Zawadi ya Harusi: Benson Mwashinga, Mwandishi na mtunzi asiye na jina ila ubora wa kazi zake ni balaa

sing8

Member
Dec 7, 2017
12
6
ZAWADI YA HARUSI, Hii ni riwaya ya kusisimua na kuelimisha inayofuata ubora uleule wa ubunifu toka kwa mwandishi mbunifu inayomhusu msichana mrembo Josephine.

Licha ya uzuri aliokuwa nao Josephine lakini matatizo hayakumuogopa; amekumbana na matatizo mengi na magumu katika maisha yake. Siku ya kufungua zawadi zake za harusi ilikuwa ni siku mbaya sana kwake, baada ya mategemeo makubwa ya furaha ya kupata zawadi lakini ikawa kinyume chake, zawadi hiyo ilibadilisha furaha ya wanandoa hawa wachanga na kutengeneza jehanamu ndogo hapa duniani.

Zawadi hiyo ilifanya ndoa ya wanandoa hawa idumu kwa muda wa siku tano tu, na hatimaye zawadi hii ya harusi ikasababisha kifo cha wanandoa hawa. Unataka kujua ilikuwaje na iliendeleaje? Fuatana na mwandishi wako kurasa kwa kurasa, neno kwa neno ili uweze kujua mkasa mzima.


SEHEMU YA 01

Mara tu baada ya kutoka kuoga tukiwa kama tulivyozaliwa kwenye uwanja wa wapendanao, maandalizi ya mchezo ule usio na mwamuzi ukaanza. Elikunda alikuwa mtundu katika mchezo huu utafikiri anashahada ya juu toka katika chuo kikuu cha Harvard nchini Marekani.

Elikunda alikuwa anaufahamu mchezo huu barabara, alijua wapi pa kuanza na wapi pa kuishia, wapi ashike na wapi asishike. Kwakifupi alikuwa ni Christian Ronaldo wangu katika mchezo, kwasababu alikuwa anaujuzi wa hali ya juu kuzitingisha nyavu za timu pinzani.

Mechi nyingi za kirafiki tulizocheza, zilimfanya ajue udhaifu wangu ulipo, naye hakucheza mbali na sehemu hizo, hapo ndipo alipokuwa anachukulia ushindi na kuwaamsha mashabiki kushangilia magoli.

Baada ya maandalizi ya kutosha, yeye mwenyewe alipiga filimbi kuashilia muda mwafaka wa kuanza mechi umefika. Mimi nilijiweka sawa sawa kabisa kwani najua mchezo huu ni tofauti kabisa na michezo mingine, mchezo huu moja kwa moja unaanza na mikwaju ya penati, na wachezaji ni wawili tu, kipa na mpiga penati mpaka ushindi upatikane.

Penati zikaanza, Elikunda akaendelea kupiga penati huku mimi nikifanya kila niwezalo kudaka mipira iliyokuwa inatupiwa golini. Muda mfupi baadaye magoli yakaanza kupatikana, utamu wa ushindi wa magoli yaliyopatikana uliufunika mwili wangu mzima, nilijiona kama nipo katika mbingu ya kwangu mwenyewe, kelele za ushindi zilinitoka hata bila kuziruhusu.

Baada ya dakika kumi na tano za mikwaji ya penati nilisikia kelele za chini kwa chini za ushindi toka kwa Elikunda akiashilia goli kupatikana, huku wazungu wake wakitoka nje ya lango kuashilia mwisho wa mchezo. Kwa pamoja tulishusha pumzi nzito huku mioyo yetu ikiwa imeridhika na suluhu iliyopatikana katika mchezo, kwani wote tulikuwa washindi wa mchezo, kitu kilichotupa wasaa wakutafuta usingizi mwanana.

Ilipofika saa saba usiku, niliamka, nikamwangalia mpenzi wangu Elikunda, taratibu nikashuka kitandani nikaenda jikoni, nikachukua kisu kikubwa, nikaingia nacho hadi chumbani nikiwa nimekificha mgongoni kwangu. Nilipofika karibu na kitanda, nikamwangalia tena mpenzi wangu Elikunda, nikajisemea moyoni mwangu 'Sasa zamu ya kulipiza kisasi imefika, Elikunda nilikupenda sana lakini kwa hili, lazima nilipize kisasi, lazime uende huko ahela ukamuombe msamaha mume wangu.

