Kama ningekuwa Mh Pinda ningejiuzulu

Kwa hili mie naona hakuna haja ya kuwa na baraza la mawaziri wala viongozi wateule:sleepy:. JK anaweza kupiga mzigo wote mwenyewe.:sleepy: Awapige wote chini abaki peke yake angalau kodi yetu itumike sehemu nyingine:sleepy:
 
Mkanganyiko wote huu na sintofahamu zake ninatokana na kutokuwa na mipaka ya wazi inayojulikana kwa wananchi kati ya roles za Rais na za Waziri Mkuu.

Kama kiongozi wa serikali ni Rais, hakuna haja kabisa ya kuwa na Waziri Mkuu. Kama ingekuwa ni kutokana na mahitaji badala ya kuiga mifumo ya kiserikali, Tanzania haipaswi kuwa na Waziri Mkuu kama madudu ya kiuongozi ndio haya tunayoyaona!!

Tufanya bidii, katika katiba mpya Kiongozi wa Serikali awe ni Waziri Mkuu. Ni kwa namna hii tu ndio hata wabunge wanaweza kumwajibisha kwa chaguo la waziri fulani. Hii itawapa wabunge uwezo wa kuamua Waziri Mkuu amuwajibishe nani au aondoke yeye. Si rahisi kumwajibisha Rais na huenda uozo wa mambo unafichwa ktk jambo hili.
 
Pinda ni hovyo. Hawezi kuisimamia ofisi hii nyeti ya PM. Nashangaa kwa nini hajihuzuru?
 
Pinda ana roho ngumu kama Maneno Oswald

Roho ngumu yake inaligharimu sana Taifa.sijuia hata kama ushauri wake kwa Mhe. Rais unapokelewa!!, Sifahamu wakati ule Luhanjo alipkuwa CS kama walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja manake inaonekana hata Luhanjo was very strong than PM.
 
sijawahhi ona cheo kinachotumia kodi za walalahi wakatio hakina kazikama hiki.

Nafikiri hiki cheo kina maana sana ila tu hakijapata mtu makini wa kukikamata hebu kumbuka kilipokuwa chin ya Hayati Edward Sokoine Moringe.

nafikiri cheo ambacho hakina maana na kinatumia kodi za walala hoi bure ni kile cha makamu wa rais na kunahaja ya kukiondoa kabisa kwani inoekana kama kipo kwa ajili ya kuwalizisha wazanzibar lakini in actual sense hakina umuhim na maana yoyote ile kwa maendeleo, ustawi na mstakabali wa taifa letu!
 
JK apo amemtreat PM kama ganda la mua bse ilibidi awepo kwa kikao cha jmosi kama mwendelezo wa vikao vya apo nyuma.
Naona JK hana imani na wasidizi wake sijaona mtu mwengine pale zaidi yake JK labda kama picha inadanganya au wapo waliokuwa nyuma ya JK
 
Mwanzo alipoteuliwa nilidhani atakua kama hayati Sokoine,kumbe tofauti anajali maslahi binafsi,ni udhaif kwa msomi kama yeye kutetea mawaziri wasitekeleza majukumu yao,shame on him,dhahiri hastahili kuwa kiranja mkuu
 
Mkanganyiko wote huu na sintofahamu zake ninatokana na kutokuwa na mipaka ya wazi inayojulikana kwa wananchi kati ya roles za Rais na za Waziri Mkuu.

Kama kiongozi wa serikali ni Rais, hakuna haja kabisa ya kuwa na Waziri Mkuu. Kama ingekuwa ni kutokana na mahitaji badala ya kuiga mifumo ya kiserikali, Tanzania haipaswi kuwa na Waziri Mkuu kama madudu ya kiuongozi ndio haya tunayoyaona!!

Tufanya bidii, katika katiba mpya Kiongozi wa Serikali awe ni Waziri Mkuu. Ni kwa namna hii tu ndio hata wabunge wanaweza kumwajibisha kwa chaguo la waziri fulani. Hii itawapa wabunge uwezo wa kuamua Waziri Mkuu amuwajibishe nani au aondoke yeye. Si rahisi kumwajibisha Rais na huenda uozo wa mambo unafichwa ktk jambo hili.

Sidhani kama tatizo ni kukosekana kwa mipaka kati ya waziri mkuu na rais. Tatizo ni kukosa "collaboration". Mipaka kikatiba iko very clear. Rais, ni kama "Board chairman" yaani sawa na mmiliki wa serikali. Waziri mkuu ni sawa na CEO wa serikali ambaye anatakiwa awe mtendaji mkuu. Model hii utaiona vizuri sana wakati wa Mwalimu, ambapo mwalimu alikuwa na role ya juu zaidi kama owner wa government kwa niaba ya wananchi. Hapa utaona roles za mawaziri wakuu zilikuwa very clear na kila tulipopata waziri mkuu mpya uliona tofauti kubwa kwa style za kiutendaji. Mfano ni pale Salim alipochukua baada ya kifo cha Sokoine.

Matatizo yaliyopo sasa hayasababishiwi na katiba, yanasababishwa na rais asiyejiamini, ambaye ameamua kujirundikia maamuzi yote kwake. Matokeo yake wale walioko chini yake wote, pamoja na waziri mkuu, wanajikuta katika hali ya kutojua wafanye nini na wakati gani. Katika hali kama hiyo, rais amegeuka kuwa mmiliki wa kampuni na vile vile anafanya kazi kama afisa mtendaji mkuu. Model hii ya uongozi hata kwenye biashara utaiona pale IPP ambapo mzee Mengi pamoja na kuwa ni mmiliki wa makampuni yale bado amejilimbikizia nguvu za kiutendaji na hufanya maamuzi ya kiutendaji. Rais wetu sasa hivi yuko hivyo.

Utayaona mambo haya kwenye sakata la Jairo, Posho za wabunge na sasa kwenye mgomo wa madaktari. Inaonekana pinda huwa anafanya maamuzi kabla ya kufanya mawasiliano na rais. Au inawezekana huwa wanakubaliana, ila akiishafanya maamuzi, rais akaona hayo maamuzi si popular, basi hujitenga na maamuzi yale. Au pinda huwa anafanya maamuzi bila kufanya collaboration na kujua maoni ya rais, hatimaye anafanya maamuzi ambayo rais hakkubaliani nayo.

Hii inamfanya Pinda aonekane kama Simba wa kuchora mbele ya macho ya wananchi.
 
Nafikiri hiki cheo kina maana sana ila tu hakijapata mtu makini wa kukikamata hebu kumbuka kilipokuwa chin ya Hayati Edward Sokoine Moringe.

nafikiri cheo ambacho hakina maana na kinatumia kodi za walala hoi bure ni kile cha makamu wa rais na kunahaja ya kukiondoa kabisa kwani inoekana kama kipo kwa ajili ya kuwalizisha wazanzibar lakini in actual sense hakina umuhim na maana yoyote ile kwa maendeleo, ustawi na mstakabali wa taifa letu!

Kilimpata Edward Mwingine toka Monduli tukamuondoa kwa fitina!
 
Mwanzo alipoteuliwa nilidhani atakua kama hayati Sokoine,kumbe tofauti anajali maslahi binafsi,ni udhaif kwa msomi kama yeye kutetea mawaziri wasitekeleza majukumu yao,shame on him,dhahiri hastahili kuwa kiranja mkuu

Ukulima wake ndio unamponza..cheo chake ni kikubwa ila ni mwoga wa kupitiliza na ndio inayomsabaishia hata pengine kujutia nafasi hiyo na inapombana sana anashindwa kuvumilia, wakati JK anachekacheka yeye anaamua kulia tu mzee wa watu maskini!!
 
Kutofautiana kati ya Pinda na JK kulitokea katika awamu ya pili ya uongozi wa JK, ambapo JK aliamua kutomchagua Pinda kuendelea kuwa PM. Lakini kwa wakati huo, Pinda alikuwa akionekana kuwa na ukaribu na wananchi (mtoto wa mkulima), na JK alishauriwa asimwache Pinda kwa kuwa ingelete chuki zaidi ya wananchi dhidi ya serikali. Hata hivyo, kitendo cha JK kumrudisha Pinda kwa shinikizo la wazee wa CCM kilimuudhi sana Pinda, na hata mwanzoni alikataa kukubali uteuzi wa kuwa PM katika awamu ya pili ya JK. Alikubali baada ya kubembelezwa na hao wazee wa CCM. Hata hivyo ufa kati ya Pinda na JK tayari ulikuwa umewekwa, na tunachoshuhudia sasa ni dalili za ukuta kuanguka. Kimsingi haijulikani kama Pinda anafanya madudu makusudi, ila JK ana kila sababu za kusema "niliwaambie mie, huyu jamaa hanifai kama PM".
 
Kusema kweli Tanzania hatuna Waziri Mkuu.
Hilo tukubali tuu!
Serikali yote imejaa makachero wa zamani, walidhani ndiyo watakuwa viongozi bora kumbe bora kuwa viongozi!
 
mi nionavyo ni kuwa PM ni mwadirifu kupita kiasi,alivyokuwa anakubari hicho kiti au uteuzi hkujua anaenda kutumikia serikali ya aina gani ya mkuu wake.JK yeye ana maamuzi yanayotegemea upepo,kwanza anashauriana na watendaji wake thn anategesha antena zake akisikilizia upepo thn anaripika tu kivyake.mfano ni pale mkuu wa wizara ya UMEME na MADINI alivyotoa maamuzi ambayo kiukweli alikuwa kashuriana na mkuu wake na aliongea kwa mbwembwe kweli ishu ya malipo ya DOWANS,mkuu akasikilizia kwanza upepo unavuma kutoka wapi,nafikiri kila mmoja anajua ni aina gani ya aibu aliipata home boy wangu.....na huyu PM ne anachezewa staili hiyo hiyo anakuwa just a rubber stamp....you just stamp on the document as you wish....kwa hiyo mtoto wa mkulima pale alipofikia ni bora liende mifuko yangu imetuna na maisha yanaenda.....hana la kufanya na posho bado anaitaka,tofauti na hapo angekuwa alishatoka mchana kweupeeeeee.....
 
Katika hili labda Mhe. Pinda angepaswa kujiuliza mara mbili iwapo Serikali ya JK ina imani nae au lah.

Tarehe 9.02.2012 alikutana na madaktari Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kufafanua sehemu tu ya Hatua ambazo Serikali imechukua ikiwemo kumwondoa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mganga Mkuu. Lakini ikumbukwe kuwa kabla ya hapo, Madaktari walikataa kuonana na Mhe. Waziri Mkuu na kumtaka awafuate kule wanakofanyia mgomo. Kufuatia msimamo huo wa madaktari, aliwatishia kwa kuwapa siku moja ili kesho yake wawe makazini vinginevyo watakuwa wamepoteza ajira zao. Hata hivyo, madaktari walishinkilia msimamo wao na ndipo Mhe. Waziri Mkuu akaona ni busara kuonana nao ana kwa ana tarehe 9.02.2012.

IMG_4279.jpg



Katika Kikao cha tarehe 9.02.2012 Mhe. Waziri Mkuu aliwataka madaktari kurejea kazini ili kuipa pia Serikali fursa ya kuendelea kushiughulikia matatizo yao ikiwemo la kuwaondoa Waziri na Naibu Wzairi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

WIki iliyopita pale (tarehe 7 Machi, 2012) mara baada ya chama cha madaktari kutangaza kuanza tena na mgomo wa kutaka kutekelezwa kwa sehemu ya madai yao wakishinikiza madai yao ya kutaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya wajiuzulu.


Mhe. Waziri Mkuu alipozungumza na Vyombo vya Habari kabla alieleza kuwa Serikali imejipanga kukabiliana na mgomo wao na tayari Serikali ilikuwa na mipango yake na ilichokuwa ikisubiri ni kuona matokeo ya mgomo huo kuanza.

ALISEMA: “Serikali imejipanga kukabiliana na mgomo huo. Pale jana (juzi) nilipozungumza na waandishi ofisini kwangu sikutaka kueleza mipango yote na kila kitu, lakini tulikuwa tunawasubiri tu wagome,”

Hata hivyo, pamoja na kauli hizo za Mhe. Pinda, madaktari bado waliendelea kugoma, na kwa kuonyesha kuwa Mhe. Pinda ameshindwa kabisa kutafuta suluhu katika hilo, Mhe. Rais mwenyewe alijitosa na kuingilia kati suala hili ambapo tarehe 9 Machi, 2012 ikiwa ni mwenzi mmoja tu tokea Mhe. Pinda kukutana na Madaktari pale Muhimbili (sio Ofsini kwake), Mhe. aliwahita Viongozi wa Chama cha Madaktari IKULU ambapo haikuelewekwa kwa nini katika kikao hicho w Mhe. Waziri MKuu ambae ndie mshauri wake na ambae alijaribu kutatua tatizo hilo hawali hakuwepo kabisa. Hali hii inadhihirisha nini??.., Je Pinda alionekana kushindwa!!?
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha ikulu jijini Dar es salaam viongozi wa Chama cha madaktari nchini. Wa pili kushoto ni Mratibu wa mgomo wa madaktari, Stephen Ulimboka na Kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi


Uamuzi wa Mhe. Rais kukutana na Madaktari unaleta maswali mengi hasakuhusu imani ambayo ofisi ya Mhe. Rais inayo kwa Mhe. Waziri Mkuu. Ili la Madaktari ni sehemu tu ya jukumu ambalo linaonyesha wazi kuwa labda Ofisi ya Waziri Mkuu imekosa ushirikiana wa dhati au imeshindwa kabisa kulishughulikia.

Ikumbukwe kuwa yapo maamuzi mengi ambayo Mhe. Waziri Mkuu amewahi kuyatoa na Serikali yake kwenda kinyume nayo. Hii haikuwahi kutokea zama zile za utawala wa Waziri Mkuu Edward Lowassa ambae labda alikua na misimamo isiyojumbishwa ukiachia tu lile lililompeleka kwenye kashfa mpaka akashauriwa na mkuu wake wa Nchi kujiona hafai tena kuwa kiongozo kwa cheo hicho cha "U-PM" (kashfa ya Richmond).

Miongoni mwa yale ambayo Mhe. Pinda alipewa dhamana ya kuyasimamia na wananchi tukajua anaweza ni pamoja na sakata la aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madaini Bw. David Kitundu Jairo ambapo japokuwa Mhe. Waairi Mkuu aliongea kwa uchungu sana Bungeni na kusema kama ingekuwa katika mamlaka yake angemwajibisha mara moja Jairo, lakini baada ya siku chache Ofisi ya Mhe. Rais ili mzunguka pale aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari ya kumsafisha Jairo na baadae Jairo kurejeshwa kwa mbwembwe Ofisini.

Mbali na hili la madaktari, katika utendaji wa kawaida, inaonekana Ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu na ile ya Mhe. Rais zimekuwa na misimamo au staili tofauti ya ushughulikiaji wa masuala mbalimbali nyeti na ya kitaifa, ikiwemo:

(i) Maamuzi katika Sakata la Richmond
(ii) Suala la Serikali kuhamia Dodoma
(iii) Migomo ya Vyuo Vikuu
(iv) Wizi wa Vocha za Pembejeo
(v) Suala la Mafuta Tanzania Visiwani
(vi) Mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi
(v) Posho za wabunge
(vi) mahakama ya Kadhi
(vii) Bomoa bomoa kwenye hifadhi ya barabara nk.

Itakumbukwa pia kuwa Machi 6,2011 Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, aliwahi kutoa kauli ilipomtaka Waziri wa Ujenzi Dr. Magufuli kusimamisha bomoabomoa katika Hifadhi za Barabara nchi nzima hadi itakapoamuliwa na Baraza la Mawaziri. Hata hivyo, Dr. Magufuli alionekana kupuuza kauli hiyo na aliendelea na zoezi la Bomoa Bomoa Mpaka pale Mhe. Rais Mwenyewe alipolizungumzia kwa staili ya kuzuia.

Na kupwaya kwa Mhe. Pinda katika maamuzi ndiko kuliko pelekea hata Mhe. Lowassa kujigamba kuwa Serikali hii imeshindwa kuchukua maamuzi magumu mara nyingi tofauti na ilivyokuwa wakati wake.

Mhe. Waziri Mkuu ifike wakati atafakali sana na ikibidi achukue hatua:

2012, DUNIA YAKO, CHAGUO LAKO, CHAGUA KUTOYUMBISHWA KWENYE MAAMUZI!!.










Mkuu, hapo umeyanena yote ya muhimu na busara kwa watu walioendelea na wanaoona mbali kifikra na kihisia! Ila kwa hapa unamaanisha Nani ajiuzulu?? PINDA?
Nilishasema ktk baadhi ya threads zangu kuwa Tanzania haijawahi kumpata kiongozi anayezuga kiuongozi na kinafiki kama PM huyu anayejiita eti mtoto wa mkulima, kumbe FEKI ya nguvu! Tanganyika yetu ina hasara kwa miaka mingine mi-3 ijayo...maana tunaye yeye na mkubwa wake, hakuna wa kumtoa mwingine tongotongo!
My Take, Mafisadi hawana 'roho'! Na huyu PM, si tumeona akiwakingia vifua mafisadi hata bungeni? Huyu usubirie punde si punde atakapoibuliwa na ma-skandali makubwa hata kuliko yale ya EL! Jamaa myeyushaji huyu, hakunaga! Ni 'Machozi ya mamba' tu!
 
Mkuu, hapo umeyanena yote ya muhimu na busara kwa watu walioendelea na wanaoona mbali kifikra na kihisia! Ila kwa hapa unamaanisha Nani ajiuzulu?? PINDA?
Nilishasema ktk baadhi ya threads zangu kuwa Tanzania haijawahi kumpata kiongozi anayezuga kiuongozi na kinafiki kama PM huyu anayejiita eti mtoto wa mkulima, kumbe FEKI ya nguvu! Tanganyika yetu ina hasara kwa miaka mingine mi-3 ijayo...maana tunaye yeye na mkubwa wake, hakuna wa kumtoa mwingine tongotongo!
My Take, Mafisadi hawana 'roho'! Na huyu PM, si tumeona akiwakingia vifua mafisadi hata bungeni? Huyu usubirie punde si punde atakapoibuliwa na ma-skandali makubwa hata kuliko yale ya EL! Jamaa myeyushaji huyu, hakunaga! Ni 'Machozi ya mamba' tu!


Kwa hiyo ni mnafiki?
 
Back
Top Bottom