Kha! Hadi taarabu na R&B itakuwa inapigwa msibani
Taratiibu tunawafikia wazungu kwenye hilo..msibani hadi kualikwa kwa kadi
Taratiibu tunawafikia wazungu kwenye hilo..msibani hadi kualikwa kwa kadi
Juzi nilikuwa namtafuta shosti kwa dharura, akaniambia yupo salon anasuka, akanielekeza nikaona nimfwate....
wakati tunaongea, kulikuwa na mrembo mmoja pembeni anashonea weaving na kutengenezwa kucha, kope, nyusi, n.k.
mara simu ya mrembo ikaita, maongezi yakaanza..... "yaani we acha tu, ndo mambo ya dunia lakini, Tunamshukuru Mungu..... asante sana....
tunaaga kesho mchana na safari ya kwenda Moshi kwa mazishi itaanza baada ya kuaga, kweli tutammiss sana kaka yetu....."
baada ya hapo maongezi yakawa yanaendelea akawa anasimulia kuwa kakake kabisa kafariki, kaumwa siku 2 tu kafa.....
sijui ndo ukijijini au ushamba wangu! kweli nilisikitika sana.....
sipati picha kakangu anafariki, mimi naweza kuwa na nguvu kwenda salon kujipiga msasa ili niende kuzika kakangu au ndugu yangu wa karibu.
Nikajiuliza mambo mengi sana.
1) ni kwamba watu siku hizi wamezoea sana misiba kiasi kwamba wanaona ni kitu cha ajabu tu kufiwa?
2) watu hatuna uchungu tena na ndugu zetu?
3) u-kisasa unatufanya tuwe hivyo?
kweli mahusiano na ndugu/jamaa/marafiki yamepungua kiasi hiki mpaka tunachukulia misiba ya ndugu zetu kirahisi namna hii?
Hata wachumba wanatafutwa msibani siku hizi
marangu kwa mara nyingine, msiba wa baba ya rafiki yangu/mwanachama mwenzangu, nipo nae kwenye kikundi, hii nayo ilikuwa funga kazi,tumetoka KCMC kuchukua mwili tukisindikizwa na tarumbeta, pale home kuna mahema ya kutosha, msiba unafatiliwa kwa njia ya projector, kila hema lilikuwa na meza kubwa ya kila aina ya vinywaji, bufee zilikuwa za kutosha, tumefika nyumbani MC anatuongoza kwa kwaya tu,(tenzi za rohoni hazina nafasi siku hizi) tuliimba kichaga kidogo wakati wakienda kuzika,makaburini walienda familia/ndugu wa karibu sana, wengine tuliendelea kufatilia na projector huku wahudumu wakiwasikiliza mnatumia vinywaji gani,rafiki yetu huyo anawatuma wahudumu "unaowana walee waliovaa sare za purple ni kikundi changu cha arusha, kuna wanaokunywa ballantin, amarula, savannah wasikilizwe kila mmoja anachotumia apatiwe", tumemaliza msiba rafiki yetu karudi arusha tumeenda kumpa pole akatuambia msiba ulitumia 22mil.
huyo sasa alipitiliza, lol!
sasa kama alikuwa na ukame sana si angmkamata mumewe maana alikuwa naye?
ha haaa, lol! haya banaUkame wapi ni kuendekeza mataa za kimwili na kuziacha akili zikilalamika baada ya majambozi
rafiki unaweza kuanzisha tu, nadhani hiyo itakuwa na mtazamo tofauti na hii yangu.Umeniwahi kidoogo tu
ilikuwa nianzishe thread kuhusu hili
mimi nashangaa zaidi na watu kuitana bar na kuweka kikao cha msiba bar
halafu siku ya mazishi watu kupiga picha full swagga...kwenye kaburi...
he heee, analo hilo.... tena huko kijijini ndo moto utamuwakia.juzi juzi kuna rafki yangu wa kike kafiwa na mumewe,basi ikawa tupo kanisani katika kuaga,lakini nikaona kama ndugu wa mume wanamtenga hv? nikauliza rafki yetu mwingine ndo akanipa mkasa,kumbe yule dada jana yake alikaa chumbani akajishonea hilo sijui weaving akajiremba sasa ndugu wa mume wakakasirika kweli,yaani mwenzio kafa hata kuzikwa hajazikwa we unajiremba....wameenda kuzika mkoani,lazima kutakua na shida sana huko. lakini watu hawana upendo wa kweli nowdays.