Nimekudanganya na penzi langu nililokupa leo ili isiwe kazi kutimiza adhma yangu ya kukuua, nashukuru na wewe umeingia mwenyewe kwenye kumi na nane zangu”

Nilifumba macho yangu, nikainua kisu juu, nikakishusha kwa nguvu kubwa utafikiri napasua kuni, nikamchoma na kisu kifuani, shingoni na tumboni mara nyingi mpaka hasira zangu zilipoisha. Nilimuona Elikunda akikoroma huku akitoa maneno ya mwisho kabla roho haijamtoka.

Kelele za kulalamika nisimuue zilisikika toka kwa Elikunda, lakini kutokana na hasira na chuki kubwa aliyoipandikiza ndani ya uvungu wa moyo wangu ilinifanya nishindwe kumuonea huruma. Damu nyingi ilimtoka ikasambaa kitanda kizima, chumba changu kikawa kama sama sehemu ya machinjio ya ng’ombe, baada ya dakika chache mauti ikamchukua mpenzi wangu, niliyemchukia kuliko kitu chochote duniani.

Nilijisemea moyoni mwangu, “Pamoja na utamu wako kitandani, ila kwa hili ulilonifanyia! Nenda salama mpenzi, nenda salama na utamu wako, ngoja na mimi niitoa roho yangu ili tukakutane wote huko ahera, kwani maisha hapa duniani hayana thamani tena”

***********************************

Siku tano toka Josephine afunge ndoa takatifu katika kanisa la Lutherani jijini Dar es Salaam, ikiwa imeshuhudiwa na maelfu ya watu, ndoa iliyokuwa ya kifahari mithili ya ndoa ya kifalme katika moja ya falme zenye nguvu hapa duniani. Sherehe za ndoa hii zilitumia pesa nyingi kufanya ifanikiwe kwa mafanikio makubwa kiasi kile. Watu walikunywa na kula kadri walivyoweza, magari ya kifahari yaliyokuwa na picha za Julius na Josephine yalionekana yakitapakaa kila kona ya jiji la Dar es salaam.

Waendesha bodaboda karibia wote wa jijini Dar es salaam walipewa vitambaa vyenye rangi ya blue na nyeupe vilivyokuwa na picha ya Josephine na Julius wavifunge kwenye pikipiki zao wakipeperusha huku wakizunguka mji mzima.

Helcopter mbili zikiwa zimefungwa kitambaa kikubwa kilichoandikwa maandishi makubwa, HARUSI YA JULIUS NA JOSEPHINE, vilikuwa vikipeperushwa angani. Ilikuwa kama siku ile iliyotabiliwa ya kuja mwana wa Adamu Yesu kristo, kwani kila mtu aliyekuwepo ndani ya jiji la Dar es salaam siku ile alijua juu ya harusi hii ya kifahari.

Lakini kitu cha kusikitisha ni kwamba ukubwa wa ndoa hii, haikuwa tiketi ya kuukwepa msemo usemao “ndoa ndoano” kwani siku tano baada ya kufungwa kwa ndoa hii takatifu; ndoa hii iliingia doa sugu, tena doa jekundu kubwa kwenye shati jeupe halafu likiwa kifuani. Doa hili liliingia siku ile walipokuwa wanafungua zawadi zao za harusi mara tu baada ya kutoka kwenye fungate katika nchi ya Ufaransa.

Ndani ya boxi mojawapo kati ya maboxi ya zawadi walikuta picha za uchi alizopiga Josephine na mwanaume wake wa zamani siku moja kabla ya harusi, picha ambazo zilipigwa kwa ustadi mkubwa kwani zilionesha karibu kila kitendo cha kimapenzi kilichokuwa kinafanyika ndani ya faragha na yule mpenzi wake wa zamani.

Picha hizo zilionesha kwa uwazi kabisa mikwaju ya penati jinsi ilivyokuwa ikipigwa, na baya zaidi mikwaju mingine ya penati ilikuwa inapigwa kwa nyuma, lakini kwasababu mpigaji wa mikwaji hii yeye mwenyewe ndiye alikuwa mwamuzi, aliyakubali magoli hayo kuwa magoli halali.

