IGP Simon Sirro apangua Makamanda wa Polisi wa Mikoa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amefanya uhamisho na mabadiliko ya makamanda wa Polisi wa mikoa kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Aprili 6, 2022 na msemaji wa jeshi hilo, David Misime imeeleza kuwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Onesmo Lyanga amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi, huku nafasi yake ikichukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Martin Otieno.

“Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Daniel Shillah amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa polisi mkoa wa Kaskazini Unguja” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mwanza (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Faustine Mafwele amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO).

“Aliyekuwa Naibu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (D/RCO) mkoa wa Mwanza Mrakibu Mwandamnizi wa Polisi (SSP) John Lwamlema anakuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mwanza (RCO)” imeeleza taarifa hiyo.

Polisi.jpg
 
Sirro ungepumzika tu braza! zama zako zimepita! Tanzania ya leo pamoja simkubali mange kimambi ila wewe kwenda kufunga akaunti yake ya benki UMEAMSHA hasira za wafanyabiashara ambao walianza kumuamini MAMA! umesababisha waanze kujiuliza tena kumbe wanaweza kurudishwa motoni tena maana wewe bado upo unafurahia tabia za ZAMANI!

SIRRO ondoa aibu jeshini humo pumzika
 
Kuna Nini Ndani Ya Jeshi La Polisi.
.
Naona Sirro amekuwa akifanya SAna Mabadiliko ya Marpc Kila WAkati.
Screenshot_20220406-162243.jpg
 
Yule aliyesema anatamani kuwa IGP nae vipi amepanguliwa au bado yupo kitengo kile kile...?
 
Sirro ungepumzika tu braza! zama zako zimepita! Tanzania ya leo pamoja simkubali mange kimambi ila wewe kwenda kufunga akaunti yake ya benki UMEAMSHA hasira za wafanyabiashara ambao walianza kumuamini MAMA! umesababisha waanze kujiuliza tena kumbe wanaweza kurudishwa motoni tena maana wewe bado upo unafurahia tabia za ZAMANI!

SIRRO ondoa aibu jeshini humo pumzika
Hivi habari inatoka tu na anafanya mabadiliko?
Kumbe yasemwayo yapo
 
Huu ni ushindi mnono kwa yule Kigagula Mange Kimambi, hususan kuhamishwa kwa Shillah (ZCO)
 
Back
Top Bottom