Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kiranga acha Kuyafanya maisha yako yakawa magumu humu Jf kwa kuwa na mitazamo ya aina hiyo kuhusu hoja zako watu wengine humu JF.
Najua watu hatufanani uwezo wa kufikiria sababu ya vitu vingi kama elimu, mazingira tuliyokulia , lishe n.k

Kama kitu haukijui au hauamini kama kipo basi anzisha uzi, watu watakuja na kukusaidia kukijua na ukiona bado haujaelewa na hauamini hilo jambo basi acha ili watu wanaojua au wanaamini hilo jambo waendelee na Imani zao.

Nimeandika hivyo sababu hoja zako zinakejeli, dhihaka , dharau n.k kuhusu hoja za watu wengine hasa hoja unazoona zipo tofauti na unachoamini wewe na kufikiria,

unatakiwa ujue kwamba duniani watu wote hatuwezi kuwa Sawa kwa kila kitu hivyo mada ambayo haikuhusu achana nayo ili maisha ya watu wengine yaendelee

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini unafikiri nayafanya maisha yangu kuwa magumu?
 
Sipo kubishana na wewe,
unaniuliza maswali ya kitoto ili nikujibu halafu tuanze kubishana?

Nimekwambia soma vizuri post yangu ya kwanza uliyo ni quote utaelewa, je baada ya kusoma ile post sehemu gani haujaelewa?
Hakuna ulipoeleza sababu ya wewe kufikiri nayafanya maisha yangu kuwa magumu.

Nataka unieleze kwa nini unafikiri nayafanya maisha yangu kuwa magumu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo Kunduchi kuna ng'ombe zipo zinajifuga zenyewe na kuna siku nimetoka zangu kwenye mishe zangu saa nane kasoro ivi napishana na ng'ombe inaenda home aisee. Na hizo ng'ombe mtu hazigusi maana zinahusishwa na kusomewa albadiri kwa sababu inasemekana ziliibiwa kumbe zilipotea zenyewe kwa hiyo atakayezichukua cha moto kitampata.
Hata kipindi cha nyuma tanga kulikuwa na mbuzi walipoteaga mwenye nao akajua wameibiwa basi akawasomea "albadiri" baadae akawaona akaambiwa awaache asiwachukue laasivyo albadiri yake itamzuru basi akawaacha

Aisee wale mbuzi walizaliana sana na walikuwa wakitembea kwa kundi wanazurura tu usiku utakapowafikia wanalala hapohapo na walinona kwelikweli wakionekana wanapita mtaani utaskia watu wanaropoka njooni muwaone wale "mbuzi wa albadiri " hakuna mtu aliethubutu kuwaiba huo msemo ukawa maarufu ulitumika mfano mtu anaweza akakutukana tu mfano mbuzi wa albadiri wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu nakumbuka enz nasoma primary kila tukienda chooni tunaskiaa harufu za pilau au vitu vinanukia vzr. Bhs nakumbuka siku rfk angu alirud speed class mpaka kuanguka kuuliza alisema kakuta sinia la pilau choon, watu wanamwambia njoo ule


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
sababu ya kiwasha ganja kabla sijalianza pori la ushirombo.