Bwana harusi alichanganyikiwa akaanza kuongea hovyo hovyo mwenyewe, wasimamizi wa ndoa ile nao walichanganyikiwa, Josephine naye alibaki akiwa ameduwaa, mdomo ukiwa wazi, asijue afanye nini.

Mara baada ya muda mfupi picha hizo hizo zikaanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, marafiki wa Josephine, marafiki wa bwana harusi, kaka zake, wafanyakazi wenzake, majirani ndugu wa mume wake na karibia kila mtu ndani na nje ya Tanzania aliyekuwa kwenye mitandao ya kijamii alifanikiwa kuona zile picha.

Picha hizo zilileta gumzo kubwa hapa nchini kwetu Tanzania, sio maofisini tu bali hata vijiweni walikuwa wakijadili picha hizo za aibu.

Zilikuwa ni picha za aibu ambazo hakuna mtu aliyeziangalia akashindwa kusikitika, na kutoa matusi na laana kwa mhusika. Baada ya hayo yote kuzagaa kila kona ya nchi, ndipo Josephine kabla ya kuitoa roho yake aliamua kuandika maelezo marefu yanayoelezea juu ya mkasa mzima ulivyokuwa na historia ya maisha yake.

**********************
Baada ya picha zangu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kufikia mahali hakuna hata mtu mmoja anayenielewa ninavyojitetea na kuomba msamaha, wazazi wangu, marafiki na mume wangu wameshindwa kabisa kunielewa na hawaoneshi dalili zozote za kunisamehe.

Kila anayenipigia simu ananitukana nakunilaumu utafikiri namiliki kikundi cha magaidi na nimefanya tukio kubwa la kuangamiza watu kwa kutumia bomu la nyuklia, kumbe nilikuwa ni mkosaji ambaye nahitaji msamaha na vile vile nahitaji angalau mtu mmoja wa kunifariji kipindi hiki cha matatizo makubwa.

Nashindwa hata kutoka nje, dunia naona ndogo kama kasha la kibiriti; sioni thamani ya maisha tena, naona giza totoro mbele yangu likiwa limenisonga, dalili ya kuiona asubuhi yenye matumaini imetoweka katika fikra zangu. Nimeshindwa kupata nguvu ya kuhimili kishindo kikubwa namna hii cha matatizo, matatizo yamekuwa mzigo mkubwa usiobebeka.

Nimeshindwa kujua hatma ya maisha yangu, hivi nitawaangaliaje wafanyakazi wenzangu, wazazi wangu, majirani na marafiki? Hivi jamii inayonizunguka itanionaje? Haya ndiyo yalikuwa maswali yangu makubwa yaliyokosa majibu. Baada ya kutafuta suruhisho la matatizo haya bila mafanikio, suruhisho moja na la pekee ambalo ndio jibu la maswali magumu ninayojiuliza, jibu rahisi kwa maswali yote hayo hapo juu ni “Bora Nife” kujitoa roho yangu ili niweze kuiepuka aibu hii.

Kabla sijajitoa roho yangu ili niepukane na aibu kubwa namna hii, napenda kuwasimulia angalau kwa ufupi historia ya maisha yangu ambayo itakuwa fundisho kwa mwanadamu yeyote anayeishi hapa duniani ili na yeye yasije yakamkuta yaliyonikuta.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka thelathini, nilizaliwa huko mkoani Mbeya na kusoma shule ya msingi hadi kidato cha nne katika wilaya ya Rungwe kabla ya kwenda Songea girls huko mkoani Ruvuma kwa masomo ya kidato cha tano na cha sita. Baadaye nikajiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo nilisomea shahada ya kwanza ya uchumi.

Baada ya kumaliza masomo yuangu, mwaka mmoja baadaye niliamua kwenda mjini Moshi nikajiunga na mafunzo ya polisi, mara baada ya mafunzo hayo nikaajiliwa kama askari polisi ndani ya jiji la Dar es salaam.

Nilifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka mitatu, baadaye bosi wangu akanipa barua ya kwenda masomoni kusomea kazi maalumu ya upelelezi, kitengo nilichokuwa nakichukia kama ninavyomchukia shetani, lakini ilinibidi kwenda kusoma kwasababu ilikuwa inamanufaa makubwa sana kwa taifa, na mimi wakati wote taifa kwanza halafu mambo mengine baadaye. Mafunzo yalikuwa ni ya miezi tisa, nilipomaliza nikarudi tena kazini.

Siku moja nikiwa ofisini kwang alikuja mtu mmoja ambaye alijitambulisha anaitwa Hosea. Ujio wake ulinishangaza, kwani nilipomuona tu moyo wangu ulishikwa na butwaa, ilikuwa kama mtu aliyeona jini mbele yake tena nikiwa katikati ya bahari tena usiku wa manane kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa Yesu walipoona mtu anatembea juu ya maji wakatetemeka.

Kijana mtanashati, umbo lake lilikuwa ni lile ambalo kila siku nilikuwa naota nije nipate mwanaume wa aina ile. Moyoni mwangu nilijisemea, "oooh! Mungu wangu, huyu ndiye mwanaume wa ndoto zangu"

Baadaye nilimkaribisha huku nikiwa namuangalia usoni utafikiri mtu anayeangalia filamu inayotisha lakini hataki kuzima runinga. "Karibu"Nilimwambia "Asante sana dada yangu" Alinijibu, sauti yake ilinifanya niangalie chini, kwani ilikuwa sauti nzito halafu kama anakunongoneza vile, ilikuwa si sauti ya kumtoa nyoka pangoni tu bali kuvuruga pango zima na kuwatoa wadudu wote ndani ya pango.

Mawazo mengi yakaingia kichwani mwangu, nikaanza kuwaza akiwa mme wangu itakuwa vizuri, nitakuwa mwanamke mwenye bahati. Nitakuwa naisikia sauti yake kila siku, hasa pale akipiga hodi anapokuwa ametoka kazini, anapokuwa ananiita jina langu. Nikiwa kwenye mawazo ambayo yalinifanya hata nichelewe kumuhudumia nikasikia sauti.

"Samahani dada nilikuwa namuulizia afande God?" Aliuliza yule kaka. "Afande God hayupo aliondoka kikazi toka jana, hayupo kazini kwa sasa"Nilimjibu. "Unadhani atarudi lini?" Aliuliza "Kesho au kesho kutwa" Nikamjibu. "Asante sana dada yangu, basi nitakuja kumuungalia keshokutwa" akamalizia.

"Kwani ulikuwa unashida gani? Siwezi kukuhudumia mimi?” Nilimuuliza ili niendelee kusikia sauti yake nzuri na kutengeneza nafasi ya mawasiliano zaidi. "Asante dada yangu, tulikuwa na kazi tumeianza hivyo nilimtaka yeye ili tumalizie" Alijibu. "Sawa, basi uje siku hiyo ambayo umesema utakuja" "Asante na kwaheri, tutaonana kesho kutwa Mungu akijaalia" Aliniambia huku akifungua mlango na kuanza kuondoka.

Kijana huyu alinichanganya kama mama mpika maandazi anavyochanganya unga wa ngano. Kazi niliyokuwa naifanya nikaiacha, nikasimama nikafungua dirisha nikaanza kumuangalia kupitia dirishani. Ilikuwa rahisi kumuona kwani ofisi yangu ilikuwa ghorofani. Nilimuangalia alipokuwa akiingia kwenye gari na baadaye akaondoka.

"Mimi mjinga, sina akili, kwanini sijachukua namba zake za simu? Ningechukua namba za simu ingekuwa rahisi kuwasiliana naye" Nilijikuta nikisema maneno hayo kama kichaa aliyeokota pesa badala ya makopo, lakini nilikuwa sina namna ya kufanya ikanibidi niendelee kubaki na mzigo mkubwa wa majuto na masononeko moyoni mwangu, kitu kilichonifanya nishindwe hata kufanya kazi, nikaamua kwenda nyumbani nikapumzike.

Niliomba ruhusa nikaenda nyumbani kwangu; nilipofika nyumbani moja kwa moja nilienda chumbani kulala. Nikiwa kitandani sikupata usingizi, muda wote sura ya yule kaka iliendelea kuja usoni na kwenye akili yangu, aliuteka moyo wangu kwa mitutu ya silaha kama book haramu.

