GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,570
- 108,911
Zipo sababu kedekede / nyingi ila hizi zifuatazo ndiyo sababu Kuu hasa baada ya kuzifanyia ' utafiti ' wa kina na wa muda mrefu wa kujua ni ' viashiria ' gani vikubwa vinavyoweza kukuambia kwamba Mwanaume fulani amerogwa ' Kimahaba ' na ama Mke au Mpenzi wake.
Nawasilisha.
- Unapenda sana kuwasema / kuwananga Ndugu zako pale unapokuwa nae.
- Unapenda mno kumuomba msamaha hata kama kiuhalisia Kosa ni lake yeye.
- Ndugu zake unawapa uhuru wote kuja Kwako ila wa Kwako unawapa masharti ya kuja.
- Mkiwa sebuleni Kwenu yeye ndiyo huwa mwamuzi wa Channel ipi / gani muiangalie.
- Akikuomba Hela / Pesa kiasi fulani Wewe ukitoa / ukimpa utamzidishia kile Kiwango.
- Ndugu zako wakimkosoa / wakimsema Wewe hugeuka ' Mbogo ' Kwao na unawachukia.
- Hupendi / Unaogopa kukagua Simu yake ila yeye ya Kwako ' anaidukua ' atakavyo 24/7.
Nawasilisha.