Juzi nilikuwa namtafuta shosti kwa dharura, akaniambia yupo salon anasuka, akanielekeza nikaona nimfwate....
wakati tunaongea, kulikuwa na mrembo mmoja pembeni anashonea weaving na kutengenezwa kucha, kope, nyusi, n.k.
mara simu ya mrembo ikaita, maongezi yakaanza..... "yaani we acha tu, ndo mambo ya dunia lakini, Tunamshukuru Mungu..... asante sana....
tunaaga kesho mchana na safari ya kwenda Moshi kwa mazishi itaanza baada ya kuaga, kweli tutammiss sana kaka yetu....."
baada ya hapo maongezi yakawa yanaendelea akawa anasimulia kuwa kakake kabisa kafariki, kaumwa siku 2 tu kafa.....
sijui ndo ukijijini au ushamba wangu! kweli nilisikitika sana.....
sipati picha kakangu anafariki, mimi naweza kuwa na nguvu kwenda salon kujipiga msasa ili niende kuzika kakangu au ndugu yangu wa karibu.
Nikajiuliza mambo mengi sana.
1) ni kwamba watu siku hizi wamezoea sana misiba kiasi kwamba wanaona ni kitu cha ajabu tu kufiwa?
2) watu hatuna uchungu tena na ndugu zetu?
3) u-kisasa unatufanya tuwe hivyo?
kweli mahusiano na ndugu/jamaa/marafiki yamepungua kiasi hiki mpaka tunachukulia misiba ya ndugu zetu kirahisi namna hii?