Ilipofika saa moja jioni niliamua niende sehemu nikapunguze mawazo kwakupata moja baridi moja moto kwenye bar iliyokuwa jirani na nilipokuwa naishi.

Nilipofika pale bar nilishangaa kumuona kaka mtanashati aliyenichanganya kichwa changu asubuhi kule kazini. Ghafla furaha isiyo kifani ikanijaa moyoni mwangu, tabasamu ya bei mbaya ikanitoka mdomoni mwangu, mwili wangu ukasukumwa na akili yangu kwenda jirani na yule kaka.

Miguu nayo haikuchelewa kusimama na kuanza kutembea kuelekea pale alipokuwa amekaa yule kaka. Sauti yangu nayo haikugoma wala kukwaruza, sauti ya mahaba na mdomo uliojaa tabasamu kama mlimbwende aliyeshinda taji la mlimbwende wa dunia ikanitoka, nikamsalimu.

"Kaka mambo vipi?" "Poa vipi mrembo?" Alinijibu "Safi sana kaka yangu, unanikumbuka?" Niliuliza hivyo kwasababu jinsi alivyonijibu ilionekana kama hanijui mpaka nikahisi ya kwamba nimemfananisha. " Hapana dada yangu naomba unikumbushe tulikutana wapi?" Aliniuliza.

"Leo asubuhi ulikuja ofisini kwetu ulikuwa unamuulizia afande God, ulinikuta mimi nikakuhudumia" Nilijaribu kumuelezea kwa ufasaha kadili nilivyoweza. "Ahaaa! Nimekumbuka, mambo vipi?" "Poa sana kaka yangu" Nilimjibu huku moyo wangu ukiwa umeongezewa furaha isiyo na kifani.

Alinikaribisha kwenye kiti chake akaagiza vinywaji tukaanza kunywa huku mazungumzo mawili matatu yakiwa yanaendelea. Kila dakika iliyokuwa inapita nilikuwa najaribu kuonesha ishara ya upendo wangu kwake, kitu ambacho kilimfanya agundue kuna kitu kilikuwa kinanisibu na kitu hicho sio kingine bali ni upendo wa kimapenzi kwake.

Tulikunywa vinywaji mpaka tukaridhika, ilipofika saa nne na nusu usiku aliniambia, " Vipi? Tunaweza tukaenda wote?" "Twende wapi?" Nilijua lengo lake lakini sikutaka kumrahisishia jibu haraka haraka, sikutaka anione mimi ni wa bei ya kitumbua.

"Twende zetu tukaipe miili yetu raha ya dunia, starehe iliyotoka mbinguni, starehe ya akili, moyo na mwili" "Ni wewe tu, mimi kwako nimeoza mpaka nanuka, na kama ni nyama sasa imeisha iva na kupakuliwa tayari ipo mezani ni wewe tu kuila, tena si kwa kijiko wala uma ni kwa mkono wako mwenyewe tena utakavyo”

Nilimuhamasisha kwa maneno ya kimahaba huku mwili wangu nikionyonganyonga kama kinyonga, kwani uzalendo wa kuendelea kuvunga vunga uliniisha ghafla, niliogopa kujifanya sitaki halafu nikakuta mwana sio wangu.

Dakika kumi baadaye tukaanza safari ya kwenda kwenye nyumba ya kulala wageni. Moyoni mwangu nilijiona msichana mwenye bahati kubwa kumpata kijana mtanashati na mwenye mvuto mkubwa kwa mwanamke yeyote ambaye anaishi hapa chini ya jua.

Mwanaume aliyejua kuvaa vizuri na kwenda na wakati, mwanaume aliyekuwa na sauti nzito lakini yenye mvuto, si mwembamba wala si mnene, mwenye kitambi kidogo kiasi cha kumsaidia kufuta simu ya smartphone.

