Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

Tutambue kuwa jeshi zima limejaza ma kamuhanda watupu!. A blood philic force!
 
“Kwa hiyo, siwezi kujiuzulu kwa sababu tukio hilo la kifo lilitokea wakati wa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti,” alisema Kamanda Kamuhanda.

Wakati mwingine unaweza pima IQ ya mtu kwa matamshi yake.......:rockon:
 
.......Daah hili lijamaa ni Zero kabisa.......huyu RPC aondolewe haraka.........yaani mtu unaua halafu unaropoka ropoka tu........halafu watu tunamuangalia tu.........damn

Kamuhanda must go......
 
Hata kama Mwangosi aliandamana na hata kama alikataa kutii sheria ni halali kumripua bomu raia asiye na silaha yoyote tena huku akiwa yuko chini kazungukwa na askari? walishindwa nini kumkamata na kumpeleka kituo cha polisi, kumfungulia charge na kumpeleka mahakamani ambako haki ingetendeka?

Majibu ya huyo kinyago ni ya kishetani. Anaongea akionyesha kuwa mauaji hayo yalikuwa na baraka zake eti kwa vile alikataa kutii bila shuruti.

Siku zote nasema polisi ni vema wawe wanapimwa akili kuona kama hawatumii majani. Endeleeni kuua kadri mnavyotaka, mnafurahi kumwaga damu za raia wasio na hatia. watoto, wajane, wagane wao wanabaki wanalia na kuomboleza.

Nyinyi mnashangilia kwamba mnatekeleza wajibu wenu kwa kunyofoa roho za watu bila huruma. Ipo siku mtajutia matendo yenu. Itakuwa nafuu ya wajane, yatima na wagane wanaoomboleza kwa sababu ya ushetani wenu.
 
Watu wengine bana; sasa kama anachosema ni kweli kwanini wamempendesha yule bwana mdogo kizimbani?
Mzee Mwanakijiji,
  1. Ile ni scapegoat tuu ili ku defuse hasira za wananchi na international comunity!,
  2. Polisi wamefanya mauaji Zanzibar kwenye maandamano ya CUF, no one ameshitakiwa!.
  3. Polisi wameua maandamano ya Chadema, Arusha, no ine ameshitakiwa!
  4. Polisi wameua maandamano ya Chadema, Mbeya, no ne ameshitakiwa!.
  5. Polisi wameua maandamano ya Chadema, Songea, no one ameshitakiwa!.
  6. Polisi wameau maandanano ya Chadema, Morogoro, no one ameshitakiwa!.
  7. Lakini baada ya polisi kuua mwandishi wa habari!, kwenye maandamano ya Chadema, Iringa, sasa ndio someone ameshitakiwa!, hamjiulizi?. Ndio maana nimewaambia its just a scapegoat!.
  8. Bwana mdogo ameshauriwa akiri kila kitu ili kumuakoa aliyetoa amri!.
  9. Kesi inageuzwa from murder to manslaughter!
  10. Na itasikilizwa kwa siku tuu na kusubiri hukumu!.
  11. Kutokana na public interest, hukumu itatolewa mapema, tena kali!.
  12. Ataondoshwa as if anaenda kutumikia kifungo, ataachiwa, atahamishwa, ata badili jina na kupangiwa kazi nyingine!.

Pasco.
 
Nadhani angefanya uungwana wa kujiuzulu ili kupisha uchunguzi....halafu hizi ripoti za tume/kamati mbona hatuzioni hadharani??. hivi haiwezekani uchunguzi ukafanywa na makundi mbalimbali tofauti??

Taasisi za haki za binadamu, taasisi za kidini nk...kukawa na ripoti nyingi nasi tupate wasaa wa kuzisoma??nadhani hii inaweza kusaidia kutuletea majibu ya kuaminika kidogo kuliko hii ambayo inaweza kuja na majibu ya '' upepo mbaya'' na ikawa siri.... kwani nayo imekaa kisiasa kama jambo lenyewe.....

