Kama tafsiri ya kubaka ni kumwingilia mtu kimapenzi bila ridhaa yake, basi vijana wengi walipaswa wawe mahakamani

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,090
22,374
Nawasalimu kwa jina la Chama pendwa CCM.

Kama tafsiri ya kubaka ni kumwingilia mtu kimapenzi bila ridhaa yake basi watu wengi hasa wanaume wangekuwa mahakamani wakijitetea kwa tuhuma za kubaka. Huu ni ukweli usiopingika. Wanawake wengi karibu wote wameshawahi kuingiliwa kimapenzi bila wao kutaka kwa muda huo.

Wanaume wengi pia walishawahi kuwaingilia kimapenzi wanawake kwa kuwalazimisha (kubaka). Inaweza kuwa ni baina ya wapenzi, wanandoa pamoja na makundi mengine.

Msingi wa huu uzi wangu unatokana kauli ya vijana wengi isemayo "akiingua geto lazima aliwe"... Hii inamaanisha kwamba endapo binti ataenda kumtembelea mpenzi wake huko "getoni" kwake basi hawezi toka bila kufanya mapenzi, iwe kwa kupenda au kutopenda.

Yaani kijana wa kiume atatumia kila aina ya ushawishi na ikishindikana kabisa nguvu itatumika. Kinachohuzunisha ni kwamba haya mambo huwa yanaishia palepale chumbani ingawa tayari ni kovu kwenye nafsi ya binti.

Na mbaya zaidi vijana wengi wa "Magetoni" huonekana mashujaa kwa kuweza kufanya ngono na mabinti hasa wale wanaoonekana kujiheshimu. Vijiweni husimuliana hayo mambo. Kuhusu wanandoa nao hali kama hii ya kulazimishana huwa pia inatokea ingawa kwenye huu uzi sitawaongelea sana wao.

Madhara ya hivi vitendo ni mengi sana ikiwemo kuambukizana magonjwa, mimba zisizotarajiwa na matatizo ya kisaikolojia. Hata familia hupata pigo endapo huu uovu ukifika mbele ya vyombo vya kisheria. Vijana wengi wameacha familia zao kwenye majonzi kwa kujikuta wanafungwa miaka 30 jela kwa makosa ya ubakaji. Taifa pia linaingia hasara kwa kuiweka nguvukazi yake jela.

Je, nini kifanyike? Jamii nzima ielimishane ubaya wa hii tabia. Vijana waambiwe muda sahihi wa kufanya ngono ni wakati wa ndoa. Endapo ikishindikana kabisa basi kuwe na makubaliano kati ya hao wapenzi badala ya kulazimishana.

Wale vijana wasemao "Akiingia geto lazima aliwe" nao wakumbushwe uwepo wa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la ubakaji. Familia nazo ziwe wazi kuwaelimisha vijana wao badala ya kusubiri matatizo yatokee na kusingizia ni mipango ya Mungu. Serikali nayo izidi kuelimisha vijana kupitia mashule, vyuo na sehemu zote wanapopatikana vijana kirahisi.

Nimalize kwa kuwasihi vijana wadogo waache matendo ya kipumbavu. Ni suala la muda wengi watajikuta jela bila kutegemea kwasababu wasichana wa leo nao wanaamka na kujua haki zao. TV, social media zimesaidia kujua wasichane wenzao kwingineko duniani wanafanyaje inapotokea hali kama hiyo.
 
Tatizo wabongo kitu chochote kinachohusisha kuvuana chupi lazima mlete masikhara.
 
Kumuingilia kimwili, na si kimapenzi.

Ni kweli, asilimia kubwa ya kinachotokea ni ubakaji, hata ukisoma Uzi wa Kula tunda kimasihara, mwanaume atamwingiza kidole mwanamke ukeni, akihisi kulowana, basi hiyo ndio ruhusa kwake.
 
Hali zenu,

Baada ya tafakuri ya muda mrefu na kuunganisha matukio nimebaini haya;

Wanawake kamwe hawawezi kusema wala kulalamika wanabakwa, wakiwa kwenye mahusiano na wanaume wanawapenda au wanaojulikana na ndugu na jamaa zao. Wanaume tunabaka sana tu, hasa tuliooa, tuwe wakweli tu.

Imagine mkeo hajisikii vizuri (haumwi ila hana mood kwa muda huo) na wewe unahitaji, hapo lazima ubake tu, ukizingatia ni usiku na mpo chumbani watoto wameshalala. Wanaume tunabaka sana tu.

Sema hawezi kukushtaki kwa sababu anajua ukishaolewa kiuhalisia "Hakuna kubakwa" isipokuwa propaganda za magharibi tu za kuharibu ndoa.

Yaani ni kutafuta mafuta kupaka kisha kusukuma taratibu ili asichubuke, hakuna namna hapo. No kumchezea wala nini, na yeye anakusubiri umalize apumzike, yaani anafanya kukuridhisha wewe kwa kuwa una uhitaji.

Hebu imagine na boksa za siku hizi zilivyo laini yaani unashangaa mashine hiyo bhana. Kubaka ndoani hakuepukiki, siyo ndoani tu hata kwenye mahusiano hakuepukiki.

NB: Simaanishi kule kwa kutumia nguvu, hapana!

Daaah, anayebisha aje hapa na aseme kuwa "Mimi sijawahi kubaka".
 
Back
Top Bottom