Nywele zake alijua namna ya kuzitengeneza vizuri utafikiri anashinda kwa kinyozi kila siku, bila kusahau tabasamu yake anayoitoa mara chache sana lakini akiitoa lazima mwanamke yeyote aliye mbele yake ataijibu kwa tabasamu iliyochanganyika na kicheko, kama sio mubashara basi ataijibu kimoyomoyo. Kama robo saa hivi ya mwendo wa gari alisimamisha gari akaniambia,

“Mpenzi; Tayari tumefika Amani Kwanza Lodge”
“Kumbe sio mbali, kwahiyo hapa panaitwaje?” Nilimuuliza lakini hakunijibu lolote, akashuka toka kwenye gari akazunguka kwenye upande wa mlango wangu, akanifungulia mlango wa gari akanishika mkono taratibu akinisaidia kushuka toka kwenye gari huku na mimi nikishuka taratibu kwa madoido.

Alipokuwa ananifungulia mlango na kunishusha toka kwenye gari, nilijiona kama malaika aliyeshushwa toka mbinguni na kukutana na mwana wa Mungu akinipokea. Nilijiona mke wa mfalme mwenye himaya kubwa kama ilivyokuwa Uingereza kabla ya vita vya pili vya dunia.

Niliposhuka tu chini nilishikwa na butwaa nikafikiri nipo kwenye ndoto au naangalia filamu ya kininja. Kwani niliona watu waliokuwa wamevaa nguo nyeusi mpaka usoni na huku wakiwa wameshika mapanga marefu. Mara nikasikia sauti ikiniamrisha "Kaa chini" Mwili wangu wote ulilowa jasho jembamba huku mkojo ukigongagonga kutaka kutoka.

Nilimsogelea mpenzi wangu ili kupata msaada, naye akanipiga teke nikaanguka chini huku wale watekaji wakiwa wamenizunguka. Sikuamini macho yangu kwamba mtu niliyemuona mtanashati, mpole na aliyekuwa amejaa na sura ya kumtumainia, kumbe alikuwa ametumwa kwa kazi moja tu, kazi ya kuniteka.

“Umdhaniavyo mtu kumbe sivyo”, pia wahenga walisema, “sio kila kitu kingaacho ni dhahabu” Nilijiuliza nilipewa nini mpaka nikatokea kumpenda mwanaume huyu ghafla! kumbe alikuwa na ajenda ya kuniteka! Lakini waswali hayo yalikuwa hayana nafasi kwa wakati ule.

"Sogea hapa malaya wa kichina wewe" Nilisikia sauti iliyosindikizwa na teke mgongoni kwangu, nikasogea mbele bila kupenda. Mara nikasikia tena sauti wakisemezana, "Hebu mfunge kamba mikono na miguu"Wakaanza kunifunga kamba miguuni na mikononi mwangu, machozi na kilio cha kuomba wasinifanyie kitu kibaya kilinitoka lakini ilikiwa haina nafasi ya kusikilizwa.

"Wewe mwanamke unajifanya unajua kufanya kazi kuliko wote pale ofisini, wapo wanaojua kufanya kazi lakini hawapo kama wewe. Hebu sikiliza wewe malaya uliyekubuhu; kama utatuambia mafaili ya kesi ya uchunguzi wa muwekezaji wa pale mkoani Mbeya, juu ya kesi ya mauaji uliyokuwa unayafanyia upelelezi yapo wapi?

Ukitusaidia kuyapata sisi hatutakufanya chochote, bila kufanya hivyo basi roho yako ni mali yetu, na tutakuchinja kama kuku na nyama yako tutaichoma mishkaki na kuila"

"Jamani! Mbona sina nyaraka hizo, niliisha peleka tayari kwa bosi" Niliwajibu. " Wewe naona hutufahamu, Jere hebu mpe chai bila kitafunwa" Mmoja wao aliongea ila sikujua chai hiyo ni ya namna gani isiyo na kitafunwa, ila nilihisi kwamba itakuwa nikipigo.

Dakika tano hivi nikiwa nimefungwa, akaja dada mmoja akiwa ameshika mijeredi na kuanza kunichapa, alinichapa bila huruma mpaka nikahisi ngozi yangu inanyofoka. Fimbo ziliendelea kushuka mngongoni kama mbwa mwizi apigwavyo, nililia kwa uchungu lakini hakutaka kuniacha.

