa uchaguzi.

Kwani makamanda wa polisi wanatakiwa kupiga kura mara 100,000?. Huu ni upuuzi ambao utaendelea kuitafuna CCM. Kazi ya polisi ni kulinda usalama si kusaidia chama cha siasa. Ila as time goes viongozi wazee wakishamalizika na natural deaths, wasomi watajua kuwa kutumia dola kung'ang'ania madaraka ni national security threat, kwani siku watu wakiamua liwalo na liwe utawaua wengi na watakaobakia watakuwa na mioyo ya kulipiza visasi kwa ndugu zao waliouwawa. Ni hapo ndipo itakapokuja kuwa kuvaa nguo za kijani ni kuji-identify kama vile watutsi na wahutu walivyokuwa wanajitofautisha kwa pua zao. Kuuzima moto wa mioyo ya visasi ni more than using SMG au maji ya kuwasha. Hakuna atakayebaki salama kwenye hilo.
 
Natabiri kamanda mpya wa kutoka Tabora kumwaga damu naye kukutana na nguvu ya umma! Huwa hatumii akili
 
Mhmm kwani hapo kapanda cheo au kashuka? Nyie wafanyakazi wa serikali mawazo yenu ni sehemu za rushwa tu!
Amepanda atakuwa deputy Commissiner kutok senior assistant commissioner.atakuwa amebakiza cheo kimoja kufikia IGP.huyu bwana ni kichwa na askari kweli.ana nafasi ya kuwa IGP kama hawatambania
 
Ana viwango vya hali ya juu.anapashwa awe IGP. Amedhibti majambaz mwz, mirung frm kenya. Kama wamemtoa kwa mbinu za kisiasa basi tutaraji damu kumwagka mwz.
 
hapa siasa tu wala intelligensia haitumiki., yaleyale ya kudai mkataba wa Mhando umeisha. Watahangaika sana wazee wa magamba jibu rahisi,. tenda haki kwa wote na wajibika basi.
 
Huyo ndiyo kiboko ya MAGWANDA, sasa jaribuni muone moto wake he he he he he heeeee

Kiboko ya magwanda how? Mbona ameachia pale Mwanza key constituencies zikaenda mikononi mwa CDM?. Huo ukiboko wa CDM unatoka wapi hapo?
 
Kiboko ya magwanda how? Mbona ameachia pale Mwanza key constituencies zikaenda mikononi mwa CDM?. Huo ukiboko wa CDM unatoka wapi hapo?
Kwakuwa ni intelligent, ndio maana anajua kusoma alama za nyakati!
 
Fafanua wengine hatumjui background yake huyo Barow Lyimo....ila yaelekea ni Mchaga huyo?
ya anaitwa Liberatus Lyimo Barrow,ni mchaga ndiyo na huwa ana jaziba sana katika kutoa maamuzi,kamanda Simon Nyakoro Sirro amepandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishina Wa Polisi yaan Deputy Commissioner of Police,ni tofauti ya cheo kimoja tu cha Kamishina ndo unamfikia IJP,ni mpiganaji na anajua kusoma alama za nyakati,hana upendeleo wa kikabila wala kikanda,ni kipenzi cha askari na wananchi. alijiunga na Jeshi mwaka 1992 alipomaliza shahada yake ya kwanza ya sayansi ya elimu - Bachelor of science with education pale UDSM,alihudhuria kozi ya ukaguzi msaidizi wa polisi na baada ya kumaliza alipangiwa kuwa mkuu wa upelelezi wa kituo cha buguruni na baadae akahamishwa kuwa mkuu wa upelelzi kituo cha Magomeni baada ya kupandishwa cheo na kuwa mrakibu msaidizi wa polisi-assistant superintendent of police. Alifanya kazi pia mkoani Tabora kama naibu mkuu wa upelelzi mkoa wa Tabora na baadae akahamishiwa tena Dar kuwa naibu mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar. Alihamishiwa Shinyanga kama mkuu wa upelelezi mkoa na baadae akawa kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga. Alihamishiwa baadae mkoani Tanga km kamanda wa polisi wa mkoa na baadae mkoani mwanza kama kamanda wa polisi wa mkoa. Amepandishwa cheo na pia kuhamishiwa makao makuu ya polisi kama mkuu wa kitengo cha operesheni maalum ndani ya jeshi la polisi! Mungu amjalie maisha mema na marefu!
 
Back
Top Bottom