Habari wadau..
January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.
Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.
Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.
Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na ceo wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi zao ambazo walikuwa wanasoma msingi, hizo olimpio na arusha school zilikuwepo tayari ila wala hawakusoma hizo shule na leo wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..
Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za serikali kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.