Kama wewe sio muoaji ni bora umwambie ukweli

Kama wewe sio muoaji ni bora umwambie ukweli

toriyama

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
1,566
Reaction score
3,234

Kama una date binti wa umri wa kuanzia miaka 23 huna mpango wa kumuoa fanya jambo la kiungwana na kumuambia ukweli.

Sikuambii umuambie kua humtaki na hutaki kuoa bali muambie kua wewe si muoaji na unaona kua utampotezea muda wake bure na kuja kumuumiza.

Ongea kiungwana na ikishindikana muache hata kibabe. Hii ni kwasababu mwanamke anawekeza vitu vingi katika mahusiano, anawekeza akili yake, mali zake, hisia na kubwa kabisa anawekeza umri wake katika mahusiano.

Unampunguzia uwezekano wa kukutana na mtu sahihi kwa kuendelea kumdanganya. Kwa Mwanamke
, ```"Age is not just a Number, Age is Everything".```

Wakati ukimuacha wewe utatafuta Binti mdogo zadi yake, yeye atalazimika kutafuta Kijana mwenye Umri Mkubwa zaidi yake. Ndiyo ilivyo sote Wanaume na Wanawake huangalia Umri katika Mahusiano.

Ukimchezea na kumuacha akiwa katika Umri wa Miaka 30, inamaana atafute kijana mwenye Umri kuanzia Miaka 32 ambaye bado ni Single.

Wako wachache sana wa namna hiyo, sisemi kua hawezi kupata, hapana.. Nasema utampa Wakati Mgumu na Uhuru wa Kuchagua.

Kuna Umri ambao Mabinti wengi huamua Kuolewa tu, si kwasababu ya Mapenzi bali kwakua hawana namna wanaona kusubiri Mtu Sahihi watapishana na Kalenda.

*Badilika, haikufanyi Mwanaume zaidi kwa kumpotezea Binti wa watu Miaka Mitano halafu unamuambia* ```"Wewe si Type yangu"*``` Fanya jambo la Kiungwana na Malizaneni Mapema.

Lakini najua kuna Mabinti ambao hawasikii wakiambiwa kuwa mambo yameisha, Mlazimishe asikie na Usimtumie na Kumuumiza kwakua anakupenda.
 
Yeah unamwambia tuu dada naomba tuwe wapenzi mpaka utakapopata mtu sahihi wa kukuoa.
 
Kuna jamaa yangu mmoja muharibifu sana.
Alianza kudate na huyu mdada akiwa ndo anaota chuchu!
Kamchakaza karibu miaka 8 na mtoto juu akampatia!mwisho wa siku jamaa anapata mchumba mwingine huku anamwambia yule alietoka nae mbali"MI SASA HIVI NATAKA KUOA BIKRA NA NDOA MWEZI UJAO"
kiukweli yule mshkaji wangu nilimchukia sana kuanzia hapo.amempotezea muda mdada wa watu kazi ikawa kwangu kila siku nambeleleza huyu dada asijiue atulie tuu amwachie mungu.
 
Duu sio vizuri kabisa, halafu malipo huwa hapa hapa dunia wala si mbali, kaanza naye bado mdogo
mpaka mtoto kisha anamuacha sio kabisa hata Mungu hapendi
 
Kuna jamaa yangu mmoja muharibifu sana.
Alianza kudate na huyu mdada akiwa ndo anaota chuchu!
Kamchakaza karibu miaka 8 na mtoto juu akampatia!mwisho wa siku jamaa anapata mchumba mwingine huku anamwambia yule alietoka nae mbali"MI SASA HIVI NATAKA KUOA BIKRA NA NDOA MWEZI UJAO"
kiukweli yule mshkaji wangu nilimchukia sana kuanzia hapo.amempotezea muda mdada wa watu kazi ikawa kwangu kila siku nambeleleza huyu dada asijiue atulie tuu amwachie mungu.
Daaah kuna watu waharibifu sana wanajua kutumia wanawake na kubadili tu wanaona sifa
 
Back
Top Bottom