Mwanafalsafa
Platinum Member
- Jun 24, 2007
- 662
- 851
Akili na ustaarabu unaanzia kwenye mipango miji.
Kama kuna Rais anayetafuta legacy ya kudumu asimamie mipango miji. Mipango miji ni legacy ya milele. Ukishapanga mitaa na barabara zitabaki hivyo milele. Ukishindwa kupanga kuja kurekebisha ni ngumu sana. Gharama yake ni kubwa sana kiasi kwamba huwa haiwezekani. Sasa mtu akija kwenye nchi zetu hizi za Afrika lazima atuone ni wapumbavu tu kama tunashindwa kitu kidogo sana na kisichohitaji akili kubwa cha kupanga miji na kunyosha makazi.
Watu wanaweza wakajenga nyumba za kifukara za mabanda lakini wazjenge katika mitaa iliyonyooka. Siku nchi ikitajirika au wananchi wakitajirika watabomoa vibanda hivyo na kujenga nyumba za kisasa.
Lakini huwezi kujenga barabara na mitaa iliyonyooka na ya kupendeza kama hukupanga mji na kuweka nafasi ya barabara zilizonyooka na zenye nafasi. Utafanya kwa kiasi kidogo tu kwa sababu gharama za kunyoosha mji ambao haujapangiliwa ni kubwa sana.
Tuanzie hapo kwanza ndo maendeleo tutayaona. Kuna faida nyingi sana kiuchumi za kuwa na miji na makazi yaliyopangiliwa. Usambazaji wa huduma na bidhaa unakuwa rahisi. Unaweza ukajenga kwa urahisi mifumo ya kusambaza huduma ambazo zina mchango mkubwa sana katiba pato la taifa kama vile mabomba ya maji, mabomba ya gesi, nyaya za mawasiliano (internet na cable TV), na kurahisha usafirishaji wa bidhaa na hivyo kuchochea biashara kwa njia ya Posta.
Mifano ya maeneo ambayo ni ngumu sana kuja kuyanyoosha ili yaoneshe kuwa hii nchi ina watu wenye akili:
Dar es Salaam
Oysterbay (kushoto), Namanga (kulia)
Mwanza (Mabatini)
ONA NYUMBA ZA KIMASKINI LAKINI ZIMEPANGILIWA ZINAVYOPENDEZA. HAPA HATA NDO UTAJIRI UKIPATIKANA BAADAE NI RAHISI KUPABORESHA PAKAPENDEZA ZAIDI.
Kambi ya Wakimbizi Kasulu (Hii ni kazi ya UN ndo imepanga hiki kijiji cha kimaskini nyumba zimenyooka)
Hii ni Nepal, kuna tajiri kajenga nyumba hizi za kimaskini kwa ajili ya watu wa kipato cha chini waweze kuishi vizuri. Ona zinavyopendeza kwa jinsi zilivyopangiliwa:
KUONESHA NI JINSI GANI WATANZANIA TUKO NYUMA KABISA KATIKA MIPANGO MIJI (YAANI HAIPO KABISA KATIKA AKILI ZETU) ONA HATA MAKABURI YETU YALIVYOKAA SHAGHALABAGHALA.
Haya ni Makaburi ya WaTanzania:
Linganisha na Makaburi ya watu ambao suala la mipango miji liko kwenye damu zao tayari. Haya ni makaburi ya wazungu na wahindi waliokufa katika vita ya pili ya wazungu (1938-1945), yako Dar es Salaam jirani na Nyumba ya Sanaa.
Na haya ni makaburi kutoka nje ya nchi:
Mimi nakerekwa sana SANA na serikali yetu jinsi ambavyo inaachia watu wajenge makazi holela holela tu. Serikali inakuwa wapi kutoa amri ya kwamba ni marufuku kujenga eneo lolote ambalo halijaingizwa katika mipango miji?
Katika suala la kuunda utitiri wa Mamlaka (Executive Agecies) kwa nini isiunde Mamlaka moja ambayo kazi yake itakuwa ni moja tu... kuhakikisha hakuna jengo lolote linalojengwa nje ya mpango mji?