Je,Umewahi kupata kipigo toka kwa kaka zake na mpenzi (demu) wako bila kosa kwa wivu tu wanakufungia ndani kwao wanakupinga kama Mbwa?

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Shalom,
Nimekumbuka hii story ya siku nyingi sana mtoto mmojawapo wa marehemu Advocate na pia Mwalimu Masumbuko Lamwai, alikuwa na demu wake mmoja hivi kitambo sana miaka 21+ hivi nyuma.

Huyu kijana wa Lamwai alikuwa na demu ambae huyo demu alikuwa na kaka zake kadhaa, kuna siku mtoto wa Lamwai alimtembelea mpenzi wake kwao, inaonekana kwa siku nyingi hao kaka wa huyo demu walikuwa na pingamizi ya huyo dada/mdogo wao kutoka kimapenzi na mtoto wa kiume wa Lamwai.

Basi inatokea siku hio mtoto wa Lamwai alifika nyumbani kwao na demu wake, basi kumbe kuna mpango mbaya umeandaliwa na kaka zake na demu wake.

Mtoto wa Lamwai alifungiwa ndani na kaka zake na huyo demu walimpiga sana sana kipigo Cha mbwa mwitu kipigo kikali sana, sijui hiki kusanga kiliishaje miaka ile.

Japo baadae miaka hio mimi nikiwa nasoma Nakuru na Eldoret kule Kenya na kisha Bachelor degree huko Mukono Christian University ( Mukono University), . Mukono, Uganda . Huyo mpenzi wake na Mtoto wa Lamwai nilikuwa nakutana nae Kwenye Bus za Scandinavia za kwenda Kampala kutoka DSM Ubungo. We traveled 27-30 hours, occasionally we also boarded Akamba bus and Kampala coach, those were the days.

Akiwa anaelekea zake Makerere University, Kampala, Uganda. Kila nilipomwangalia yule demu akiwa amenona niliwaza sana juu ya maumivu ya mshikaji.

Maisha ndio haya haya ukipata demu mle kwa kuusikilizia sana minyanduano you never know what might happen as repercussions.

Naomba malegend wa Visiga Seminary School wenye kumbukumbu mwambie msela aje asimulie zaidi mjulishe kuna thread ipo hapa.

I had to recall this though it's painful trauma to remember about our mate.

Wenye visa vya kupigwa na mashemeji au collabo za kupigwa na mashemeji kisa wivu wa kutoka na Dada yao au mdogo wao wa kike kujeni hapa.

Ramadan Kareem

Ni hayo tu

Wadiz
 
Umenikumbusha mbali enzi hizo utiineja unanisumbua, nikiwa form 5 yeye alikua form 4, nilimnunulia simu siku ya pili baada ya kufahamiana. Kaka yake akaifuma akaichukua, mi sijui chochote nikampigia alivyopokea tu nikaanza kuongea, nikaona kimya kama sekunde 20 iv alafu nikasikia sauti ya kiume chaap nikamwambia nimewrong number samahani. Akaniambia dogo ntakupoteza achana na mdogo wangu umewrong namba wakat namba yako imeseviwa humu, ntakukamata na utajuta. Nikakata simu huku nmejawa na hofu.

Ukapita muda pisi ikanialika kwao uzuri bro wake alikuwa hanijui kwa sura ila jina ananijua. Nikaenda kwa makubaliano ikifika saa 9 hadi saa 10 kasoro niwe nishaondoka. Nikaingia kwenye saa 4 nikajiachia kama kwangu, story plus mahaba saa 9 hii hapa na sijaambulia utelezi, binti alikuwa anaogopa kwa sababu alikuwa hajawahi kufanya. Ile saa 9 akaniambia muda umeenda ila nakupa kwa kuwa nakupenda sana, nikapewa. Muda ukazidi sogea ghafla mvua na n saa 10 na madakika nafosi niondoke mtoto ananiambia ningoje mvua ikate nikafosi kuondoka, ile natoka tu getini natembea hatua kama 7 mbele nikakutana na bro wake 😂 moyo ulipiga paah kama ilivyo desturi yetu watz tukasalimiana tukiwa tunapishana. Niliapa sitokaa nije nirudie kosa la kwenda kwa mwanamke. Yule bro mpaka leo hii huwa ananiulizia akimkebehi mdogo wake kuwa tumefikia wapi na mahusiano yetu.
 
Back
Top Bottom