Kama serikali ya Zanzibar lazima iwepo, basi kuirudisha Tanganyika hakuepukiki

Hiyo ni sababu ya kijinga kabisa, mbona kuna jamii (makabila) madogo sana yenye watu wachache ambao hawafiki hata 100,000 hayajafutika mpaka hivi leo
Eti Zanzibar itamezwa, nani anakula nchi na watu wake? Hakuna mtu anayeweza kumeza hata kijiji wala Kata. Vijiji vingi vilikuwepo tangu enzi wakoloni hawajakuja na vipo mpaka sasa. Ukweli wazanzibar hawapendi Muungano.
 
Umeon
Baada ya Ikulu zote nchini Kisiwandui, Magogoni na Chamwino kukaliwa na watanzania visiwani ndiyo nikaona umuhimu wa kuwa na serikali tatu au moja tu. Serikali tatu itasaidia kutunza siri na nyaraka za serikali ya Zanzibar na siri na nyaraka za serikali ya Tanganyika. Serikali moja inasaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano iliyeko madarakani kuzifikia, kuzijua na kuzitunza siri za Zanzibar na Tanganyika kwa wakati mmoja tofauti na sasa ambavyo siri na nyaraka za wazanzibar ziko chini ya wazanzibar wenyewe lakini zile za Tanganyika ziko wazi kwa watanganyika na wazanzibar pia

CCM imetufikisha hapa tulipo sana. CCM bara wako kwa maslahi binafsi ya matumbo yao, lakini CCM Zanzibar wako kwaajili ya maslahi mapana ya Zanzibar.

Kama serikali ya Zanzibar lazima iwepo litoke jua inyenye mvua basi kuirudisha Tanganyika hakuepukiki sasa ili kuweka mambo sawa.
Umeongea kitu rahisi sana lakini kwa jicho la mbali mjadala wake haupaswi kuacha upite tu.
 
Huu ni muungano uliotengeneza Serikali mbili ambapo ilikubalika Zanzibar iendelee kuwa na serikali yake, Tanganyika itoweke na maslahi yake yabebwe na Serikali ya muungano.
Over.
Naona kama watu wanashupaza shingo kwa vitu visivyohusiana kabisa.

Mtaalamu amesema, kama Tanganyika haipo, kwanini Znz iendelee kuwepo? Kwa miaka yote, hakuna mZnz aliyewahi kuwa raisi wa JMT, waTanganyika waliona ni sawa tu kwakuwa wanawakilishwa na raisi wa Jamhuri, sasa tuna raisi ambaye ni mZnz halisi, Znz inaendelea kuwa na raisi wao, TANGANYIKA inawakilishwa na makamu?

Kumbuka hata suala la raisi wa Znz liliondelea kwa dhumuni kama hilo, kuwa isije kutokea raisi wa JMT akakata moto, kisha wa Znz akakaa pale na kule wakaendelea na uZnz.

Sukari, kweli? Wanayozalisha haiwatoshi, ukauze ili upate pesa? Lililojificha nyuma ya pazia ni kuwa, sukari ile haizalishwi Znz bali ni kutoka nje ya Znz na mostly ni magendo.
 
Ninashauri iwepo serikali moja tu,Nadhani ndilo lilikuwa lengo la Nyerere.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno Nyerere alitaka serikali moja tu. Lakini bila kumung'unya maneno Karume alikuwa hataki Muungano kabisaaa, ni woga tu uliomsukuma akubali muungano. Sio vibaya sisi tuliofaidi matunda ya muungano tukatengeneza muungano wetu uwe bora kutokana na manufaa yake kwetu na namna matukio yanavyotukuta katikati ya muungano.

Hatuna Nyerere na Karume tena wa kututengenezea muungano wetu hivyo tuwe wakweli tutengeneze Muungano wetu uwe bora kabisa.

Serikali moja tu ndilo suluhisho
 
Ni kweli kabisa mzee, ni ruksa kwa Mzanzibar kuongoza Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja lkn mtanganyika hawez kuongoza Zanzibar. nafikir hapa waasisi wa muungano walikwenda chaka kidogo.
 
Nani alikuambia hilo lilikuwa lengo la Nyerere? Kama lilikuwa lengo lake kipi kilimzuia kutekeleza akiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano kwa miaka 20?
Usidanganye watu, hasa vijana ambao wanataka kuifahamu historia ya nchi yao.

Unaweza kueleza sababu hasa za Aboud Jumbe kuachishwa urais wa Zanzibar? Unaweza kusema akina Maalim Seif rip walivyotoka CCM?
 
Wazanzibar Mungu awajalie sana, wanajitambua, wana hofu ya Mungu, wanalijali taifa lao na Mungu anawasikiliza na kujibu maombi yao. Wazanzibar wako kwenye bunge la Tanganyika na watanganyika hawako bunge la Zanzibar.

Wazanzibar wooote wana maono lakini Watanganyika ni Nyerere tu peke yake ndiye aliyekuwa think tank peke yake, waliobaki wanafikiria wao, familia zao, ndugu zake, marafiki zake, kabila lake na kanda yake tu baaaaasi. Wazanzibar wanajali hatima yao kama taifa kabla ya kama watu binafsi ndani ya muungano
Huyo Nyerere ndie alituletee huu muungano wa mazingaombwe
 
hivi ukitenganisha hizo nchi mimi mwananchi wa kawaida huku Ikunghulyabhashi nafaidikaje
 
Ni wazi kuwa Tanganyika ndio inang'ang'ania Muunganiko wake na Zanzibar na kwa miaka mingi tumekuwa tunawasikia Wazanzibari wakitaka kujitenga na zaidi baadhi husikika kuwa hata rais wa Kwanza wa Zanzibar alipenda ku-nullify muungano wa ajabu, ikawa kama ndio kwamba Mungu pekee anaweza kukuumba lakini kukufisha chochote kinaweza!
 
Sababu zinazotolewa za kuibakiza serikali ya Zanzibar hazina mashiko kabisa. Eti isije ikaonekana Tanganyika inaimeza Zanzibar kutokana na udogo wake. Hii ni sababu ya watu wasiokuwa na nia njema. Ni nani atakaeona Zanzibar inamezwa? Inamezwaje wakati mipaka yake inafahamika? Ikimezwa kunatokea nini? Mbona Tanganyika sasa hivi imemezwa na Zanzibar mbona maisha yanakwenda? Si unajua Rais ana nguvu nyingi kwa mujibu wa katiba yetu, akipenda anaweza kuuhamisha mlima kilimanjaro kwenda anakotaka yeye?
Kwa 3 nakuunga mkono,lakini 1 Ng'o.

Sisi tuliunganisha Baadhi ya Mambo tuu, na hatuko tayari kuongeza ila tunafikiria kuyapunguza.

kama Tanganyika wanapenda Muungano si walobi na Nchi za Malawi,au Kenya au Kongo mbona wametushikilia sisi zanzibar tuu utafikiri Ruba.

Unganeni naMsumbiji ,si muliwasaidia kuwakomboa hao kwa kuwasaidia kijeshi na silaha?

Kwanini Tembo ajigambe kuuwa Sungura?., Zanzibar kwa Tanganyika nikama Tembo na Sungura kwa ukubwa.

Tafuteni laiki yenu, musituwekee kero lisilo kwisha.

WAZANZIBARI TUNATAKA MUUNGANO WA USAWA. KAMA NCHI ,HAMUTAKI UNGANENI NA WENGINE MUONEJOTO YA JIWE. MUNATUONEA KWA KUWA SISI WADOGO TUU.
 
Now siri za Tanganyika (kiuchumi, kirasilimali, kinguvu, nakadhalika) ziko vinganjani mwa wazanzibari

Tanganyika imeingia cha kike
Kuna umuhimu wa kubadilisha katiba,makamu wa rais sharti atoke visiwani hata kikitokea kifo nk
 
Bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno Nyerere alitaka serikali moja tu. Lakini bila kumung'unya maneno Karume alikuwa hataki Muungano kabisaaa, ni woga tu uliomsukuma akubali muungano. Sio vibaya sisi tuliofaidi matunda ya muungano tukatengeneza muungano wetu uwe bora kutokana na manufaa yake kwetu na namna matukio yanavyotukuta katikati ya muungano.

Hatuna Nyerere na Karume tena wa kututengenezea muungano wetu hivyo tuwe wakweli tutengeneze Muungano wetu uwe bora kabisa.

Serikali moja tu ndilo suluhisho
Nadhani Nyerere aliamua tu kuwaheshimu Zanzibar kwa kuwa hata uwezo wa kuwapiga na kuvichukua visiwa kwa nguvu especially wakati ule Zanzibar ilikuwa unstable alikuwa nao.Ila hakutaka Historia ianze vibaya ndiyo maana akaamua kutumia ustaarabu mbele ya Karume lakini bado jamaa akawa mbishi.Nyerere amesacrifice nchi na jina la Tanganyika kwa ajili ya muungano lakini bado hakuliona hilo.Nadhani kuna siri juu ya kifo cha Karume na siri juu ya muungano na sidhani kama kuna rais atakayekuwa na uwezo wa kuuvunja maana anaweza kupotezwa kabla hajatekeleza.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
nani atakaeona Zanzibar inamezwa?
Ukweli sijawahi kuelewa maana halisi ya nahau/msemo huu wa "Zanzibar kumezwa".

Leo ndiyo umezidi kuchanganya kabisa kwa swali la "nani atakae ona Zanzibar imemezwa!?". Yaani nimevutiwa kumjua huyu anayesema/amini kuwa tukiwa na serikali moja na nchi moja Zanzibar itamezwa. WanaJF ninaomba ufafanuzi wa mambo haya.
 
Nadhani Nyerere aliamua tu kuwaheshimu Zanzibar kwa kuwa hata uwezo wa kuwapiga na kuvichukua visiwa kwa nguvu especially wakati ule Zanzibar ilikuwa unstable alikuwa nao.Ila hakutaka Historia ianze vibaya ndiyo maana akaamua kutumia ustaarabu mbele ya Karume lakini bado jamaa akawa mbishi.Nyerere amesacrifice nchi na jina la Tanganyika kwa ajili ya muungano lakini bado hakuliona hilo.Nadhani kuna siri juu ya kifo cha Karume na siri juu ya muungano na sidhani kama kuna rais atakayekuwa na uwezo wa kuuvunja maana anaweza kupotezwa kabla hajatekeleza.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
JPM unamuona kabisa rohoni mwake kuwa alisukumwa na Utanganyika kuyafanya yale aliyoyafanya kwa muda mfupi. Rais ambaye hana Utanganyika rohoni hawezi kukifikia kiwango kile cha utendaji hata kidogo. Yule mwenye msiba ndiye ambae macho yatavimba kwa kulia. Huwezi kumnyonyesha mtoto wa jirani wakati wa kwako anakonda.
 
Zanzibar ni sehemu Tanzania. Wazanzibari pia hawaruhusiwi kuuza sukari bara
Yaani duka la mtanzania mwenye kujitambulisha mzanzibari wa Pemba anayemilika duka Magomeni Dar es Salaam haruhusiwi kuuza sukari!? Ebu eleza vizuri inamaanisha nini hapa!?
 
Back
Top Bottom