Kama ni kweli na ushahidi upo....

Kama ni kweli na ushahidi upo....

Watu wa kanda ya ziwa utawajua tu.
Hata wale waliokuwa na misimamo huko nyuma, kwenye utawala wa mtu wao wanaleta ngonjera.

Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
 
NECTA walitoa tangazo la kumtaka mtu yeyote mwenye ushahidi juu ya mtu yeyote anayetumia cheti cha kughushi au cheti kisichochake awasiliane nao kwa,

Email:esnecta@necta.go.tz.

Namba:0742484955

Cha kushangaza wadau wanabweka mitandaoni na kwenye makanisa tu ilhali issue ni simple tu.

Kwangu Mimi hii issue mpaka sasa naona ni ngonjera tu mpaka watakapochukua hatua hao wabwekaji.
Kumbe hadi NECTA washatoa mwaliko kwa watu kupeleka ushahidi wao huko?

Sasa sijui Gwajima keshaupeleka huo ushahidi wake....
 
usiwe na shida gwajima alisema anavyo mezani anasubiri mkulu atafanya nini asipofanya lolote yeye atavitoa. Tunasubiri tamko la baba
Hahahaaa huyo Gwajima si ndo yeye huwa anafufua wafu pia?

Au si yeye?
 
Unasema niachane na Makonda kwani mimi ndo nimemganda?

Kwanza we mwenyewe mbona umeshindwa kuachana na mimi hapa?
Ninmesema hivyo kwa sababu wewe umekomaa na watu kuwa wakupe ushahidi ili umshukie Makonda.
Sasa mimi lazima nihoji kama ni lazima umshukie?
Kama watu wanapiga blabla bila ushahidi wewe si uendelee na mambo mengine?
 
Ndugu Nyani Ngabu kinachonisikitisha ni kwanini mnawalaumu hawa "walalamikaji" wa kwenye media badala ya kuwalaumu mamlaka husika polisi na vyombo vingine kwa kukaa kimya na kutokufanya uchunguzi na kuja kuclear doubt au wamuombe Makonda mwenyewe aje afanye clearance kama si kweli:
Hili ni kosa la jinai (uhalifu) kuwa umefanyika kwanini polisi wapo kimya.

I wonder why police need to be moved to take action on this. Tumeona hata practice polisi wetu si lazima wamuvuzishwe popote pale wanapoona pana harufu ya uhalifu huingia hata bila kuambiwa iweje sasa this criminal offense is alleged to be done nao wapo kimya?

Polisi utendaji wao ni tofauti na mahakama tumezoea mahakama wanamsemo kwamba "the court is not your mother cannot give you what you didn't ask" kwamba mahakama ni lazima imuvuzishwe hata jaji akiwa amepata taarifa kuwa kuna mtu ameuawa au umezurumiwa hawezi kujihusisha na hiyo kesi mpaka imeletwa mahakamani na usipoileta shauri yako hiyo ndiyo maana ya "mahakama siyo mama yako haiwezi kukupatia usichokiomba"

Lakini kwa polisi ni tofauti akipata taarifa kuwa kuna mtu ameuawa lazima achunguze haijarishi taarifa hizo ameziona kwenye gazeti, mtandaoni au popote.

Iweje hili swala la Makonda wasubiri mtu akaripoti eti? Hizo taarifa za kiintelejensia zipo wapi?
Mbona linapokuja swala la uchochezi wanafanyia kazi taarifa za mtandaoni? Kwanini?.

Mwisho.
Hii ni kesi ya jinai polisi ndiyo wanatakiwa kuonesha interest mpaka sasa wapo kimya eti wanasubiri taarifa rasmi isipopelekewa hiyo ripoti basi mtuhumiwa aendelee kuenjoy good life in the cape of Good Hope of south Africa?

Na hao waliosimamisha ajira zote wakikagua vyeti nao wanasubiri taarifa rasmi?

Just imagine hizi tetesi zingekuwa juu ya uwepo wa magaidi wa amboni au ujambazi BOT wangebaki ofisini wakisubiri taarifa rasmi?
Hao akina Gwajima and co. unawaita walalamikaji?
 
Kwakweli kama ushahidi upo wamburuze mahakamani...
hizi bla bla zinazoendelea hazina mantiki yoyote!!!

Halafu waTanzania ni vigeugeu sana...
baada ya mwaka mmoja mtasema mbona mateja wamejaa viongozi wako wapi
 
Sasa kama kila katuhuma Mange anakokasema lazima katolewe maelezo itakuwa Taifa la ajabu sana.

