Hata hivo Ngoshwe Mh anastahili kujiuzulu kwa ajili ya kushinda kufanya kazi ama sababu ya kutoa Kauli inayopinzana na matendo yake?
Sio kwa kushindwa kazi, bali kwa kuchezewa chezewa kila wakati kama hana maamuzi ya kiserikali,..(apime labda wenzie akiwemo yule aliemteua pengine hamwamini kwenye utendaji wake na ndio maana wanaweza kumvuruga kama vile alivyovurugwa na Luwanjo na Mkuu wa Nchi akakaa kimya tu asiseme lolote.
Unadhani Mh. Pinda ni Kiongozi wa type ya kujali anafikiriwa nini? Amewehuka na yale yote ambayo yanaambatana na kua Kiongozi for him to care. Anajua nini anakipata pale na maisha anayo ishi. Naona Uongozi pale ni Secondary to hasa kile ambacho anakipata tokana na hicho cheo. Kama viongozi walo chin yao kuwaamuru kustaafu inakua ni kazi kubwa sembuse yeye mwenyewe? Siamini kua hana akili kiasi hicho cha kuweza kuona kua Wananchi na viongozi wenzake wote wamepoteza Imani dhidi yake.
Tulidhani kwa taaluma yake kama Mwanasheria siasa zisingemshambulia ashindwe kuelewa nini anafanyiwa au nini anapaswa kufanya, katika kipindi chake chote imeonekana kama hawezi hiyo nafasi labda alichukuliwa kwa upole wake tu ili aburuzwe. Maeneo mengi yamepwaya na hata ile mipango ya maendeleo imeshindwa kutekelezwa kabisa hakuna KILIMO KWANZA wala Mpango wa ELIMu ya SHule za Sekondari na Msingi; Hakuna Mkakati wa Kufufua Zahanati wala kuinua pato la wakulima na Wafugaji. Yote ni Zero Zero..sasa tunaambiwa karibia asilimia 69 ya bajeti ya Serikali iliyopitishwa bna Bunge kwa aajili ya kuwaletea maendeleoa wananchi imekatwa Hazina kwa ajili ya kusaidia Shughuli za Chaguzi Ndogo na za Wabunge wakati watanzania wanakufa, maisha magumu na uchumi unayumba.
Fedha kibao zilitumika katika Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru na hakuna manufaa yeyote tuliyoyaona zaidi ya kuzawadiana nishani tu wakubwa na kutonnyesha vifaa vya zamani vya kivita.
Pinda ana roho ngumu kama Maneno Oswald
Sa kama Pinda analijua hilo si aachie ngazi ili kulinda heshma yake???Mimi naliona tofauti.Kikwete ndio kigeugeu,Pinda hawezi kukurupuka Kuongea na Madaktar pasipo Rais mwenyewe kujua,mbona alibarik posho za wabunge harafu akaja akakana!? Rais hatuna kabisaaaa