marangu kwa mara nyingine, msiba wa baba ya rafiki yangu/mwanachama mwenzangu, nipo nae kwenye kikundi, hii nayo ilikuwa funga kazi,tumetoka KCMC kuchukua mwili tukisindikizwa na tarumbeta, pale home kuna mahema ya kutosha, msiba unafatiliwa kwa njia ya projector, kila hema lilikuwa na meza kubwa ya kila aina ya vinywaji, bufee zilikuwa za kutosha, tumefika nyumbani MC anatuongoza kwa kwaya tu,(tenzi za rohoni hazina nafasi siku hizi) tuliimba kichaga kidogo wakati wakienda kuzika,makaburini walienda familia/ndugu wa karibu sana, wengine tuliendelea kufatilia na projector huku wahudumu wakiwasikiliza mnatumia vinywaji gani,rafiki yetu huyo anawatuma wahudumu "unaowana walee waliovaa sare za purple ni kikundi changu cha arusha, kuna wanaokunywa ballantin, amarula, savannah wasikilizwe kila mmoja anachotumia apatiwe", tumemaliza msiba rafiki yetu karudi arusha tumeenda kumpa pole akatuambia msiba ulitumia 22mil.