ha haaa, lol! huko marangu sijui nina rafiki mmarangu?marangu kwa mara nyingine, msiba wa baba ya rafiki yangu/mwanachama mwenzangu, nipo nae kwenye kikundi, hii nayo ilikuwa funga kazi,tumetoka KCMC kuchukua mwili tukisindikizwa na tarumbeta, pale home kuna mahema ya kutosha, msiba unafatiliwa kwa njia ya projector, kila hema lilikuwa na meza kubwa ya kila aina ya vinywaji, bufee zilikuwa za kutosha, tumefika nyumbani MC anatuongoza kwa kwaya tu,(tenzi za rohoni hazina nafasi siku hizi) tuliimba kichaga kidogo wakati wakienda kuzika,makaburini walienda familia/ndugu wa karibu sana, wengine tuliendelea kufatilia na projector huku wahudumu wakiwasikiliza mnatumia vinywaji gani,rafiki yetu huyo anawatuma wahudumu "unaowana walee waliovaa sare za purple ni kikundi changu cha arusha, kuna wanaokunywa ballantin, amarula, savannah wasikilizwe kila mmoja anachotumia apatiwe", tumemaliza msiba rafiki yetu karudi arusha tumeenda kumpa pole akatuambia msiba ulitumia 22mil.
umeona eeh!Ushamba na ujuha wetu Ndio unatufanya tuonekane wajinga...
ha haaaa, full vitenge na kanga....mmmh . . . ndugu yangu!! Bora hata yasifike yaishie hukohuko mjini, sie wengine mambo ya kutokelezea kibongo movie ilhali ni mkanda wa msiba hatuyawezi mweeeh!
mlongo wangu kwa kweli naomba tu tuwe tunatembea wote, maana naona huu mji unanipeleka siko.....ahahahhah dada langu bana!
si ajabu ulianza kulia hapo!
hii ndo daslam bana!
we unadhani wote hawaogi siku tatu kama kule kumpitimbi?
NAJUA ULIVYOSTUKA dada wa mimi!
lakini ndo hivo tena!pooole mpenzi kuanzia leo naanza kuongozana na wewe kokote wasije wakaniulia dadangu bure kwa presha!
ha haaaa, karibu yataenea kooote, maana si ndo hawa hawa tunaishi nao huko mijini?yanayotokea uko uchagani siku hizi ni aibu tupu pesa imetufanya kua malimbukeni.
mwenzangu, huu ushamba kweli unanipeleka pabayaacha ushamba bana!!
ntawezaje sasa!mlongo wangu kwa kweli naomba tu tuwe tunatembea wote, maana naona huu mji unanipeleka siko.....
sasa nikipata presha si utapata kazi sana kulea wale vifaranga wote?
ha haaaa, full vitenge na kanga....
angalau siku hizi hatuvai nguo nyeusi, lol!
hata kama mahusiano na marehemu hayakuwa mazuri huwa tunaonyesha huzuni.....Undugu wa siku hizi umebaki kuwa ni indentity tu.Nikupe mfano halisi huyu mama amebahatika kupata watoto sita.Inafikia hatua huyu mama anaishiwa nguvu na anaumwa sana.
Kati ya watoto hawa,ni watoto watatu tu wenye kuonesha kujali hali ya mama yao,na bahati mbaya uwezo wao wa kifedha ni mdogo.Ugonjwa aliougua mama yao waweza kutibika pengine kwenye referal hospitals,ndugu hawa hawaoneshi kumuhangaikia mama yao inavyostahili.Hatimaye siku inafika mama anafariki.
Wakati wa msiba umoja unaooneshwa na ndugu hawa ni wa kushangaza,kwa mara ya kwanza wanakutana na kujadiliana kuhusu mazishi ya mama yao 'kipenzi".
Bajeti kubwa ya mamilioni inapitishwa,sare zinashonwa,spika kubwa na Dj mzoefu vinakodishwa na chakula cha kila aina kipo msibani.
Nikija kwenye uzi ulioletwa hapa,kuna mawili,huyo dada inawezekana kwa upande mmoja anawakilisha familia ambazo hazijaliani,undugu isn't a big deal,na kwa vyovyote kujirembua nk ni maandalizi ya ufahari utakaoenda kuoneshwa msibani.
Kwa upande wa pili huyu dada pengine anaonesha true colour yake kwa misingi ya kwamba mahusiano yake na huyo kaka ambaye ni marehemu tangu mwanzo hayakuwa mazuri,hii inaweza kuwa inachangiwa na sababu nyingi zikiwemo tofauti za wazazi,kosa la marehemu nk
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Ndo mtajua maana ya kuwa na mashosti kila angle. Mtoto wa kike mjini lazma uwe na shosti wa kukukopesha hata kope, viatu, pochi, wigi etc. Usisahau sehemu za huduma kama kukopa besdei party (unaenda kujimwaya mwaya utalip mwisho wa mwezi...tena masakiii). Huduma ya pedicure na ya kurembwa uso inahusika. Anadaiwa reginald mengi seuze mie?ha haaa, na mfuko utatobokaje!
au King'asti mnafanyaje inapofikia hivi?
atakopa arusha wing yote maana sidhani kama mshahara utatosha
ha haaaa, hapo ndo ntadead kabisaaaaa......ntawezaje sasa!
sasa hao ni vifaranga hao baba zao!lol kazi yake ni kubwa sana!bora tu niwe nakupeleka kila sehemu!
unawexza ukakutana na watu wamevaa blouze pale muhimbili clinic ukakimbia kitumbini kununua mawax eti uwafunge!
au utakutana na watu wapo msibani wanachagua rangi ya leggins itakayoendana na jeneza ukajizimikia bure!
lol!