Kama ukipewa ofa ya kuchagua miaka ya kuishi na mwenyezi Mungu, utachagua mingapi. Mimi 120

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,373
Wasalaam.

Kwa sababu ya uhaba wa umeme, maji safi, uwezekano wa ajali, na magonjwa ya kushtukiza na kujisababishia wabongo wengi wamekata tamaa na wanaishi kana kwamba sekunde yoyote anakufa.

Hii imepelekea ufisadi, wizi, ujanjaujanja na ukosefu wa mipango mikubwa endelevu maana watu wanajua watakufa muda wowote na wanaowaacha watafaidi.

Utafiti wa kisayansi unaonyesha mapinduzi makubwa ya kisayansi na AI yanakusudiwa kupunguza uwezekano wa kufa kuliko miaka ya zamani. Chanjo, kinga na mapinduzi ya kidaktari nayo ni kichocheo.

Mfano mwla 1999 nilishuhudia mtu anaaanza kukohoa kikohozi cha kwanza hadi anakohoa cha mwisho akiaga dunia akiwa na kilo zisizozidi kumi kwa shambulizi la HIV.

Sasa hivi ukikutwa hivyo, nitakupiga kofi nikumalizie maana ni uzembe na matumizi mabovu ya uvumbuzi wa kitabibu. Nimeona mtu anatoka kwenye hali ya semiskeleton na leo ni bonge hafikirii kifo kwa matibabu ya kisasa.

Yote haya lengo langu ninini? Ni kutaka ujiulize ikiwa utapewa uchague miaka mingapi uishi ili ufe kifo cha asili, unangechagua miaka mingapi?

Binafsi huwa namwambia Mungu ikimpendeza anipe 120, ambayo nimeikata katika vipindi vya miaka 20 kwa 20. Akiruhusu anisaidie kitu cha pili ndani ya kipindi hicho niwe nimesaidia watu Bilioni nane wampende na kuishi sawsawa na mapenzi yake hasahasa wazungu.

Ukipewa uchague uishi miaka mingapi utachagua kuishi mingapi na utaifanyia nini?

Ni hayo tu.

Karibuni.
 
Mungu hayupo mkuu. Najua ni ngumu sana kumeza.

Lakini nitakushauri, labda utaweza, ila ni ngumu.

Kuna sehemu zinaitwa blue zones. Ni sehemu ambazo zina idadi kubwa ya centenarians(watu wenye 100+)

Kuna documentaries, docuseries, na vitabu kuhusu jinsi hao watu wanavyoishi, unaweza ukafuatilia

Na ukizingatia mtu aliyevunja rekodi ya kuishi aliishi miaka 122, basi kinadharia lengo lako la 120 linafikika
 
Biblia ni neno la Mungu. Hila uzito wa neno la Mungu linaweza kutofautiana kutokana na nyakati na nani kalitamka; Kwa mfano: Agano jipya ni bora kuliko agano la kale (neno katika agano la kale uthibitishwa kwa agano jipya).

Vile vile katika Biblia kuna neno lililotamkwa na Mungu mwenyewe kwa kinywa chake; na kuna neno la Mungu alilolitamka kupitia mitume na manabii.

Neno alilotamka kwa kinywa chake ni bora kuliko la mitume na manabii. Kuhusu umri wa kuishi; Mungu kwa kinywa chake mwenyewe alitamka katika kitabu cha "Mwanzo 6:3

Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini." (miaka 120)

Vile vile alitamka kupitia nabii na kuhani Musa (kwasababu Musa alipewa na alikuwa na vyeo vyoote vya kuwa kuhani, nabii na mtume) katika "Zaburi 90:10

Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara."

(miaka 70-80 neno linasema waziwazi ni kwa wale wanaoishi maisha ya dhambi wakiwa wamefunikwa na neema ya Mungu)

Sasa: NI UHAMUZI WAKO uchague miaka hipi ya kuishi! Walio wengi nawashangaa wanachaguaga miaka 70. Akiona kafikisha miaka 70, inayoongezeka zaidi ya hapo anasema kapendelewa, jambo ambalo ni la imani haba.

Mwanadamu anayejitambua na kuzienenda ahadi za Bwana miaka yake ni 120. Wako watu katika dunia hii hii ulimwengu huu huu wamepiga miaka 90, miaka 100 na kuzidi na bado wananguvu. Kuna wanaume wababa/wazee wanauwezo wa kupeleka moto hata kutungisha mimba! Uamuzi ni wako!

Mimi niliishachagua miaka 120 na Mungu anajua hivyo. Kwa umri wangu na mwonekano wangu huwezi kuamini na ninajua na ninaendelea kumuomba Mungu anipe neema na unyenyekevu nifikishe 120! Wengine Kalaghabao! matunduizi
 
Back
Top Bottom