Balozi Polepole saidia maafisa mipango miji/ardhi wakajifunze Cuba

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Polepole akiwa katika mahojiano na Jenerali Ulimwengu mojawapo ya mambo aliyoisifia Cuba ni upangaji miji kwa ustadi mkubwa sana. Anasema mitaa Cuba imepangwa vizuri sana kiasi kwamba unaweza kuchora mstari ulionyooka kwa rula mtaa mzima bila hata nyumba ya mtu mmoja kutoa pua nje ya mstari.

Kwa kuzingatia matatizo makubwa yaliyoko Tanzania katika upangaji miji ni vyema Polepole awasiliane na Jerry Silaa, Wizara ya ardhi na TAMISEMI wapeleke maafisa ardhi na mipango miji kujifunza Cuba namna bora ya kupanga miji yetu.
 
Hao wataalam wako maofisini tu, hawajawahi kufika kwenye maeneo kabla hajajengwa. Wao husubiri miji ijae ndio waje kwenye migogoro.

Ndio maana hadi hifadhi zetu zinavamiwa.
 
Back
Top Bottom