Kama ningekuwa Mh Pinda ningejiuzulu

Kama ningekuwa Mh Pinda ningejiuzulu

Pinda hawezi kujiuzulu kwa sababu hana historia ya ujasiri wala sifa ya uongozi na uwajibikaji.
 
Namuonea huruma.Anatamani kutoa maamuzi magumu, tatizo uwezo HANA!!!!.
Pole kaka Pinda. Nawe pia ni GAMBA umeshndwa kutusaidia WANANCHI!!!!!

Bora gamba EL tusingefika kote huku

Jairo angekua anapalilia bustani
 
jamani!! Pinda siku ile hakusema angemwadabisha jairo. Alichosema ni kuwa angekuwa na mamlaka angetoa maamuzi juu ya suala la jairo - maamuzi hayo pengine mojawapo lingekuwa kama mkuu wa nchi alivyoamua kulitenda. Wabunge walilalama au walitoa allegations na hawakumtaka pinda categorically arudishe jibu bungeni. Ni sahihi kuwa wabunge hawakuridhika na wameamua kuunda tume teule kufanya uchunguzi wao. Pinda ni pinda na serikali yake - si sahihi kwa wabunge ku-sympathise dramatically kuhusu pinda na mahusiano yake na serikali. Tusubiri maamuzi ya tume teule ndipo tutaziona true colours za pinda kama tulivyoziona wakati "akitekeleza" maazimio ya tume teule ya bunge kuhusu richmond.

k wewe
 
Salaam, kwa ufinyu wangu wa mawazo nadhani ulikuwa wakati muafaka wa mh pinda kukaa pembeni.
Sasa tunapata picha halisi ya serikali ya jk na maswahiba wake.
Sasa naelewa kwa nini magufuri alisema anatamani angekuwa mbunge wa kawaida tu.

Kuna uwezekano mkubwa akafanya hivyo wakati atakapokuwa anaahirisha bunge la kumi ijumaa kesho kutwa. Tusubiri tuone Vinginevyo hii ni nafasi yake pekee ya kuonyesha uadilifu wake.
 
Salaam, kwa ufinyu wangu wa mawazo nadhani ulikuwa wakati muafaka wa mh pinda kukaa pembeni.
Sasa tunapata picha halisi ya serikali ya jk na maswahiba wake.
Sasa naelewa kwa nini magufuri alisema anatamani angekuwa mbunge wa kawaida tu.

Mkuu uko sawa kabisa. Ila kwa mizengwe iliyopinda usitarijie chochote hapo hajui yupo hapo kama nani. PM alikuwa EL lakini naye alikuwa na uchu wa mali sana ndiyo yakamkuta yaliyomkuta. Msimseme sana PM wetu wa sasa atalia hadharani!!!???
 
hakuna sababu ya kujiuzulu kwani luanjo amedharau wote pamoja na bunge zima sio pinda mwenyewe
 
Ajiuzuru wakati hata mpanda Rami bado haijaenda! Pinda naye ndo walewale2 kwanza ilibidi awe afsa mashamba huyu!

sasa si ndo anatakiwa aachie ngazi ili achaguliwe atakaefikisha lami mpanda?
 
Jairo kasimamishwa kazi tena huenda mh pinda alitaka kufanya hivyo ngoja tuone
 
Kama jk mwenyewe ameuona huo ni moto tena unaunguza kama nin nae ameona ajiweke pemben je ni kweli au anatutega
 
Katika hili labda Mhe. Pinda angepaswa kujiuliza mara mbili iwapo Serikali ya JK ina imani nae au lah.

Tarehe 9.02.2012 alikutana na madaktari Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kufafanua sehemu tu ya Hatua ambazo Serikali imechukua ikiwemo kumwondoa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mganga Mkuu. Lakini ikumbukwe kuwa kabla ya hapo, Madaktari walikataa kuonana na Mhe. Waziri Mkuu na kumtaka awafuate kule wanakofanyia mgomo. Kufuatia msimamo huo wa madaktari, aliwatishia kwa kuwapa siku moja ili kesho yake wawe makazini vinginevyo watakuwa wamepoteza ajira zao. Hata hivyo, madaktari walishinkilia msimamo wao na ndipo Mhe. Waziri Mkuu akaona ni busara kuonana nao ana kwa ana tarehe 9.02.2012.

