Bahati mbaya sana wasiowachuna ndio mnaowapotezea muda. Mwanamke anayekuchuna ndoa sio kipaumbele chake kwako.Sasa ukinichuna kila siku kwanini nikuoe? si bora tuwe tunachunana nikiwa nashida na mimi
Kwahiyo unasapoti hili suala la wanawake kupotezewa muda sio?[emoji23] [emoji23] kumwambia mwanamke naomba mchezo tu sikuoi labda wale wengine wa sokoni ila sio nyie. utaanzia wapi.
Natamani wanaume wote wangeuchukua huu ushauri.....jamani acheni kutupotezea muda,mnatuumiza sana!
Wanachoudhi unamkuta mdada anahangaika na njemba miaka nenda miaka rudi eti boifrendi. Waoaji wa kweli hata salamu zao hazijibiwi. Na ole wako umwambie anapotezewa muda uone matusi utakayokogeshwa. Mi najisemeaga wakome tu.
Duuh! Lakin neno UUNGWANA litawale ktk mioyo yetuaaah wapi kuna vichunaji vimezaliwa na roho za kuchuna...
nyie tuendeleeni hivi hivi... kuviziana hadi kieleweke.
SawaAcheni kuwalaumu wanaume...wee binti na akili yako mnadate na njemba miaka 2 Bado hajatangaza Nia unakenua meno tuu Hui no ujinga wako mwenyewe. Tumikisha mayele yako.
Tuwe wakweli hivi ni wanawake wangapi mnawekeza Mali zenu kwenye mahusiano tunayokuwa nanyi?
Kama una date binti wa umri wa kuanzia miaka 23 huna mpango wa kumuoa fanya jambo la kiungwana na kumuambia ukweli.
Sikuambii umuambie kua humtaki na hutaki kuoa bali muambie kua wewe si muoaji na unaona kua utampotezea muda wake bure na kuja kumuumiza.
Ongea kiungwana na ikishindikana muache hata kibabe. Hii ni kwasababu mwanamke anawekeza vitu vingi katika mahusiano, anawekeza akili yake, mali zake, hisia na kubwa kabisa anawekeza umri wake katika mahusiano.
Unampunguzia uwezekano wa kukutana na mtu sahihi kwa kuendelea kumdanganya. Kwa Mwanamke, ```"Age is not just a Number, Age is Everything".```
Wakati ukimuacha wewe utatafuta Binti mdogo zadi yake, yeye atalazimika kutafuta Kijana mwenye Umri Mkubwa zaidi yake. Ndiyo ilivyo sote Wanaume na Wanawake huangalia Umri katika Mahusiano.
Ukimchezea na kumuacha akiwa katika Umri wa Miaka 30, inamaana atafute kijana mwenye Umri kuanzia Miaka 32 ambaye bado ni Single.
Wako wachache sana wa namna hiyo, sisemi kua hawezi kupata, hapana.. Nasema utampa Wakati Mgumu na Uhuru wa Kuchagua.
Kuna Umri ambao Mabinti wengi huamua Kuolewa tu, si kwasababu ya Mapenzi bali kwakua hawana namna wanaona kusubiri Mtu Sahihi watapishana na Kalenda.
*Badilika, haikufanyi Mwanaume zaidi kwa kumpotezea Binti wa watu Miaka Mitano halafu unamuambia* ```"Wewe si Type yangu"*``` Fanya jambo la Kiungwana na Malizaneni Mapema.
Lakini najua kuna Mabinti ambao hawasikii wakiambiwa kuwa mambo yameisha, Mlazimishe asikie na Usimtumie na Kumuumiza kwakua anakupenda.
naliunga mkono hadi siku tutakayosema tunapotezeana muda.Kwahiyo unasapoti hili suala la wanawake kupotezewa muda sio?
Kuna mzee namjua ana miaka almost 60 now huwa hafichi anasimuliaga historia yake.Kuna jamaa yangu mmoja muharibifu sana.
Alianza kudate na huyu mdada akiwa ndo anaota chuchu!
Kamchakaza karibu miaka 8 na mtoto juu akampatia!mwisho wa siku jamaa anapata mchumba mwingine huku anamwambia yule alietoka nae mbali"MI SASA HIVI NATAKA KUOA BIKRA NA NDOA MWEZI UJAO"
kiukweli yule mshkaji wangu nilimchukia sana kuanzia hapo.amempotezea muda mdada wa watu kazi ikawa kwangu kila siku nambeleleza huyu dada asijiue atulie tuu amwachie mungu.
wanawake mnapenda maneno matamu.
sasa ni maneno machache ya kweli matamu. mengi matamu ya uongo...[/QUOTE
Sio kweli.
Hakuna uongo mtamu. Maneno ya uongo ni matamu kwa anayeongea.
Ule uongo unaoongea unatakiwa uwe ukweli na ni haki kwa binti kufanyiwa hayo na sio magumu kumtendea ndomana binti anaamini.
Ila sababu binadamu we are selfish and evil unamfata binti ili umharibu na huo ndo ukweli wako kwaio sababu unajua fika hastahilo kufanyiwa uharibifu then unakuja na uongo.
Issue sio mabinti wanapenda kudanganywa, ni kwamba unakuja kwa binti kwa lengo lako la kishetani ila unatumia uongo kujifanya malaika.
Kosa la binti ni kuamini kuwa wewe ni malaika kumbe ni shetani halisi
Haswaa. Hii niliwah kuandika makala kuhusu kitu kinaitw "circle of pain". The concept behind ni kuwa unapomtumia mwanamke na kumuumiza, na yeye atabeba hayo maumiv na kisasi, atakutana na mwanaume mwenye nia na upendo, atamuumiza huyo mwanaume. Na huyu mwanaume atabeba maumiv na kisas na kumuumiza mwanamke mwingine.Ndio chanzo cha kufanya wasichana wawe wakorofi...wachunaji...maana wanaishi na maumivu ya kuachwa...
Hahaha yalinikuta hayo. Niliitwa mume siku ya kwanza, ya pili nikapigwa bomu la nuclear Ukimuangalia ni mdada mzuri na anamchumba wake. Sa sijajua ni dhiki au yunaoimana imanna wanawake wa siku hizi mnajua kutingisha kiberiti kweli.
unachukua mawasiliano ukifika nyumbani ukisema usalimie meseji ya kwanza ushaitwa baby. ya nne Baby mwenye nyumba wangu anasumbua.