Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

Huyu mzee naona anakaribia kufa narudia tena kufa.Kulikuwa na watu wana kiburi kama akina Dito, wako wapi?
 
JUMAMOSI, SEPTEMBA 22, 2012 08:48 NA ELIZABETH MJATTA

KAMANDA wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, ameibuka na kusema hawezi kujiuzulu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, Daud Mwangosi, aliyeuawa hivi karibuni mkoani Iringa.

Kamanda Kamuhanda alitoa msimamo huo jana alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Radio cha Radio One wakati wa kipindi cha Kumepambazuka.

“Ninachofahamu mimi ni kwamba, kesi ya msingi iko mahakamani na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ameshaunda kamati ambayo inachunguza mwenendo mzima wa tukio hili na baadaye itatoa taarifa.

“Kwa hiyo, siwezi kujiuzulu kwa sababu tukio hilo la kifo lilitokea wakati wa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti,” alisema Kamanda Kamuhanda.

Alipoulizwa kuhusiana na kuwajibika kutokana na mauaji hayo alisema, hawezi kuwajibika kwa sababu hana makosa.

“Niwajibike kwa kosa lipi?, kuna kosa mtu anaweza akawajibika, lakini kama huna kosa huwezi kuwajibika, haiwezekani watu waliofanya makosa wenyewe kwa kuandamana bila uhalali wasiwajibike halafu mimi niwajibike, haiwezekani.

“Sisi tunapokuwa kazini, tunalinda raia na mali zao na ndiyo tulilofanya na mara zote tunasisitiza utii wa sheria bila kushurutishwa.

“Kwa hiyo, hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika, kilichofanyika ndiyo utii wa sheria bila shuruti, wangetii sheria bila shuruti yote yasingetokea,” alisema.

Septemba 2 mwaka huu, Mwangosi aliuawa kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu alipokuwa kazini katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Baada ya kulipuliwa na kitu hicho, mwili wake ulisambaratika vipande vipande ingawa pia askari mmoja aliyekuwa jirani naye, pia alijeruhiwa mguu.

Baada ya tukio hilo, waandishi wa habari, wanaharakati na watu mbalimbali, walilaani tukio hilo na kutoa matamko yao wakitaka Kamanda Kamuhanda ajiuzulu, kutokana na mauaji hayo.

Septemba 12 mwaka huu, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mwenye namba G2573, Pasificus Simon, alipandikizwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Iringa, kwa kosa mauaji ya marehemu Mwangosi.

Mtuhumiwa huyo alipofikishwa mahakamani hapo, hakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa linalomkabili haliwezi kusikilizwa katika mahakama hiyo. Hadi sasa mshitakiwa yuko mahabusu.

Hapa linalotakiwa ni kweli siyo kujiuzulu bali kufikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji. Kutii sheria bila shuruti pale haihusiki, kamanda nadhani inafaa apewe video clips aangalie, tukio la mauaji lilitokea baada ya watu kutii amri yake na kutawanyika. Pia ajue kuwa yale hayakuwa maandamano kama anavyodai labda atumie sheria ya Mkusanyiko, alafu ajue aliyeuawa si kiongozi wa chama, bali Mwandishi wa habari aliyekuwa kazini tena akiwa na amani na si katika fujo kama yeye alivyokuwa pale. Mbaya zaidi, Mwandishi hakuwa na silaha yoyote hatarishi, alikuwa ameshawekwa chini ya mikono ya askari zaidi ya mmoja(asome sheria ya kumu-arrest mtu) na kosa lake Kamanda, alikuwa pale maeneo ya tukio akishuhudia toafuti na ilivyokuwa kwa afande Zomba(hakuwepo katika tukio). Kifupi, mazingira ya mauaji, uwepo wake ndio ulizidisha hata wale askari kutotii amri ya kumuacha aliyokuwa anawaeleza kamanda aliyekuwa nao, badala yake walikuwa wanatii huyu kamanda Kamuhanda. Ni katika hili, yeye ilipaswa awe mshtakiwa namba moja, askari hao wengine pamoja na huyo aliyepelekwa mahakamani washrakiwa namba mbili na kufuata. Kung'ang'ania utii wa sheria bila shuruti haina mshiko hapo, na ikutumiwa hivyo atasababisha watu kudai kujiuzulu kwa viongozi wake wa juu, yeye sasa hivi akiri amesababisha haya yote, haikuwa maandamano ajue hilo,aangalie video clips zimsaidie anapoongea badala ya haya aliyosema.
 
Wakuu naomba kuuliza swali la ufahamu, "Mada kama hizi mbona siwaoni Ritz na Zomba"? Au wao wanahusika kwenye mada za CDM tu???
 
Chondechonde watanzania wenzangu tusiache huu uppuzi uendeleee. Tunaomba vyama vya siasa bila kujali ni chama gani wakishirikiana na wananchi wote tuandee maandamano ya kulazimisha huyu muuaji pamoja na wenzake kujiuzulu. Amenikera kweli huyu shetani.
 
Majibu yake yamenistua sana.

Hakika sheria si mali kitu kwa the keeper.
 
acheni kelele, kamanda kesha ongea, andamaneni tena tuwatwale mitwe.
Afterall mna uhakika gani kuwa bomu lililomuua mwangosi limetoka kwenye bunduki ya yule dogo. Inawezekana walikuja nalo ili wawalipue polisi kwa jazba na kumbe wameua mwandishi.
Ni mawazo yako Mkuu kama vile hao unaotaka waache kelele nao wanavyotoa mawazo yao. Kuhusu hilo bomu tayari jibu lishatolewa na mamlaka husika kumbe hatujadili jambo hilo na hatunasababu ya kutumia neno"inawezekana" bali tunajadili wahusika wa mauaji ili wachukuliwe hatua stahiki.
 
acheni kelele, kamanda kesha ongea, andamaneni tena tuwatwale mitwe.
Afterall mna uhakika gani kuwa bomu lililomuua mwangosi limetoka kwenye bunduki ya yule dogo. Inawezekana walikuja nalo ili wawalipue polisi kwa jazba na kumbe wameua mwandishi.