ilikuwa mwezi wa ramadhani mwaka 2013 mida ya saa 11 jion na siku hiyo kulikuwa na mvua ya rasha rasha, nilikuwa naendesha pulling ya kampuni moja ya mafuta na hilo gari sikuwa nimekabithiwa mimi dereva wake alipata udhuru ambaye pia ni mjomba wangu na kwa kuwa yeye ndiye aliyenifundisha gari akachukua chuma akaja nayo mpaka river side akanikabithi gari yeye akaenda kwenye mambo yake, mimi nikashobokea dundo nikaomba dua mdogomdogo, ikumbukwe hata lesen yangu wakati huo haikuwa ikiruhusu nikokote lile gari ni ubishi tu wa kibongo, basi kufika mji mmoja unaitwa masumbwe ile gari ikaanza mapicha picha inachemsha hatari, nikawa nalikokota hivyo hivyo temp ikishuka safar inaendelea, sasa ktk lile pori chuma ikaanza kuchemka tena, nikashuka chini nikawa naisubiria ipoe niwahi runzewe nikafturu nilikuwa nimefunga ila ni zile funga za masela c unajua tena? sasa nimemaliza kujaza maji nikasema ngoja nichungulie feni nikakuta chuma inataka kuanguka, na pale porin nikaona hapa nikijikokota nafika runzewe, naingia ndani ya gari fresh ile chuma inaanza ondoka dah naona mdada anatokea nyuma ya kitanda, nilistuka nusu niruke sasa akili ingine ikanikatalia kufanya hivyo, nikamuuliza we umeingia saa ngapi humu? huku sasa napaki gari pemben akaniambia ukipaki tu hii gar inawaka moto, ****** alafu mle ndani ya gari harufu imebadilika kuna marashi yanakera ndani ya pua zangu, sasa kuna jambo liliniponza mimi dini yetu inasema wakati wa mwez mtukufu viumbe vya ajabu vinafungiwa huyu katoka wapi? katoroka? nikakumbuka nna ganja tena ishanyongwa nilikuwa nasubiri nifungulie niilipue, ikabidi nifuturu bangi nikapandisha vioo ananiangalia tu ananichekea mm jasho linanitoka na vile sikula tangu asubuhi na mwili nauhisi unaisha nguvu akasema we mtoto usiwashe hayo majani mimi nikabana usukani na goti nikawasha alafu nikampulizia ule moshi, hamkuwepo ila nahisi nilikuwa na malaika maana mle katika cabin ulitanda moshi mzito na kelele ambazo sijui mpaka leo niseme ni za mnyama gani, hapo chuma inatembea maana nilihisi giza likiingia niko ma lile dubwana basi ndio kifochangu baada ya ule moshi kutanda mm nilichochora, chuma ikatoka nje ya barabara lakini nashukuru sikuingia kule kwenye ule msitu, wakati gari imesimama mle ndani moshi umejaa kama cabin inaungua, nikashuka nikaacha mlango wangu wazi ule moshi ukawa unatoka hapo natetemeka sasa nikakimbilia barabarani, chuma nimeiacha kule ktk njia ambayo ilikuwa diversion zaman, nimesimama pale kama dakika kumi hakuna gari hata moja kupita, hapo ganja yangu imebak kikucha, nikasema ngoja niende ktk gari nikaangalie yupo? hapo eneo lile lishaanza kuingiwa na ukimya na giza, narudi kule sikumkuta, hali ipo shwari kabisa, nikaizunguka gari kuikagua kama kuna janga lolote nimesababisha hamna, nikapanda nikaihakiki gar yote na nikaridhia niko mwenyewe chuma ikatoka huyoo mpaka runzewe nimeingia pale kama saa moja na robo sasa kilichonifanya niandike hapa ni hiki wakat nimefika runzewe nikapaki jiran ya mzee mmoja anauza kahawa, maana bado nilikuwa na wasiwasi nilitaka niwahadithie lile tukio nijue yule ni jini ama wenge la lile gari kabla sijashuka namuona yule mwanamke upande wa pili anaomba lifti katika gari ya Azam ambayo inarudi kule kule tulipotoka alaf tayar giza limetanda, nilipiga honi nikamwambia kaka usimpakie huyo mwanamke jini huku nashuka basi yule dada hata sijui alipoteaje lakini baada ya mm kuvuka nikamuambia kaka ungempakia yule mwanamke yangekukuta makubwa ananiuliza mwanamke gani? jaman si huyo ulikuwa unaongea nae hapa anakuomba lift? jamaa akasema yeye hajaongea na mtu katoka kula anaondoka zake nikamwambia basi kaka we lala hapa ondoka asubui hapa leo kuna jinni kisirani sio bure, ndio baada ya kuwahadithia wenyeji wakasema nyie mnabahati sana, kuna mwanamke jinn hapo ktk hilo pori, nikauliza lakin mwezi huu wanafungiwa wenyeji wakaishia kucheka tu.
 
Back
Top Bottom