Maneno yake yalikuwa "kama hutatoa ushirikiano ili tuweze kupata nyaraka zote za ushahidi basi wewe ni halali yetu" "Jamani naombeni mniache nitawasaidia kupata" Niliwaomba. "We mwanamke sema nitawaletea!! au unafikiri sisi hatujui chochote?" Ilikuwa ni sauti nyingine ya kiume iliyotoa maneno hayo. Nilishtuka kwani ilikuwa ni sauti ya mtu ninayemfahamu vizuri tena tunafanya naye kazi pale ofisini, si mwingine bali ni Afande God.

“Hahahaa! God! Ni wewe au ninaota! Na wewe umejiingiza kwenye kundi hili la watekaji!" Niliuliza kwa mshangao mkubwa. "Sikiliza Josephine, mimi sio mtekaji bali nipo hapa kumsaidia muwekezaji ili asiingie kwenye hukumu iliyopo mbele yake, kuna watu watatu ambao tunaweza kumsaidia, ambao ni wewe, bosi wetu mr. Daudi na mimi.

Wote sisi wawili yaani mimi na mr Daudi tumekubali kumsaidia muwekezaji ila tatizo limebaki kwako" Aliongea kwa upole lakini kwa uhakika akaendelea kusema. "Josephine! Nilikwambia mara kadhaa tumsaidie muwekezaji, na walituletea ofa kubwa ya milioni ishilini kila mmoja lakini wewe bado ulikataa.

Sasa nakuomba ufanye kitu kimoja, sisi tunataka ukubali wako wa kwenda kubadilisha zile nyaraka ili tutakapofika mahakamani ushahidi ukosekane wa kumuweka hatiani muwekezaji yule" "God, kweli wewe upo tayari kuuweka uzalendo wako kando! kipo wapi kiapo ulicho apa cha uadilifu?

Huu ndio uadilifu? Kwanini unaweka pesa mbele kuliko uadilifu? Kama vifo vya watu masikini wasio na hatia vinatokea katika nchi yetu na sisi ndio tunatakiwa kuwa watetezi wao, lakini sisi ndio tunakuwa wa kwanza kuwasaliti kwa ajili ya pesa!

Kweli pesa mwanaharamu" "Josephine sikiliza! Wazazi wako walikusomesha ili uje upate pesa, unafikiri hapa mjini wafanyakazi wote wangekuwa kama wewe wangeweza kujenga nyumba za kifahari! Wangeweza kununua magari ya kifahari, tunayoyaona yametapakaa kwa wafanyakazi wa serikalini namna hii! Hapa mjini ofisi uliyonayo inatakiwa ikusaidie wewe kupiga dili za maana ili mambo yako yote yaende shwali"

"Mr God sikiliza; mimi sipo tayari kufanya hilo unalotaka nilifanye, bora kupoteza kazi lakini siyo kujiingiza katika ushetani wa namna hiyo" "Josephine nakupenda sana sitaki mabaya yakupate ila ninachokuomba wewe ni kitu kimoja tu, ukubali kutusaidia ombi letu, ukishindwa kufanya hivyo basi roho yako itatenganishwa na mwili wako.

Hawa unaowaona hapa wamelipwa na kazi yao ni moja tu, kutoa uhai wa watu wabishi kama ninyi, mimi ngoja niende zangu nikuache ufikiri kwa mda" Aliongea God kwa msisitizo. "Siwezi kuusaliti moyo wangu na kiapo changu cha uadilifu, kifo sikiogopi, kwani waoga wote wa kifo hawawezi kuwatetea wanyonge, hata Yesu Kristo ilimbidi afe ili kumuokoa mwanadamu toka kwenye dhambi"Nilimwambia God.

"Wewe mwanamke unajifanya unakiburi, sasa tunakupa siku tatu za kujitafakari. Utakaa hapa kwa muda wote huo halafu siku ya tatu tutafikia mwafaka kati yetu na wewe" Alisema mmoja wa wale watekaji ambaye alijificha sura yake asijulikane.

Walinichukua wakanipeleka kwenye chumba kilichokuwa na giza na harufu mbaya. Nilikaa kwenye kile chumba kwa muda wa siku zile tatu nikajiona kama nimekufa vile, nilijiona kama nipo kaburini. Nilitafakari maisha yangu ya nyuma, nilimwomba Mungu anisamehe dhambi zangu kwani nilijua mwisho wa maisha yangu umefika


.............. Itaendelea..............
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom