Tupe proof ya ulichokiandika mtoa uzi
Umesema nitoe
proof. Biblia ndiyo ushahidi wangu, mkuu. Kama huiamini Biblia, basi tayari umejifunua kama mmoja wa wale niliowataja kwenye mada—wale ambao wamejitoa kupinga Injili kwa nguvu za giza na hoja za kipagani.
Nimesema shetani anapotosha watu kwa mafundisho ya uongo—
yes, and the proof is biblical.
1 Timotheo 4:1 —
“Basi Roho asema waziwazi ya kwamba katika nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.”
Nimesema shetani anawatumia wasomi na waandishi kupinga Neno la msalaba.
1 Wakorintho 1:18 —
“Maana neno la msalaba ni upuzi kwa hao wanaopotea; bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.”
Nimesema shetani anawashawishi vijana waamini eti Mungu hayupo.
Zaburi 14:1 —
“Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu.”
Nimesema shetani ni kama simba azungukaye akitafuta mtu wa kummeza
1 Petro 5:8 —
“Adui yenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka akitafuta mtu apate kummeza.”
Nimesema shetani alitupwa kutoka mbinguni.
Ufunuo 12:9 —
“Yule joka mkubwa akatupwa chini, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa chini hata duniani, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.”
Nimesema shetani anajua muda wake uliobaki ni mchache.
Ufunuo 12:12 —
“Ole wa dunia na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”
Nimesema Yesu atawachukua waaminio na hakutakuwa na muda wa kutubu.
1 Wathesalonike 5:2-3 —
“Kwa maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana huja kama vile mwivi ajavyo usiku… ndipo uharibifu utakapowajia ghafla.”
Sasa, ndugu yangu, nimekupa
proof ya nilichokiandika. Ukikataa ushahidi huo, sio kwamba umenikataa mimi, bali umekataa Neno la Mungu. Na kama huamini Neno hilo, basi ni wazi:
wewe si mtafutaji wa ukweli, bali ni ajenti wa shetani.
Mpaka hapo bado unatafuta tu ushahidi au unataka kutubu?