Kamanda Sirro kushika mikoba ya Tossi Oparesheni maalum

ya anaitwa Liberatus Lyimo Barrow,ni mchaga ndiyo na huwa ana jaziba sana katika kutoa maamuzi,kamanda Simon Nyakoro Sirro amepandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishina Wa Polisi yaan Deputy Commissioner of Police,ni tofauti ya cheo kimoja tu cha Kamishina ndo unamfikia IJP,ni mpiganaji na anajua kusoma alama za nyakati,hana upendeleo wa kikabila wala kikanda,ni kipenzi cha askari na wananchi. alijiunga na Jeshi mwaka 1992 alipomaliza shahada yake ya kwanza ya sayansi ya elimu - Bachelor of science with education pale UDSM,alihudhuria kozi ya ukaguzi msaidizi wa polisi na baada ya kumaliza alipangiwa kuwa mkuu wa upelelezi wa kituo cha buguruni na baadae akahamishwa kuwa mkuu wa upelelzi kituo cha Magomeni baada ya kupandishwa cheo na kuwa mrakibu msaidizi wa polisi-assistant superintendent of police. Alifanya kazi pia mkoani Tabora kama naibu mkuu wa upelelzi mkoa wa Tabora na baadae akahamishiwa tena Dar kuwa naibu mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar. Alihamishiwa Shinyanga kama mkuu wa upelelezi mkoa na baadae akawa kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga. Alihamishiwa baadae mkoani Tanga km kamanda wa polisi wa mkoa na baadae mkoani mwanza kama kamanda wa polisi wa mkoa. Amepandishwa cheo na pia kuhamishiwa makao makuu ya polisi kama mkuu wa kitengo cha operesheni maalum ndani ya jeshi la polisi! Mungu amjalie maisha mema na marefu!

Asante sana mkuu....(lakini mie nimeomba Background ya Barow), Huyo Sirro tunamjua toka akiwa UDSM akiwa mtu makini darasani na nje katika jamii iliyomzunguka,
 
Kumbe kamanda Sirro sio mzee kabisa na umri wake unamruhusu hata kuja kuwa IGP baada ya Mwema,may God bless him. Natumai huko alikopelekwa atafanya mambo makubwa hata zaidi ya Tossi!
 
Natabiri kamanda mpya wa kutoka Tabora kumwaga damu naye kukutana na nguvu ya umma! Huwa hatumii akili[/QUOTE
Siku zote inapotokea uhamisho wa Makamanda wa Polisi wamikoa napenda kuwakumbusha uhamisho wa Kamanda Basilio Matei kutoka Arusha baada ya kufanya kazi iliyotukuka ya kuzuia umwagaji damu na damu iliyomwagika baada ya kuletwa Kamanda Andenginye. Sipendi kuamini kwamba "UCHAWI" alioufanya IGP kwa kumuhamisha Matei Arusha unajirudia Mwanza.
 
Kwangu mimi kuhamishwa kutoka Mwanza kuja Dar ni promotion!

Mawazo finy hayo ndugu usifikiri kila anayehamishwa kutoka mkoano kuja Dar makao makuu anakuwa amepanda cheo, inategemeana na nafasi unayoishika lakini kwa kifupi kufanya kazi makao makuu hakuna ulaji kama kuwa kamanda wa mkoa.
 
Mhmm kwani hapo kapanda cheo au kashuka? Nyie wafanyakazi wa serikali mawazo yenu ni sehemu za rushwa tu!

Jifunze kuwa Muungwana,
To much generalization,
Mimi si mfanyakazi wa serikali,
Lakini kwa mawazo kama yako ni upotoshaji uliokithiri Jombaa.

jamani matusi ya nn humu,2we wastaarabu.wawe wamemwamisha kwa kutegemea itakuwa faida kwao wanajidanganya tu,kwn arusha wamefanikiwa sasa?mbona harakat ndo zimeshka kasi?
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Simon Sirro amehamishiwa makao Makuu ya jeshi hilo kushika nafasi ya aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Oparesheni Maalum Venance Tossi ambaye amestaafu.
Katika uhamisho huo nafasi yake itashikiliwa na kamanda wa mkoa wa Tabora Barow Lyimo. Hata hivyo inasemekana uhamisho huu unamsukumo na mkono wa CCM kutokana na madai kuwa hakukisaidia chama wakati wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa mke wangu (alikuwa huko wakati wa kampeni kama mwangalizi wa kimataifa )wakati wa kampeni aliyekuwa kamanda huko Mwanza alikuwa SACP Jamal Rwambo. Kisha akaamisha siku chahce kabla uchaguzi.
 
Mawazo finy hayo ndugu usifikiri kila anayehamishwa kutoka mkoano kuja Dar makao makuu anakuwa amepanda cheo, inategemeana na nafasi unayoishika lakini kwa kifupi kufanya kazi makao makuu hakuna ulaji kama kuwa kamanda wa mkoa.

Hapo sikubaliani na wewe, Kufanya kazi kwa kutegemea ulaji usio halali ndo unadidimiza Taifa letu.
 
ya anaitwa Liberatus Lyimo Barrow,ni mchaga ndiyo na huwa ana jaziba sana katika kutoa maamuzi,kamanda Simon Nyakoro Sirro amepandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishina Wa Polisi yaan Deputy Commissioner of Police,ni tofauti ya cheo kimoja tu cha Kamishina ndo unamfikia IJP,ni mpiganaji na anajua kusoma alama za nyakati,hana upendeleo wa kikabila wala kikanda,ni kipenzi cha askari na wananchi. alijiunga na Jeshi mwaka 1992 alipomaliza shahada yake ya kwanza ya sayansi ya elimu - Bachelor of science with education pale UDSM,alihudhuria kozi ya ukaguzi msaidizi wa polisi na baada ya kumaliza alipangiwa kuwa mkuu wa upelelezi wa kituo cha buguruni na baadae akahamishwa kuwa mkuu wa upelelzi kituo cha Magomeni baada ya kupandishwa cheo na kuwa mrakibu msaidizi wa polisi-assistant superintendent of police. Alifanya kazi pia mkoani Tabora kama naibu mkuu wa upelelzi mkoa wa Tabora na baadae akahamishiwa tena Dar kuwa naibu mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar. Alihamishiwa Shinyanga kama mkuu wa upelelezi mkoa na baadae akawa kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga. Alihamishiwa baadae mkoani Tanga km kamanda wa polisi wa mkoa na baadae mkoani mwanza kama kamanda wa polisi wa mkoa. Amepandishwa cheo na pia kuhamishiwa makao makuu ya polisi kama mkuu wa kitengo cha operesheni maalum ndani ya jeshi la polisi! Mungu amjalie maisha mema na marefu!
Kumbe ni msomi, hagangi njaa!!
Kweli hata mie namzimikia uongozi wake, he is great!! Bravo kamanda! mungu amuwezeshe zaidi awe IGP!
 
Back
Top Bottom