Kama Wewe ni Mwanaume halafu una hivi viashiria jua 100% umerogwa Kimahaba

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,528
Zipo sababu kedekede / nyingi ila hizi zifuatazo ndiyo sababu Kuu hasa baada ya kuzifanyia ' utafiti ' wa kina na wa muda mrefu wa kujua ni ' viashiria ' gani vikubwa vinavyoweza kukuambia kwamba Mwanaume fulani amerogwa ' Kimahaba ' na ama Mke au Mpenzi wake.

  1. Unapenda sana kuwasema / kuwananga Ndugu zako pale unapokuwa nae.
  2. Unapenda mno kumuomba msamaha hata kama kiuhalisia Kosa ni lake yeye.
  3. Ndugu zake unawapa uhuru wote kuja Kwako ila wa Kwako unawapa masharti ya kuja.
  4. Mkiwa sebuleni Kwenu yeye ndiyo huwa mwamuzi wa Channel ipi / gani muiangalie.
  5. Akikuomba Hela / Pesa kiasi fulani Wewe ukitoa / ukimpa utamzidishia kile Kiwango.
  6. Ndugu zako wakimkosoa / wakimsema Wewe hugeuka ' Mbogo ' Kwao na unawachukia.
  7. Hupendi / Unaogopa kukagua Simu yake ila yeye ya Kwako ' anaidukua ' atakavyo 24/7.
Hivyo kila Mwanaume aliyemo humu JF aziangalie hizo ' indicators / viashiria ' kisha tupeanae mrejesho hapa hapa kwamba ni nani zimemgusa 100% ili tuweze kumpa pole lakini pia kwa wale Wanaume ambao hawaingia katika huo ' mtego ' wa Kurogwa huko ' Kimahaba ' basi si vibaya pia nao wakasema hapa hapa ili tuweze Kupongezana.

Nawasilisha.
 
Inaweza kuwa kweli au sio kweli. Sio wote wenye viashiria hivyo wamelogwa ni nguvu ya mapenzi. Mapenzi yanafanya watu mazuzu, malofa n.k jaribu tu kuangalia mtu ambaye ameamua kujiua kwa sababu ya mapenzi vitu kama hivyo ni rahisi kuvifanya.
 
GENTAMYCINE samahani naomba ubadilishe font, hii font yako kwangu kidogo hainivutii, nashindwa kusoma fresh
posti zako.
 
GENTAMYCINE samahani naomba ubadilishe font, hii font yako kwangu kidogo hainivutii, nashindwa kusoma fresh
posti zako.

Katika Font style ninayoipenda ni hii na sijui kama itatokea siku nitakuja kuibadili. Sasa kama Font yangu inakutesa na huwezi kusoma imekuwaje umeweza kujua nilichokiandika na umekuja kutoa hilo ombi lako?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom