Kama sielewi elewi vile!

Kama sielewi elewi vile!

Fixed Point

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Posts
11,304
Reaction score
12,753
Juzi nilikuwa namtafuta shosti kwa dharura, akaniambia yupo salon anasuka, akanielekeza nikaona nimfwate....
wakati tunaongea, kulikuwa na mrembo mmoja pembeni anashonea weaving na kutengenezwa kucha, kope, nyusi, n.k.
mara simu ya mrembo ikaita, maongezi yakaanza..... "yaani we acha tu, ndo mambo ya dunia lakini, Tunamshukuru Mungu..... asante sana....
tunaaga kesho mchana na safari ya kwenda Moshi kwa mazishi itaanza baada ya kuaga, kweli tutammiss sana kaka yetu....."
baada ya hapo maongezi yakawa yanaendelea akawa anasimulia kuwa kakake kabisa kafariki, kaumwa siku 2 tu kafa.....
sijui ndo ukijijini au ushamba wangu! kweli nilisikitika sana.....
sipati picha kakangu anafariki, mimi naweza kuwa na nguvu kwenda salon kujipiga msasa ili niende kuzika kakangu au ndugu yangu wa karibu.
Nikajiuliza mambo mengi sana.
1) ni kwamba watu siku hizi wamezoea sana misiba kiasi kwamba wanaona ni kitu cha ajabu tu kufiwa?
2) watu hatuna uchungu tena na ndugu zetu?
3) u-kisasa unatufanya tuwe hivyo?
kweli mahusiano na ndugu/jamaa/marafiki yamepungua kiasi hiki mpaka tunachukulia misiba ya ndugu zetu kirahisi namna hii?
 
ndio hapo tulipofika binamu, ila binadamu tunatofautiana wapo wanaochukulia msiba kama sehemu ya kwenda kuuza sura na kutafuta mabwana hasa hapa mjini hiyo tabia ipo ukitaka kujua hayo nenda kwenye vibaa au grocery zilizoko karibu na msiba ndio utajua kuwa kufa kufaana. kwa mwenye akili siku hizi walionda msibani utawajua na walioenda kwa malengo yao utawajua wala hawajifichi, michango ya msiba tu watu wanatia ndani sembuse hiyo kujiremba na kuvaa madera yanayotikisa nyonga. binam usiku mwema
 
Hata mimi nashangaa mkubwa mwenzangu,

Siku hizi kuna watu wamegeuza misiba kuwa kama mashindano ya mavazi au urembo...

Anyway..yetu macho, tena ukizingatia tulishajistaafia..

Babu DC!!
ni bora kujistaafia aisee lakini hali inatisha....
nimejaribu kuchukulia poa watu ambao wanaenda kuzika wakiwa wamevalia sababu labda wao siyo ndugu na hawana uchungu na marehemu,
lakini inapofikia mtu kafiwa na close relative halafu anakimbilia salon kujisopua, ukweli hainiingii kichwani mkubwa mwenzangu
 
Mambo yalianza kubadilika tangu zamani sana lakini hatukushituka. Vile vile misiba imekuwa mingi kiasi kwamba watu wamezoea. Pamoja na yote msiba unakuhusu huwezi kuuzoea.
 
Mambo yalianza kubadilika tangu zamani sana lakini hatukushituka. Vile vile misiba imekuwa mingi kiasi kwamba watu wamezoea. Pamoja na yote msiba unakuhusu huwezi kuuzoea.
kama niliposema hapo juu kweli sishangai sana kwa watu wa mbali walioenda msibani....
lakini huyu aliyefiwa na kakake, tena kaugua kwa siku 2 tu! mmmh!:nono:
 
ni bora kujistaafia aisee lakini hali inatisha....
nimejaribu kuchukulia poa watu ambao wanaenda kuzika wakiwa wamevalia sababu labda wao siyo ndugu na hawana uchungu na marehemu,
lakini inapofikia mtu kafiwa na close relative halafu anakimbilia salon kujisopua, ukweli hainiingii kichwani mkubwa mwenzangu

Haya bwana,

Mimi nilishajinyamazia...

Unaenda kwenye msiba na kuambiwa kuwa bajeti ya mazishi ni 10mil....

Wakati huo unahangaika na karo za watoto ambazo ni <4mil....

Ngoja kwanaza tulimbuke...

Babu DC!!
 
Wewe kweli babu! Bajeti ya msiba ya milioni 10 ilikuwa miaka 3 ama 4 nyuma. Sasa tunaongelea mil 15 baba. Na familia ina minimum contribution!
Haya bwana,

Mimi nilishajinyamazia...

Unaenda kwenye msiba na kuambiwa kuwa bajeti ya mazishi ni 10mil....

Wakati huo unahangaika na karo za watoto ambazo ni <4mil....

Ngoja kwanaza tulimbuke...

Babu DC!!
 
Siku hizi msiba ni show tupu my dear. Hawakuongelea mwenye saluni akawapake makeup ama maznat alishawahi tenda?
Ningekuwa mie ndo wewe mbona ningechomekea tenda ya sare!
ha haaaaa, na ushamba huu nani angenipa hiyo tenda?
maana nilionyesha wazi wazi kushangaa dada mtu kuja kujipara ili akamlilie kakake
 
Hiyo ni mpya cjapata kuona ndo leo nasikia. hata kama ni kidigital mnavyoita nyie, lkn ndugu yako afariki we unakwenda saloon! Hao ndio wale wanaoanza kupigia mahesabu nyumba ya kaka atarithi nani, kadi ya bank iko wapi, ile RAV 4 cjui atapewa mkewe au mimi. Mungu atunusuru.
 
Juzi nilikuwa namtafuta shosti kwa dharura, akaniambia yupo salon anasuka, akanielekeza nikaona nimfwate....
wakati tunaongea, kulikuwa na mrembo mmoja pembeni anashonea weaving na kutengenezwa kucha, kope, nyusi, n.k.
mara simu ya mrembo ikaita, maongezi yakaanza..... "yaani we acha tu, ndo mambo ya dunia lakini, Tunamshukuru Mungu..... asante sana....
tunaaga kesho mchana na safari ya kwenda Moshi kwa mazishi itaanza baada ya kuaga, kweli tutammiss sana kaka yetu....."
baada ya hapo maongezi yakawa yanaendelea akawa anasimulia kuwa kakake kabisa kafariki, kaumwa siku 2 tu kafa.....
sijui ndo ukijijini au ushamba wangu! kweli nilisikitika sana.....
sipati picha kakangu anafariki, mimi naweza kuwa na nguvu kwenda salon kujipiga msasa ili niende kuzika kakangu au ndugu yangu wa karibu.
Nikajiuliza mambo mengi sana.
1) ni kwamba watu siku hizi wamezoea sana misiba kiasi kwamba wanaona ni kitu cha ajabu tu kufiwa?
2) watu hatuna uchungu tena na ndugu zetu?
3) u-kisasa unatufanya tuwe hivyo?
kweli mahusiano na ndugu/jamaa/marafiki yamepungua kiasi hiki mpaka tunachukulia misiba ya ndugu zetu kirahisi namna hii?

Inategemea na namna walivo kuzwa toka utoto,katika hali ya kujua
huyu ni ndugu yangu,tuna thaminiana vipi,nini maana ya undugu.

Nikupe mfano?

Baba yangu ana watoto 6,kila mtoto ana mama yake.
Sijakaa na baba yangu ila mama.

ndugu zangu tunaoshare mama tumekua wote,tumecheza wote,tumelala njaa wote,
tumesherehekea wote mafanikio etc. Tunajua nini maana ya kua ndugu.

Tofauti na ndugu zangu wale watoto wa baba yangu. Akifa mmoja kati ya watoto wa
baba,feelings hazitakua sawa sawa na ndugu zangu tulio share mama.

Ni mfumo mbaya,ambao ndio upo kwenye maisha ya sasa. Watoto wana sambaa bila kujua ndugu
zao wako wapi,ni vipi wanapaswa pendana kama ndugu,ni nini uthamani wa binadamu mwenzako
ni kitu ambacho hatukipati/kukitoa kwa watoto wetu. Mungu na atusamehe.
 
Haya bwana,

Mimi nilishajinyamazia...

Unaenda kwenye msiba na kuambiwa kuwa bajeti ya mazishi ni 10mil....

Wakati huo unahangaika na karo za watoto ambazo ni <4mil....

Ngoja kwanaza tulimbuke...

Babu DC!!
kwetu kijijini gharama huwa ni ya jeneza tu...... vingine vyote bure...
chakula watu wanaleta na kupika, maji mnachotewa, kaburi linachimbwa........
kuoga mnapelekwa mtoni baada ya kutoka kwenye mazishi.....
huo wanja utauona wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom