Mwanaume akikuomba vitu hivi vitatu jua hana mpango wa kukuoa

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,910
MWANAUME AKIKUOMBA VITU HIVI VITATU JUA HANA MPANGO WA KUKUOA

Katika mapenzi kila mtu ana watu wa aina mbili, aina ya kwanza ni ile ya watu wa kuzuga nao na kupotezea muda na aina ya pili ni ile ya watu ambao wanamipango ya baadaye kwa maana ya kuingia kwenye ndoa. Mara nyingi ni ngumu sana kugundua kwamba mpenzi wako anakupenda kweli au la (wewe ni wa kuzugia au wa ndoa)

Lakini kuna mambo ambayo mpenzi wako akikufanyia unajua kabisa hakupendi. Leo tujadili mambo matatu ambayo wewe mwanamke kama mpezi wako akikuomba jua basi hana mpango wa kukuoa. Hapa sisemi kwamba hatakuoa kabisa, hapana anaweza kukuo lakini kwa bahati mbaya kama mipango yake ikishindikana na si kwakua anakupenda.

(1) Kukuomba Mapenzi Kinyume Na Maumbile; Hii ni mada yenye ukakasi sana lakini kwa bahati mbaya nikuwa mabinti wengi siku hizi hutoa mapenzi kinyume na maumbile ili tu kuwashikilia wanaume. Sasa dada yangu kama unatoa kwakua wewe na wewe ni punguani tu unapenda ujinga huo basi endelea ila kama ni kupalilia ndoa basi acha.

Hakuna kitu ambacho kinatia kinyaa kwa mwanaume kama hicho, mwanaume mwenye akili atafanya kitu hicho huko nnje lakini si kwa mkewe. Hii nikwasababu anafahamu madhara yake, anajua baada ya muda misuli ya huko italegea na mke atalazimika kuvaa nepi. Sasa ingawa anapenda sana hiyo kitu ila bado anachukia kukaa na mtu ambaye wakati wowote anaweza kuchafua shuka.

Ukiona mwanaume kakuomba huo mchezo, kuna mambo matatu, kwanza nikwakua anataka kukuacha hivyo anakujaribu akijua kua kama una akili utakataa na atakuacha. Pili nikwakua hakupendi anajua kuwa hata akikuharibu hatakuoa atatafuta mwingine mzimaa wakuoa na wewe akuache uwe msala kwa fala mwingine.

Lakini jambo la tatu nikwakua ashakua addicted sana na hawezi kufanya mapenzi bila hivyo. Ubaya wa huyu nikuwa hata akikuoa baada ya muda wewe ukishaharibika unatia kinyaa basi atatafuta mwingine. Maana kama ni mkewe anakufanyia kila siku hata mwaka hutamaliza utakua ushaanza dozi ya nepi, kama una akili ushanielewa!

(2) Anakuomba Umzalie Kwanza: Huu mtego unabeba wanawake wengi sana, mwanaume amekuambia anakupenda labda kajitambulisha anakuambia tuzae kwanza na wewe unakubali. Mwanaume hukuambia uzae naye kwanza kabla ya kukuoa kwakua hana mpango wa kukuoa, anaona umri unaenda na yeye anahitaji mtoto.

Ukilogwa ukakubali basi jua atakutelekeza. Hii ndiyo maana wanaume wengi huwaomba wanawake amabo wana kazi, au wanatoka katika familia zenye pesa. Hapa anajua kuwa hata akikutelekeza basi mtoto wake hatapata shida kwani utamtunza vizuri. ni nadra sana kuona mwanaume anamuomba mwanamke ambaye hana kazi.

Anatoka katika familia duni na kila siku anamsumbua pesa za matumizi. Hivyo dada yangu ukikubali ujinga huu, sijui nizalie ndiyo nikuoe jua wewe ni shamba darasa lake, yaani anakutumia kujua yeye kidume lakini atakutelekeza. Ikitoke akakuoa basi jua ni kwa bahati mbaya kwamba amemkosa aliyemtarajia.

(3) Nikopeshe Ni Fanye Kitu Flani: Ndiyo mnaonekana kupendana sana, dada una kakazi au kwenu mko vizuri, mwanaume anataka kujenga au kununua gari. Anakuambie umkopeshe kiasi flani ili ajenge au aongezee anunue gari. Dada yangu jua wewe unaliwa, mwanaume anayekuambia hivyo ashajua kuwa unampenda saaana.

Huna akili wala malengo binafsi hivyo anaona akutumie kutimiza malengo yake. Mwanaume anayekupenda akitaka mfanye kitu kwa pamoja atakushirikisha akikuambia Baby kwanini tusinunue kiwanja, kwanini tusijenge, kwanini tusinunue gari, ingawa sikushauri ufanye hivyo na mtu ambaye si mumeo ila angalau huyo anakupenda.

Lakini kama akianza na nneo nikopeshe ndugu yangu hiyo ni kengele, hembu muambie nitakupa lakini hiyo nyumba muandike majina yenu wote, au gari kadi iwe na majina yenu na ikae kwako halafu utaona kuwa atasemaje. Hivyo Dada acha kujifanya unapenda umechanganyikiwa inawezekana hata kawakopa wengi hivyo hivyo na wote wanajua wanaolewa.

Utaniuliza kwanini nimetoa mifano yote hiyo mitatu nikwakua wiki hii tu nimekutana na kisa cha Dada kaachwa baada ya kutoa mwili kinyume na maumbile, mwingine kaachwa baada ya kupewa hata hajajifungua. Mwingine kamuongezea pesa jamaa kanunua gari na gari anakuta anaendesha mwanamke mwingine!

Tujadiriane vizuri tu jamani tusikashifiane
 
Back
Top Bottom