IMG_4279.jpg



Katika Kikao cha tarehe 9.02.2012 Mhe. Waziri Mkuu aliwataka madaktari kurejea kazini ili kuipa pia Serikali fursa ya kuendelea kushiughulikia matatizo yao ikiwemo la kuwaondoa Waziri na Naibu Wzairi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

WIki iliyopita pale (tarehe 7 Machi, 2012) mara baada ya chama cha madaktari kutangaza kuanza tena na mgomo wa kutaka kutekelezwa kwa sehemu ya madai yao wakishinikiza madai yao ya kutaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya wajiuzulu.


Mhe. Waziri Mkuu alipozungumza na Vyombo vya Habari kabla alieleza kuwa Serikali imejipanga kukabiliana na mgomo wao na tayari Serikali ilikuwa na mipango yake na ilichokuwa ikisubiri ni kuona matokeo ya mgomo huo kuanza.

ALISEMA: "Serikali imejipanga kukabiliana na mgomo huo. Pale jana (juzi) nilipozungumza na waandishi ofisini kwangu sikutaka kueleza mipango yote na kila kitu, lakini tulikuwa tunawasubiri tu wagome,"

Hata hivyo, pamoja na kauli hizo za Mhe. Pinda, madaktari bado waliendelea kugoma, na kwa kuonyesha kuwa Mhe. Pinda ameshindwa kabisa kutafuta suluhu katika hilo, Mhe. Rais mwenyewe alijitosa na kuingilia kati suala hili ambapo tarehe 9 Machi, 2012 ikiwa ni mwenzi mmoja tu tokea Mhe. Pinda kukutana na Madaktari pale Muhimbili (sio Ofsini kwake), Mhe. aliwahita Viongozi wa Chama cha Madaktari IKULU ambapo haikuelewekwa kwa nini katika kikao hicho w Mhe. Waziri MKuu ambae ndie mshauri wake na ambae alijaribu kutatua tatizo hilo hawali hakuwepo kabisa. Hali hii inadhihirisha nini??.., Je Pinda alionekana kushindwa!!?
​
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha ikulu jijini Dar es salaam viongozi wa Chama cha madaktari nchini. Wa pili kushoto ni Mratibu wa mgomo wa madaktari, Stephen Ulimboka na Kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi


Uamuzi wa Mhe. Rais kukutana na Madaktari unaleta maswali mengi hasakuhusu imani ambayo ofisi ya Mhe. Rais inayo kwa Mhe. Waziri Mkuu. Ili la Madaktari ni sehemu tu ya jukumu ambalo linaonyesha wazi kuwa labda Ofisi ya Waziri Mkuu imekosa ushirikiana wa dhati au imeshindwa kabisa kulishughulikia.

Ikumbukwe kuwa yapo maamuzi mengi ambayo Mhe. Waziri Mkuu amewahi kuyatoa na Serikali yake kwenda kinyume nayo. Hii haikuwahi kutokea zama zile za utawala wa Waziri Mkuu Edward Lowassa ambae labda alikua na misimamo isiyojumbishwa ukiachia tu lile lililompeleka kwenye kashfa mpaka akashauriwa na mkuu wake wa Nchi kujiona hafai tena kuwa kiongozo kwa cheo hicho cha "U-PM" (kashfa ya Richmond).

Miongoni mwa yale ambayo Mhe. Pinda alipewa dhamana ya kuyasimamia na wananchi tukajua anaweza ni pamoja na sakata la aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madaini Bw. David Kitundu Jairo ambapo japokuwa Mhe. Waairi Mkuu aliongea kwa uchungu sana Bungeni na kusema kama ingekuwa katika mamlaka yake angemwajibisha mara moja Jairo, lakini baada ya siku chache Ofisi ya Mhe. Rais ili mzunguka pale aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari ya kumsafisha Jairo na baadae Jairo kurejeshwa kwa mbwembwe Ofisini.

Mbali na hili la madaktari, katika utendaji wa kawaida, inaonekana Ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu na ile ya Mhe. Rais zimekuwa na misimamo au staili tofauti ya ushughulikiaji wa masuala mbalimbali nyeti na ya kitaifa, ikiwemo:

(i) Maamuzi katika Sakata la Richmond
(ii) Suala la Serikali kuhamia Dodoma
(iii) Migomo ya Vyuo Vikuu
(iv) Wizi wa Vocha za Pembejeo
(v) Suala la Mafuta Tanzania Visiwani
(vi) Mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi
(v) Posho za wabunge
(vi) mahakama ya Kadhi
(vii) Bomoa bomoa kwenye hifadhi ya barabara nk.

Itakumbukwa pia kuwa Machi 6,2011 Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, aliwahi kutoa kauli ilipomtaka Waziri wa Ujenzi Dr. Magufuli kusimamisha bomoabomoa katika Hifadhi za Barabara nchi nzima hadi itakapoamuliwa na Baraza la Mawaziri. Hata hivyo, Dr. Magufuli alionekana kupuuza kauli hiyo na aliendelea na zoezi la Bomoa Bomoa Mpaka pale Mhe. Rais Mwenyewe alipolizungumzia kwa staili ya kuzuia.

Na kupwaya kwa Mhe. Pinda katika maamuzi ndiko kuliko pelekea hata Mhe. Lowassa kujigamba kuwa Serikali hii imeshindwa kuchukua maamuzi magumu mara nyingi tofauti na ilivyokuwa wakati wake.

Mhe. Waziri Mkuu ifike wakati atafakali sana na ikibidi achukue hatua:

2012, DUNIA YAKO, CHAGUO LAKO, CHAGUA KUTOYUMBISHWA KWENYE MAAMUZI!!.








​
 
Pinda ni kama shokabuzoba ktk gari. Au unataka niseme ni popo!
 
anasubiria mafao yake jamani mwache avurunde mwishowe arudi Mpanda kupumzimka na Heshima yake ya waziri mkuu mstaafu
 
sijawahhi ona cheo kinachotumia kodi za walalahi wakatio hakina kazikama hiki.
 
Kujiuzu ni utamaduni wa watu wenyehekima na utu, mtu anayeweza kulinganisha cheo chake na wajibu wake. Viongozi wetu wamepeana vyeo bila wajibu. kwa hiyo ajiuzulu kwa lipi? Ameshindwa nini?
 
IMO ninavoona hapa na siku zoote tokana na matukio yanayopinzana kati ya Raisi na viongozi wengine ni kua JK Matatizo yakitokea amekua ni ile attitude ya kuonesha kua Wizara/Viongozi husika wana absolute say na maamuzi katika baadhi ya mambo. Hasa kwa Mizengo Pinda. Na inapotokea Pinda katoa maamuzi ambayo yeye JK kwa wakati huo anaona hayafai for whatever reasons ndio hapo anaingilia kati bila kujali kua maamuzi yamesha tolewa. Na bahati mbaya ilioje, kakuta Mh. Waziri mkuu anapenda kutoa kauli haraka haraka bila kukaa kutafakari maneno yake (nina wasi hata kama hua anaomba ushauri).

Hata hivo Ngoshwe Mh anastahili kujiuzulu kwa ajili ya kushinda kufanya kazi ama sababu ya kutoa Kauli inayopinzana na matendo yake?
 
Kikwete ndio kigeugeu,Pinda hawezi kukurupuka Kuongea na Madaktar pasipo Rais mwenyewe kujua,mbona alibarik posho za wabunge harafu akaja akakana!? Rais hatuna kabisaaaa
 
Kikwete ndio kigeugeu,Pinda hawezi kukurupuka Kuongea na Madaktar pasipo Rais mwenyewe kujua,mbona alibarik posho za wabunge harafu akaja akakana!? Rais hatuna kabisaaaa


Kwa hii serkali inavoendeshwa inawezekana kabisa.... Hapo inaonesha udhaifu wa wazi kuhusiana na Ushirikiano kati ya Raisi na viongozi wengine. Unakumbuka mambo ya posho na pale Makinda alipotoa kauli kua Raisi kakubali kuhusu posho hali hapo hapo JK alisema kakataa na kawaambia watumie busara? Ili tatizo naona ni Sugu katika huu utawala na hawajifunzi tokana na makosa...
 
Kikwete ndio kigeugeu,Pinda hawezi kukurupuka Kuongea na Madaktar pasipo Rais mwenyewe kujua,mbona alibarik posho za wabunge harafu akaja akakana!? Rais hatuna kabisaaaa

Kama Pinda asingekuwa mchumia tumboni angekwisha jiuzulu toka wakati ule mkweree alipomuabisha kwenye sakata la Jairo! Huyu Pinda amekwisha lose credibility mbele ya wananchi kiasi kwamba lolote atakalosema watu hawatamuamini kwani wanajua kuwa hana authority!!
 
Back
Top Bottom