Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Mimi na mshkj wng niliwahi kuenda kwa mtaalam mmoja nilimsindikiza uyo mshkj wng mimi nilikuwa sina imani na nguvu za giza insuch kipindi iko afu nilikuwa mbishi, sas bana yule mzee alisema kimasihara kuwa kuna dawa nikiwapa unaona wachaw na majin usiku, mshkj wng aliogopa akaikataa mm kwa kiherehere changu niliiomba uku nikijichekesha nakudhan ni mchezo wa kuigiza. Alinipa akaniambia hii utaoga usiku alafu na hii utaipaka kabla ya kulala afu hii kesho asubuhi utaogea na kupaka ili kuiondoa iyo hali ya kuendelea kuona ila sharti ni moyo usizungumze chochote pindi utakapokuwa uona ukizungumza utajijengea mazingira ya uadui..nikakubali, Haha ayse yanii ule usiku siusahau kwa vituko nilivyokuwa naviona dunia ina mambo mengi nyiny zaidi ya unavyoiona..

Sent using Jamii Forums mobile app
Uliona nini???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna rafiki etu mmoja walikuwa na party koko beach,sasa yeye ni mnywaji wa pombe zote.sasa akiwa coco beach akaja muhudumu àkamletea soda,jamaa akamfokea wewe mimi nimeagiza kitu fulañi na sio soda.yule mwanamke ambaye ni muhudumu àkàmsogelea na kumfungulia huku akimwàmbia utàkunywa soda.
Muda huo ni yeye ndie anayemuona muhudumu wale wenźie hawamuoni.
Baada ya muda ndugu zake wanamuona kaka yao àkiogelea kweñda kati kati ya bahari,sasa wao wanamshangaa si ameagiza kinywàji na kuogelea hajui anaogeleaje kufika kule (maji mengi) .Wakainuka na kuañz kumkimbilia huku wakimwita jina lake jamaa hakugeuka wakamwita sana hakugeuka mara àka wapotea baharini.
POLISI na familia źikamtafuta kando wa mbambao siku tatu jàmaaa hakuonekana hai wala màiti.siku ya tatu usiku ndio jamaa kaja mwenyewe anajokokota hajiwezi na kufika nchi kavu akadondoka.wàtu kumuokota muhimbili.
Alipopona ndio akatusimulia kuwà baada ya kukataa soda yule mwanamke alikasirika sana na akamchukua na kwenda nae baharini çhini kabisa kuna mwamba ambao walikuwa wàkibishana muda wote .yule mwanamke alikuwa anamwambia kuwa anampenda na jamaa alikuwa na msimamo wa kumkataa na alivutwa kutaka kuelekea chini ya mwamba zaidi ndio jamaa alijizatiti ende zaidi na wamepambana muda wote mwishowe yule mwanamke àka mwambia una bahati mizimu ta kwenu ina nguvu na imekulinda.
akaçhwa ,jamàa akawa ana hangaika kupanda ule mwamba wa mawe maana alikuwa ànaona njia ya kutoka shida ni kupanda amehangaika kupanda juu wabmwamba wa jiwe mpaka akatoka.ndio kutoka amepoteza fahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hayajakukuta ni rahisi sana kuita hii ni chai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anasimulia dereva wa Fuso Jangwani.

Hiyo siku wamekaa maskani kama kawaida wakisubiri wateja, haukupita muda akaja mzee wa kiarabu hivi(mburushi).

Mzee akaulizia huduma ya kupelekewa mizigo yake wanapopandia boti za kwenda Mafia, wapo waliomkatalia, akajitokeza kidume, akamwambia mzee twende. Akamwambia kuna vity vyangu nimenunua vingi viko Kariakoo, twende tuvipitie, swala la muda lisikupe tabu, nitakulipa kijana.

Huyu alikuwa ni mzee wa makamo kidogo, basi jamaa mpaka Kkoo, wakapakia safari ikaanza. Kufika pa kupandia boti, mzee akamwambia dereva sasa kijana wangu naomba unielewe hili, naomba twende nyumbani tuvuke pamoja nikakupe pesa yako, swala la muda wa kukuweka huku isikupe tabu. Dereva keshayavulia tena ikabidi akubali tu, safari ikaanza. Wamekwenda, boti ikafika pahala ni kwenye maji bado, yule mzee akamwambia muendeshaji kuwa simamisha hapo mi nimefika.

Kila mtu mle ndani haamin mzee anachokisema, mzee akawaambia simamisha, kweli nahodha wa chombo akatii, mzee akakuta wameshamsubiri tayari vijana wake, wakaanza kupakua mzigo ukaisha boti ikaendelea na safari. Sasa yule dereva akaamua kuwa mpole tu, akaambiwa na yule mzee kwa ukarimu kabisa, usiogope kijana karibu nyumbani, yule jomba akashukuru, wakaingia ndani, kwanza aliposhuka toka chomboni akaona bonge moja la mji, hajawahi fikiria kuliona. Kakirimiwa vizuri, akaambiwa ukitaka kuoa, njoo tu huku nina mabinti zangu hawajaolewa usiogope. Jamaa akapewa pesa yake akapelekwa pale pale aliposhukia akapandishwa chomboni mpaka ng'ambo. Baada ya tukio lile yule jomba hata umwambie nina mzigo nipelekee Temeke, humpeleki.
Niongezee sukari mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Congo, Wale waasi Wachawi balaa....una shoot ni karatasi tu zinatoka! Lakini walikaa na kagame wao, walale Salama Wenzetu mbele za haki,raia hawajui, hao waasi kuna muda sehemu za Tungi na mishe mko nao Marafiki kabisa.ila amri ikitoka hakuna namna
 
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi

Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri

Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma

Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma

Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea

Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge

si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.

wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.

Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele

Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"

Aisee nimecheka sana hii story
 
Nimecheka mpk yf kaniomba simu! Wewe Jamaa utakuwa CCM wewe!
Haahah,kuna kisa cha mpemba Mafia, alikua ameanika samaki wake baada ya kuwavua, ikafika mda akatoa mkeka akawa anapiga rakaa(Anaswali).Amemaliza kuswali kugeuka hamadi samaki wake wawili hawapo, akauliza kuna ntuu kachukua samaki zangu arudishee kila mtu akakakana akasema mi natoa dakika kumi tuu msiporudisha Walah! atakufa mtuu hapa na si masiharaa... Ebanaeee baaada ya dakika 10 zikaanguka kunguru mbili(hawa ndege Weusi) zimeshakaukaa zamani mdomoni wanamabaki ya samaki....

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi

Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri

Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma

Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma

Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea

Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge

si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.

wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.

Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele

Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
Hii chai ina pilipili manga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilikuwa siamini hizo mambo lakn kipind cha wife ana ujauzito wa mtt wetu wa kwanza.. nikiwa mchanga kbsa kiimani,siku hio nakumbuka tumelala tukaota ndoto moja mm na wife.. ndoto ilikuwa ni mmama mmoja anasema anataka mtt alieko tumboni ili amtoe kafara,tukashtuka.. baada ya kushtuka tukasikia mipaka inalia nyuma ya nyumba kwa sauti kubwa,nilikuwa nmeshafundishwa kuomba na kukemea.. asee niliomba sana usiku huo kwa ujasiri na nguvu maana wife yeye muda huo alikuwa analalamika tumbo linamuuma na mtt alikuwa anarukaruka hatar tumboni... wakat naendelea kuomba kwa nguvu na ujasiri nkaanza kusikia sauti za paka zinaendelea kusogea mbali na nyumba lakn kitu ambacho kilikuja kunishangaza mpka sasa ni kwamba wakat naendelea kuomba nilianza kusikia vishindo kbsa kwnye bati na nyumba haikuwa na celingboard yaan vile vishindo ni kama mtu akiwa anatembea juu ya bati ikatembea alafu nkasikia hiko kishindo kimetua kama kudondoka nyuma ya chumba changu... nkapata ujasiri wa kukatisha maombi ghafla nkafungua mlango kwenda kuangalia nione hata nyayo.. bt sikuona chochote... Hata siku wife kaumwa na uchungu mida ya jioni mapaka yalilia sana siku hio.. akaenda hosptal akajifungua na alijifungulia pale amana enzi hizo na wakt anajifungua paka alitokea akabeba na kondo lake la nyuma,akatoka salama... tukaendelea kumlea mtt wetu lakn mtt alikuwa anaumwa kila siku mwisho hasa kuharisha na kutapika na tukienda hosptal ugonjwa hauonekani..so mtt alipofika mwaka na miez miwil sku hio hali ya mtt ikiwa dhoofu wazaz wakaomba tupeleke mtt akaugulie huko.. basi nkamwambia wife akapaki akapanda daladala kwenda home.. akiwa kwnye daladala mzee mmoja mwnye mapetepete mengi ya rangirangi na kanzu na kibalaghashia chake akauliza huyu mtt anaonekana anaumwa eeh wife akamjibu ndio.. akamwambia ugonjwa wake sio wa hosptalin bt hakumwelewa alimaanisha nn,kufika home kakaa siku ya kwnza siku ya pili usiku akiwa amelala akaota ndoto wamekuja mmama na kundi lake kavaa kaniki akasema mmalizieni kabiss huyo mtoto afu ndoto ikakatika...kesho yake asbh mie nko mtaani napiga mzgo wife akanipgia simu hali ya mtt imechange na kwl haikupita dk kumi wife akiwa anamnyonyesha mtt akamfia hapohapo... R.I.P katt kangu ka kike first born wangu..


Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana brother. Inaumiza sana. Endelea kuomba kumtumaini Bwana Yesu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga acha Kuyafanya maisha yako yakawa magumu humu Jf kwa kuwa na mitazamo ya aina hiyo kuhusu hoja zako watu wengine humu JF.
Najua watu hatufanani uwezo wa kufikiria sababu ya vitu vingi kama elimu, mazingira tuliyokulia , lishe n.k

Kama kitu haukijui au hauamini kama kipo basi anzisha uzi, watu watakuja na kukusaidia kukijua na ukiona bado haujaelewa na hauamini hilo jambo basi acha ili watu wanaojua au wanaamini hilo jambo waendelee na Imani zao.

Nimeandika hivyo sababu hoja zako zinakejeli, dhihaka , dharau n.k kuhusu hoja za watu wengine hasa hoja unazoona zipo tofauti na unachoamini wewe na kufikiria,

unatakiwa ujue kwamba duniani watu wote hatuwezi kuwa Sawa kwa kila kitu hivyo mada ambayo haikuhusu achana nayo ili maisha ya watu wengine yaendelee
Utasemaje hakuna uchawi wakati hata kuu define uchawi hujaweza?

You are not even wrong!

At least someone can be wrong, but on topic.

You are off topic.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
121 Reactions
Reply
Back
Top Bottom