Ah wee...huyo tena akishasema basi. Hakuna kuhoji. Ni kumeza tu kama Fanta Orange vile.

Na hahitaji kutoa ithibati yoyote ile. Anachohitaji ni kuandika tu huko sijui ndo Instagram, baaaasi. Hakuna kubisha, kudadisi, wala kuhoji.

Mie naamini tuhumu za kutolea maelezo ni zile zilizoambatana na ushahidi, kama vile living certificates za Paul na Daudi zilizo na picha. Lakini mtandaoni tu ujibu tuhuma, itakuwa uhuni uliopita kiwango.

Umeelezea vizuri sana hapo. Unanidai Heineken.
 
Watu wa kanda ya ziwa utawajua tu.
Hata wale waliokuwa na misimamo huko nyuma, kwenye utawala wa mtu wao wanaleta ngonjera.
Vipi...we unao ushahidi wa Paul Makonds na Daudi Bashite?
 
Ninmesema hivyo kwa sababu wewe umekomaa na watu kuwa wakupe ushahidi ili umshukie Makonda.
Sasa mimi lazima nihoji kama ni lazima umshukie?
Kama watu wanapiga blabla bila ushahidi wewe si uendelee na mambo mengine?

Niendelee na mambo mengine?

Mbona hata kuomba ushahidi napo ni kuendelea na mambo mengine tu....

Vipi, we unao ushahidi wa Paul Makonda na Daudi Bashite?
 
Majibu ya Ole sendeka nakumbuka yaliletwa tena yakiwa katika list ya wenzake, kwanini ya Daudi bashite hayaletwi tunasikia kelele tu.. Hakuna karatasi yoyote ya kuonyesha matokeo, tunasikia tu alipata ziro, akachukua cheti cha mtu lakini hatuyaoni
 
Kwakweli kama ushahidi upo wamburuze mahakamani...
hizi bla bla zinazoendelea hazina mantiki yoyote!!!

Halafu waTanzania ni vigeugeu sana...
baada ya mwaka mmoja mtasema mbona mateja wamejaa viongozi wako wapi
Watanzania tu watu wa ajabu sana.

Majuzi tu hapa walisema Makonda ana sijui magari ya kifahari..majumba..manini nini sijui....lakini yote hayo sasa yashapita.

Kinachobamba ni Daudi Bashite.

Na sina shaka kabisa siku Makonda akiamua kuhamia CHADEMA atapokewa kwa matarumbeta na mavuvuzela.

You watch....
 
hivi haya yote yalianza baada ya Mbowe/Gwajima/Manji kutajwa?

maana naona sasa hivi CDM wengi wanaipinga hio vita ya madawa, na kusapoti tuhuma za chini chini dhidi ya Mkuu wa mkoa wa Dar...

Ifike mahala kila kitu kisihusishwe na siasa.
maana hata viongozi wakikosea hamtaona makosa kwa sababu ni viongozi wenu katika vyama vyenu vya siasa.

Alieturoga ni wakati sasa wa kutuagua
 
Watanzania tu watu wa ajabu sana.

Majuzi tu hapa walisema Makonda ana sijui magari ya kifahari..majumba..manini nini sijui....lakini yote hayo sasa yashapita.

Kinachobamba ni Daudi Bashite.

Na sina shaka kabisa siku Makonda akiamua kuhamia CHADEMA atapokewa kwa matarumbeta na mavuvuzela.

You watch....
Tuombe uhai,jumapili hii Gwajima kasema rasmi anavaa sucide vest na anatiririka na viashiria vyote-proof kamili mpaka waalimu na wanafunzi-tuombe tuu hii misa isifanyiwe figisu figisu-na itakuwa live you tube
 
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
Kama lema amekosa dhamana kwa dhamana iliyowazi kisheria .,na Dunia nzima inashudia .,hata kwa daudi bashite mwana kipenzi wa mtukufu ,ni mahakama ipi itajali kama mahakama zinaamuriwa zitoe maamuzi ya mkutufu aonavyo inafaa.
[HASHTAG]#reference[/HASHTAG] ;dhamana ya Lema.
 
In short the allegations can be true but timing is very poor....why this time? Any sane person will know to it as a hit back from the drug lords using ducks mouth....Makonda has been in power since JK's reign and no one had come up against his qualifications, why this time then? Eti JPM amtumbue, for whose benefits? Or u drug lords wanna show the public that ur untouchable and can win the war against the state?not this time brothers....Makonda can be Daudi but his actions justify him to be the RC and after all his position is a presidential pleasure and there are no pre-qualifications.....
 
Back
Top Bottom