Na ndiyo hoja ya NN kuwa wenye ushahidi kwanini wasiende mahakamani? Hapa tupo pamoja
Upande wa pili, kukamatwa Gwajima kulikuwa na taharuki kwasababu ni maarufu na ana kundi nyuma yake. Hakuna ushahidi uliopatikana kama ilivyo kwa tuhuma za Mange n.k.
Like wise madai yanayotolewa na 'almaarufu' Gwajima yanabeba uzito ule ule aliyoubeba wakati anatuhumiwa. Si lazima Paul ajibu, lakini kuna political impact hapa
Ukiwa na Ng'ombe 10 mtaani pengine hawatajua kama una zizi.
Ukibeba kilo moja ya nyama iliyooza Wilaya nzima watajua maana hiyo ndiyo habari
Paul ni mwakilishi wa Rais.
Ana njia mbili, kusema si kweli au ni kweli au njia ya pili ni kukaa kimya.
Kwa mtu aliyezoea kutumia media inapotokea akakaaa kimya hoja ya
Gamba la Nyoka (Tacitly accepting allegations) inabeba nguvu
Tatizo, Paul atakuwa kilo moja ya nyama iliyooza itakayozungumzwa kila uchao
Akiwa mwakilishi wa Rais, atambebesha Rais kilo moja ya nyama iliyooza na kuwa story hata kama Rais ana ng'ombe 1000 walionona.
Zoezi zima litakuwa halina maana kwasababu linagubigwa na ambiguity ya double std
Kwavile alitumia media kuwatuhumu watu wengine bila ushahidi kama Gwajima, what goes around comes around, anajikuta automatic analazimika kusema neno