Mauwaji aliyoyafanya ni ya kisiasa,na kwahiyo majibu yake pia ni ya kisiasa.
Hata asipojiuzulu,kuna wakati atajibu tuhuma hizi za mauwaji.Nchi za wenzetu kashfa kama hii wala asingethubutu kupanua mdomo,maana angekuwa keshajiuzulu na angeogopa maneno yake yasitumike dhidi yake wakati wa mashtaka.Kwa mfano kauli kuwa watu wakikusanyika kufunguwa tawi basi wauwawe kwasababu wamevunja sheria.Kauli kwamba walifanya maandamano ni ya kisiasa,kwasababu mwanzoni alisema ni mikutano haitakiwi kwasababu ya sensa,lakini cha ajabu ccm ilikuwa na mikutano,na pia kulikuwepo na fiesta.
Only in Tanzania haya ndo yanaonekana kuwa ni ya kawaida.
Huyu jamaa uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana,yaani pamoja na kusimamia mauwaji ya kizembe yanayolalamikiwa na ulimwengu mzima bado haoneshi ata chembe ya kujutia. Kama wasiotii sheria bila shuruti hukumu yao ni kuuawa mbona hawakuua walioandamana bila kibali kushinikiza kuachiwa waliogomea sensa au waliokata uzio uliowekwa na polisi pale kidongo chekundu? Kama polisi walikuwa wanatekeleza majukumu yao halali kwa nini mtuhumiwa amepelekwa mahakamani? Sishangai sana lkn maana ata raisi wetu ana fikra kama za Kamuhanda ndio maana akuona umuhimu wa kutoa japo pole ya mdomo tu kwa wafiwa.