Kama dunia inazunguka kwanini hatumwagiki?

Kama dunia inazunguka kwanini hatumwagiki?

Kwanza wanatuambia dunia ni duara, pili tunaambiwa tupo nje ya dunia na sio ndani ndio sababu tunaliona jua, duh. Sasa mi najiulizaga, hivi ingekuwa dunia ni duara, si kungekuwa na miteremko kila upande wa huo mduara, bahari zingekaaje, kuna ziwa, mito. Maji yote yangeshamwagika. Kaazi kwelikweli. Halafu inawezekanaje dunia ikawa inazunguuka, halafu mtu kama umezaliwa Arusha, unaishi hadi unazeeka, upo palepale. Mzunguko haukuhamishi, mfano mkoa upo mashariki, ukizunguka si utaenda labda kusini, basi ulione jua kwa upande huo. Lakini wapi. Endeleeni kutudanganya wasomi. Tunaambiwa kuna sayari, nazo ni kubwa kweli kweli, hatuzioni. Na hatutaziona hadi mwisho wa dunia.
Hahaaaa sio mwisho wa dunia mpa ufwe awa wazungu washenzi sana.
 
Kwanza kabisa, dunia ina mizunguko ya aina mbili,...
1.Kuzunguka jua
2.Kujizungusha kwenye mhimili wake.
Kuhusu kutomwagika sayansi inasema hivi,
1.Kuzunguka jua, matufe anga zinavutana kwa Kani mvutano ambayo ni F=Gm1m2/r2, kwa kifupi hii kani inaleta msawazo kati ya sayari na jua ambalo ndio kitovu kikuu cha mfumo wa jua ili sayari kuweza kubaki kwa njia yake bila kumwagika. (hapa fikiria umefunga kamba jiwe na halafu unashika ncha ya kamba na unalizungusha huku wewe( au mkono ukiw kama ndio jua na jiwe ni sayari)

2.Kwenye mhimili wake:Kani ya uvutano kati ya dunia na kitu kilichopo juu ya uso wa dunia ndio inayofanya tusimwagike, F=mg, ambayo pia inaathiriwa na umbali n uzito wa kitu husika kutoka katika kitovu cha dunia ndio maana meli anga" space ship" zikifika umbali fulani zinakuwa kani mvutano ndogo sana hivyo kuonekana kama zinaweza kumwagikia huko angani......
(Hapa fikiria kwanini ukiruk unarudi chini au chukua jiwe rusha juu na linarudi chini)

Kwa hiyo ni kani ya mvutano ambayo huelezewa kwa namna mbalimbali ndio husababish sisi kutokumwagika

Wasallam
 
Ni swali gumu kidogo hasa katika kukuelewesha vile ilivyo; iko hivi,,, kwanza ukumbuke kuwa dunia ina mizunguko miwili
1. dunia kulizunguka jua
2.dunia kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake;
Katika mzungunguko wa pili yaani dunia kujizungusha yenyewe ndio hasa inayozungumziwa,,
Wakati dunia inajizungusha hatuanguki kwa sababu sisi wenyewe ni sehemu ya mzunguko huo, na pia dunia ni kubwa sana na sisi ni wadogo kiasi kwamba siyo rahisi kuhisi mzunguko huo. lakini pia hatuwezi kujikuta tuko sehemu nyingine kwa sababu hata sehemu hizo nazo huzunguka pia, kwa hiyo tunajikuta tuendelea kuzunguka muda wote ule. Katika mzunguko huo ndio hupelekea kutokea kwa usiku na mchana,,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom