Kama ni kweli na ushahidi upo....

Jamaaa sijui anauchawi gani.kumbuka mama Ane kilango alipokosea akatumbuliwa palepale .yule jamaa wa Tanesco akatumbuliwa .Kitwanga akatumbuliwa na wengine wengi lakini huyu yupo jijini na vyeti feki anadunda na Rais amfanyi chochote na inawezekana kaishapigiwa simu yakumtia jeuri kabisaaa
 
Kesi ya jinai inaendeshwa na serikali na sio mtu binafsi.

Mwenye wajibu wa kuchunguza na kumpeleka huyo jamaa mahakamani ni serikali.
Sio kwel acheni kugeuza maneno...unaweza mshtaki kiongoz yeyote...mbona CUF walimshtak IGP....nenden zenu...msihadae watu....kama kwel mnajiamn makonda ana fake nenden mahakamni
 
So far hakuna ushahidi wowote! Hii ni propaganda tu! Case closed!!
 
Hivi kama anachafuliwa kwanini Asiende, mahakamani? Mbowe ametaka kumshitaki pamoja na kuwa na wanasheria unaona anavyohangaika. Tutaendelea kumbana namna hii mpaka a choose, la a tuonyeshe vyeti halisi tangu Kolomije mpaka digrii.
 
Kwa hiyo mimi nikija hapo ulipo na kukutwanga ngumi kwenye chembe huwezi kwenda mahakamani kunifungulia mashitaka ya kukushambulia?
Jeuri hiyo huna unapigwa mpaka unazimia we nyani.
 
Hivi kama anachafuliwa kwanini Asiende, mahakamani? Mbowe ametaka kumshitaki pamoja na kuwa na wanasheria unaona anavyohangaika. Tutaendelea kumbana namna hii mpaka a choose, la a tuonyeshe vyeti halisi tangu Kolomije mpaka digrii.
Naam, swali zuri kabisa tena ambalo laweza kuulizwa kwa pande zote!
 
Jeuri hiyo huna unapigwa mpaka unazimia we nyani.
Sijawahi kushindwa street fight yoyoye ile mimi.

Kama unaweza tukutane sehemu tuzipige.

Mi naweza kuja hata uani kwa babako....
 
Kesi ya jinai inaendeshwa na serikali na sio mtu binafsi.

Mwenye wajibu wa kuchunguza na kumpeleka huyo jamaa mahakamani ni serikali.
Nyani Ngabu your thread has been closed. Sasa uhoji kwanini jamhuri isimshtaki makonda ili akajibu tuhuma za zinazoelekezwa kwake?
 
Hivi kama anachafuliwa kwanini Asiende, mahakamani? Mbowe ametaka kumshitaki pamoja na kuwa na wanasheria unaona anavyohangaika. Tutaendelea kumbana namna hii mpaka a choose, la a tuonyeshe vyeti halisi tangu Kolomije mpaka digrii.

Yeye kwenda mahakamani ni uamuzi wake binafsi.

Hakuna shurti ya kisheria inayomlazimu kufanya hivyo.
 
Vyeti Kumng`oa Rc Makonda? - Udaku Special Blog

Wakati Gwajima akidai kuwa na nakala za vyeti vyote viwili vya Paul Makonda, vikiwemo vile alivyotumia kuanzia kidato cha nne, upo mkanganyiko mkubwa kutokana na maelezo ya Paul Christian (mtu aliyedaiwa kumpa vyeti Makonda) aliyoyatoa kwa gazeti moja la kila siku la hapa nchini.

Paul Christian, anayedaiwa kuwa ndiye ambaye cheti chake kilitumiwa na Paul Makonda aliliambia gazeti hilo;

“Paul Makonda nimemfahamu kupitia habari na jina wanavyolitaja (waliotunga taarifa ya mtandaoni) wanakosea kwani mimi naitwa Paul Pierre Christian Kagezi, hatuna uhusiano, mimi Mhaya yeye Msukuma.”

“Taarifa hizo (za kumpa cheti Makonda) si za kweli kwa sababu huwezi kutoa cheti wakati umepata daraja la kwanza kidato cha sita, utakwenda vipi chuo kikuu? Sasa niliwezaje mimi kwenda chuo kikuu halafu kwa wakati huo nimpe naye aende chuo kikuu?”Alihoji.

Cristian aliendelea kudai kuwa katika kidato cha tano na sita, alichukua mchepuo wa sayansi masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), hivyo si rahisi kutoa cheti hicho kwani angeshindwa kumudu huko alikokwenda.

Alihoji kama Makonda hakufanya vema kidato cha nne au hakusoma kidato cha sita, akatumia cheti cha mtu mwingine, angeweza vipi kufanya vema katika mitihani yake ya chuo kikuu?

Alifafanua kuwa watu wamekuwa wakipika na kuoanisha majina yao, huku akiendelea kukanusha kuhusu taarifa hizo.

“Kama wanataka kumpata huyo bwanamdogo (Makonda) kwa njia hiyo wamemkosa, kwani kwa mantiki nimekuuliza ukipata daraja la kwanza kidato cha sita lazima uende chuo kikuu?” alihoji.

“Huyo bwana anajitegemea yeye kama yeye na walichokifanya wao (waliosambaza taarifa mtandaoni) kwa makusudi yao bila shaka wana lengo lao, wao wametaka kuingiza hoja ambazo hazina mshiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…