Unajua hujui kuwa hujui!. Coincidence: Kamuhanda (mhaya), alimtuma Pasificus Simon (mhaya), kumuua Mwangosi (Mnyakyusa) na mtetezi wake OCD - Mwampamba (mnyakyusa) akajeruhiwa. Haya yanasemwa site!.
 
Nikisoma habari kama hii najiuliza maswali mengi,jibu ninalopata ni kwamba hatuna jeshi la Polisi hapa,bali watu wasiokua na nidhamu wala mafunzo ambao wanajiita Polisi. Ni heri ya mgambo kuliko hawa watu wanajiita Polisi hapa Tanzania!
 
Majibu yake yamenistua sana.

Hakika sheria si mali kitu kwa the keeper.
Mkuu hata humu nadhani yupo,maana kuna watu huwa wanaposti maneno kama hayo kabisa.Yaani ya ku justify kile kifo kwa namna anayoifanya Kamuhanda.Mkuu muwe mnawalima ban ili at least tupate hata justice kidogo hapa kume enzi marehemu.Huku tukisubiri haki ichukuwe mkondo wake na huko uraiani God willing!
 
Waandishi wa habari mnazidi konyesha udhaifu mwingine baada ya Kifo cha Mtanzania mwenzetu D. Mwangosi mimi sisemi mwandishi wa habari tu bali mtanzania mwenzetu kwa maana mlolongo wa mauaji yanayo ligusa jeshi la polisi ni mengi sasa nilifurahi sana kusikia Azimio la wanahabari baada ya kifo cha huyu ndugu yetu lilikuwa kuanzia siku hiyo hadi siku 40 wanahabari hawataaandika habari yoyote inayohusiana na jeshi la Polisi ajabu hata wiki mbili baadhi ya vyombo vya habari vina waaalika watuhumiwa wa mauaji ya ndugu zetu nao wanaishia kutoa matamko kama mliyoyasikia ndugu zangu mnajipendekeza kwao ili iweje????????????? wengine walisema pale Jngwani kwamba hawana Ugonvi na Waziri E.Nchimbi, wala hawana ugonvi na serikali yao nikajiuliza wanahabari ninyi mgonvi wenu katika hili ni nani hasa??endapo baada ya kumuona waziri mwenye Dhamana na chombo anachokiongoza mkamtumia salaamu za kumpenda sasa mgonvi wenu ni nani hasaaaaaaaaaaaaaaaaaa?????????
 
Kamanda wa uongo huyu, kamanda gani mwoga vile, kama kweli wanajiamini si wangeweka silaha chini zikapigwa kavukavu? sasa wewe unakuja na bunduki?
 
Hahaha mkuu.
Kanuni za JF hazuruhusu kuwa bias kwenye maamuzi na hakuna aliye juu yake.
Ha ha ha!sawa mkuu,ila sidhani kama justice iko bias.Hakuna justification ya kuwaua raia wasokuwa na hatia kwa kusema ukweli mkuu.So unaweza usimlime Kamuhanda ban humu,however ukamwambia azingatie ubinaadam kidogo.Kwa mfano kuna picha humu iko wazi kabisa kuwa polisi ameuwa,lakini utashangazwa upotoshaji wa wazi wa either kujustify tukio lile ama kusema ni chama cha upinzani kimefanya mauwaji.

Anyways mkuu,ni kweli kama justice ikichukuwa mkondo wake,basi hawataweza kutetea unyama kama ule humu ndani.

Kazi njema mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
kwanza kabisa aliyekuwa anamuhoji hakuwa na nia ya kujua mengi kutoka kwa muhojiwa;
alikuwa anatimiza wajibu wake wa kazi kwa waandamanaji walioshindwa kutii sheria bila shuruti, hivi mwangisi alikuwa akiandamana? huwa hakuna exemption kati ya waandishi wa habari na raia wengine? kama ipo kwa nini mwangisi ameuawa wakati yeye sio mwandamanaji? ( walao ingekuwa na raia angesingizia hicho anachokisema). halafu hakumfahamu marehemu kabla ya mauaji kutekelezwa? mbona picha zilimuonyesha amejiegesha pembeni akifuatilia tukio zima? kwa hiyo sasa mmeamua kusema tu hata uongo wa wazi bila kujali ukweli ulioko wazi?
Mungu akitujalia uzima tutajua ukweli tu, yatajidhihirisha tu kwa namna yoyote ile
 
Wakuu naomba kuuliza swali la ufahamu, "Mada kama hizi mbona siwaoni Ritz na Zomba"? Au wao wanahusika kwenye mada za CDM tu???

Kwenye mada zinazocompromise position ya JK Ritz na Zomba ni observers tu. Baadae JK atawadebrief ili kutathmini upepo

Mfano mwingine ni ile mada ya gas na oil hutamwona Ritz au Zomba kule. Maslahi ya JK yameguswa
 
Kwenye mada zinazocompromise position ya JK Ritz na Zomba ni observers tu. Baadae JK atawadebrief ili kutathmini upepo

Mfano mwingine ni ile mada ya gas na oil hutamwona Ritz au Zomba kule. Maslahi ya JK yameguswa

Kwa sasa wako kwenye SHIMIWI kule Morogoro wakisimamia hii timu ya IKULU

sh2.jpg
 
Back
Top Bottom