Kingine cha ajabu uchunguzi unaendelea na kesi inaendelea mahakamani
 
kwa nini waandishi wa habari huwa mnawaauliza hawa mnaowauliza maswali mwongozo? kwa nini usimuulize ni makosa gani ambayo yanapaswa mtu akawajibika kama alivyosema kuna makosa ya kuwajibika?

mi ningemuuliza 'KAMA MNALINDA RAIA NA MALI ZAO,MBONA MMEUA?,SWALI LA PILI KAMA ISHU NI UTII BILA SHURUTI JE MWANGOSI ALIKUA ANAANDAMANA AU ANATEKELEZA WAJIBU WAKE KAMA WEWE?'
TATIZO LA WAANDISHI MAKANJANJA HILO
 
Mzee Mwanakijiji,
  1. Ile ni scapegoat tuu ili ku defuse hasira za wananchi na international comunity!,
  2. Polisi wamefanya mauaji Zanzibar kwenye maandamano ya CUF, no one ameshitakiwa!.
  3. Polisi wameua maandamano ya Chadema, Arusha, no ine ameshitakiwa!
  4. Polisi wameua maandamano ya Chadema, Mbeya, no ne ameshitakiwa!.
  5. Polisi wameua maandamano ya Chadema, Songea, no one ameshitakiwa!.
  6. Polisi wameau maandanano ya Chadema, Morogoro, no one ameshitakiwa!.
  7. Lakini baada ya polisi kuua mwandishi wa habari!, kwenye maandamano ya Chadema, Iringa, sasa ndio someone ameshitakiwa!, hamjiulizi?. Ndio maana nimewaambia its just a scapegoat!.
  8. Bwana mdogo ameshauriwa akiri kila kitu ili kumuakoa aliyetoa amri!.
  9. Kesi inageuzwa from murder to manslaughter!
  10. Na itasikilizwa kwa siku tuu na kusubiri hukumu!.
  11. Kutokana na public interest, hukumu itatolewa mapema, tena kali!.
  12. Ataondoshwa as if anaenda kutumikia kifungo, ataachiwa, atahamishwa, ata badili jina na kupangiwa kazi nyingine!.

Pasco.

polisi waliua MWAMBE CHAI,hakuna aliyeshtakiwa,polisi wameua nyamongo,
 
Nazani damu ya Mwangosi imeanza zaa matunda maana mzee keshaanza changanyikiwa CDM walikuwa na mkutano wa ndani yeye anaongelea maandamano!
Kamanda ni busara kukaa kimya otherwise unaaribu
Alafu na huyu mwandishi yuko shallow na hakujiandaa kabisa au ndo uko katika harakati za kumsafisha Kamudandu?

Mbona mnahangaika jamani!! ASKARI anatakiwa kutumia nguvu sana na AKILI KIDOGO. hiyo ndio falsaha ya Jeshi la kikoloni
 
nina shaka na elimu ya kamhanda kwani yawezekana hata mtu ambaye tunaongea naye pengine hata uwezo ni mdogo siyo tu kielimu bali pia hata kiwango cha kufikiria nachokipo chini kama kweli kazi ya polisi ni kulinda haki za raia na yeye anakiri iweje huyo simon amabaye ni askari apandishwe kizimbani kujibu mashitaka kama asingekuwa na kosa kama huyo anayejiita kamuhanda anavyosema basi hata huyo simon asingepandishwa kizimbani na pia nina wasiwasi na tafsiri halisi ya kutia bila shuruti maana naona anatumia kigezo hicho kukiuka sheria hii na kama ataendelea kuitafsiri kama anavyodai basi kuna uwezekano wa kuua raia wengi zaidi ya hao waliokwisha tangulia mbele ya haki
 
mi ningemuuliza 'KAMA MNALINDA RAIA NA MALI ZAO,MBONA MMEUA?,SWALI LA PILI KAMA ISHU NI UTII BILA SHURUTI JE MWANGOSI ALIKUA ANAANDAMANA AU ANATEKELEZA WAJIBU WAKE KAMA WEWE?'
TATIZO LA WAANDISHI MAKANJANJA HILO
hakika comrade ukanjanja ndio unaotuumiza wakishapokea bahasha bhaaaaaaaaaaaaaaas ni baadhi lakini
 
.
Njaa mbaya sana. Waandishi wengi Tanzania wanauliza maswali huku wakiwa wamechora picha ya bahasha ya kaki kichwani.
.
ni kweli comrade hii nchi isha haribikiwa kabisa ni ya kitu kidogo makanjanja wanaidhalilisha fani ya uandishi wa habari
 
mzee akumbuke kuna video ya dk 26 na tumeona kila kitu
 
ok naona msuso wa waandishi wa habari unaendelea kwa nguvu kubwa
 
Back
Top Bottom