Kama ilivyokuwa kwa Mtikila kufungua kesi ya Mgombea Binafsi, Tundu Lissu kufungua kesi kuhoji ni kwanini matokeo ya Urais hayapingwi Mahakamani!

Hii sio tu sheria kandamizi, ni uzwazwa kukubali kuitumia
 
Akili ndogo inayoongozwa na akili ndogo pia
 
Hivi mleta mada unajua Tanzania ni monist state na siii dualist state
Uwe unafanya tafiti angalau kidogo
Huko mahakama ya Africa mashariki maamuzi yake yana ibind Tanzania?
Hata kama hayaibani lakini yanaivua nguo Tanzania katika jumuiya ya kimataifa kwa uozo wa watawala
 
Mkuu, jifiche au futa kabisa uzi wako huu. Kumbe hufahamu hata kazi za mahakama. Sheria za taratibu zote zimetungwa au kupitishwa na Bunge. Hujawahi kusikia Mahakama hutafsiri sheria?? Mbona mahakama hizi hizi zinatengua ubunge, udiwani nk??

Hapa kinachotakiwa ni tafsiri ya katazo hilo. Sio kuiondoa. Usitumie hasira kujadili mambo usiyofahamu vizuri.

Unaweza kuona kisima kimoja ni jambo la muhimu kama unahitaji maji. Ni sawa na kesi hii kama unahitaji haki. Unadhani matokeo ya Zanzibar 2015 Seif Hamad hakuhitaji haki ya mahakama??
 
Mahakama ya Tanzania haina mamlaka ya kusikiliza shauri lolote kupinga matokeo ya uraisi
Kasome election act mkuu ya 1985 na katiba ya 1977
 
Wewe bado mvulana saana, sasa subiri uone kama anaweza kushinda.
Tundu.lisu hajui sheria nae anabahatisha tu na wakati mwingine ana wa rob mahakim mambo yake yanashinda lakini sio mjanja kiivyo.
Walizoea zamani mahakim na waendesha mashitaka hawakujali ila kwa sasa wanakutana na vyuma mpaka majasho yanawatoka.
Hapo kenya majaji walitengua ushindi, mara ya pili wakabalance mpaka leo odinga aliangukia pua.

Rasimu pendekezwa(2014), chini ya Tume ya Jaji Warioba ilikuwa inaruhusu matokeo ya Rais kupingwa mahakamani, waTz wazalendo tunamlaumu sana JK kutunyima katiba Mpya.
 
Rasimu pendekezwa(2014), chini ya Tume ya Jaji Warioba ilikuwa inaruhusu matokeo ya Rais kupingwa mahakamani, waTz wazalendo tunamlaumu sana JK kutunyima katiba Mpya.
this time wataachia tu. Ngoja mambo yaanzae !
 
Mahakama ya Tanzania haina mamlaka ya kusikiliza shauri lolote kupinga matokeo ya uraisi
Kasome election act mkuu ya 1985 na katiba ya 1977
Ninajua sana lkn hapa haifunguliwa kesi ya hivyo inafunguliwa kesi ya kwa nini Sheria na Katiba haziruhusu kesi za kupinga matokeo ya Rais. Umeelewa sasa?
 
Ninajua sana lkn hapa haifunguliwa kesi ya hivyo inafunguliwa kesi ya kwa nini Sheria na Katiba haziruhusu kesi za kupinga matokeo ya Rais. Umeelewa sasa?
Mbona kama jibu lake ni rahisi..judge au hakimu atamwambia yeye atungi Sheria au katiba, KAZI ya judge na hakimu ni kutafsiri tuu..pengine Lissu angejaribu kupereka lalamiko lake Kwa wananchi(Kwa kupitia chama chake) ili wampe wabunge wengi watakaomsaidia kubadili hiyo Sheria/kipengere katika katiba yetu..but as long as watunga Sheria walio wengi wako comfortable na Sheria zilizopo , Lissu atapata taabu Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…