Kama dunia inazunguka kwanini hatumwagiki?

Kama dunia inazunguka kwanini hatumwagiki?

"Nakumbuka shuleni tulisoma dunia inajizungusha" bwana we mtaongezea maneno siunajua enzi zetu divison5 @ naomba msaada kwa nini hatuhisi kuzunguka?
Kwa nini maji hayamwagiki baharini?
Kwanini hatujikuta tuko ulaya tule maisha maana uwezo wa kupata viza sijui passport maana sielewi hata...
Wataalamu nipeni elimu
Ungeanza na kujieleza kuwa kiwango chako cha elimu ni kipi. Nahisi maelezo mengine yanaweza kukuzidi uwezo na kukuchanganya zaidi kama shuleni ulifundishwa bado hukuelewa basi watu wachangie kulingana na kuwa jiografia ya ulipoishia ilikomea wapi na uongezewe wapi.
 
je

ukiwa ndani ya bus ukarusha sarafu juu huku basi likiwa speed sarafu hiyo itatua usawa uleule mikononi mwako au?

vipi mdudu kama nzi anayeruka ndani ya bus lililo speed...!

vipi kuhusu helicopter inayoshusha wanajeshi huku ikiwa imesimama angani nayo inavutwa na kuzunguka pamoja na dunia?
Sina majibu lakini apa naona una maswali ya msingi mkuu ila wenye majibu ngoja waje kukujibu
 
je

ukiwa ndani ya bus ukarusha sarafu juu huku basi likiwa speed sarafu hiyo itatua usawa uleule mikononi mwako au?

vipi mdudu kama nzi anayeruka ndani ya bus lililo speed...!

vipi kuhusu helicopter inayoshusha wanajeshi huku ikiwa imesimama angani nayo inavutwa na kuzunguka pamoja na dunia?
Sijakuelewa ebu rudia
 
"Nakumbuka shuleni tulisoma dunia inajizungusha" bwana we mtaongezea maneno siunajua enzi zetu divison5 @ naomba msaada kwa nini hatuhisi kuzunguka?
Kwa nini maji hayamwagiki baharini?
Kwanini hatujikuta tuko ulaya tule maisha maana uwezo wa kupata viza sijui passport maana sielewi hata...
Wataalamu nipeni elimu
Hahahhahhahhah..... you made my day
 
According to wanasayans

Dunia pamoja na vitu vilivyomo ndan yake tupo kwenye speed sawa na mzunguko wa dunia yapata speed ya 10000km kwa dakka moja ivo hiz movement tunazozifanya zipo katika speed ambayo unaweza ukaipuuzia(neglect)

Kwa mfano chukua jiwe zen weka kwenye kopo halaf hilo kopo lifunge kamba halafu anza kulizungusha utakuja kugundua kwamba jiwe ndani ya kopo litakaa katika sehem moja bila kuzunguka ovyo ..nwton first law of motio

Jamaa una matango pori wewe, mifano yako hata haiendani na kuzunguka kwa dunia na hilo kopo!!!

TAFADHARI KAMA HAUELEWI KUHUSU CENTRIFUGAL FORCE NA GRAVITATIONAL FORCE, husizungumze!

Mfano wa kopo ulio toa ni wa centrifugal force wakati ili uweze kuwa intact ktk uso wa dunia ni lazima gravitational force iwe kubwa kuliko centrifugal force.

Jibu kwa mleta mada ni kwamba; hatumwagiki kutokana na kani ya gravitaty ambayo inavuta kila kitu kuelekea ktk kiini cha dunia ndio maana ukirusha jiwe haliendi juu litashuka chini... lakin kwenye mwezi jiwe halitoshuka chini
 
Speed ya dunia ni kubwa lakini pia ni constant ndo maana huwezi kuhisi hiyo motion mfano ni kama gari lipo kwenye Barbara nzuri halafu linakimbia speed kubwa kama halijabadili gia unaweza hisi kama haliendi vile ni kwa sababu na ww unatembea na gari katika same speed au ukiwa kwenye lift huwezi hisi motion mpaka lifti ikisimama

Mmh speed kubwa!! Embu iweke ktk namba hiyo spidi
 
Ukikaa ndani ya meli inayotembea kwa ndani wakati hakuna mawimbi huwezi jua kama meli ipo kwenye mwendo.
Lakini ukiangalia nje unaona miti majumba na uoto wa asili unatembea.
Mbona sisi tunaokaa ndani ya dunia inayokimbia hatuoni nyota ambazo haziko ndani ya hiyo Atmosphere zikitembea kama tunavyoona kwenye meli inayotembea ?
Mi najua kuwa Nyota na Jua havipo ktk Atmosphere ya Dunia.
Lakini cha ajabu Jua na Mwezi tunaona vinatembea, lakini Nyota hazitembei.
Kwanini Jua na mwezi vitembee, ila Nyota zibaki bila kutembea ?
Wakati zote zipo nje ya Atmosphere ya Dunia ?

Jua halitembei, lipo static katika sehemu yake.
Mwezi unatembea na ndio unaizunguka dunia na ina orbit yake spesho.. lakini dunia inalizunguka jua. Atmosphere ni tabaka linalolizunguka dunia pekee.

Kwanini mwezi unatembea?
Itabidi kurudi mwanza kabisa mwezi ulitokeaje.. hilo ni somo refu lkn mwezi una uhusiano mkubwa na dunia na ndio unao determine majira ya mwaka,
 
WATU WAJINGA, MI NIMETOA MFANO WA GARI, MTU UKIKAA KWENYE GARI IKAWA INATEMBEA UTAMWAGKA? KWA SABABU SPEED YA GARI IKO SAWASAWA NA MZGO ULIOBEBWA, NA NDIYO MAANA DEREVA AKFUNGA BREK ZA GHAFLA HULETA SHDA, THE SAME TO DUNIA, INAVYOZUNGUKA HUZUNGUKA KWA SPEED COSTANT PAMOJA NA KILICHOBEBWA KTK DUNIA, NA KAMA INGETOKEA DUNIA IKASMAMA GHAFLA BAS UNGEONA JINS UTAKAVYOMWAGKA KAMA KWENYE GARI DRIVER ANAVYOFUNGA BREK ZA GHAFLA AU KUENDESHA OVYO.

MFANO WA PILI NI NDEGE INAVYOKUWA ANGAN INAKIMBIA KWA SPEED KUBWA LAKN U DONT FEEL KAMA INAKMBIA, HATA MHUDUMU WA NDEGE ANAPOKUHUDUMIA KULE ANGANI KWA KIKOMBE CHA CHAI, WALA CHAI HAITINGISHIK, KWA SABABU SPEED YA NDEGE INAKUWA COSTANT NA KILA KILICHOBEBWA KWENYE NDEGE, ILA IKTOKEA NDEGE IKABADILI SPEED GHAFLA HAPO NDO UTAKAPOJUA KWAMBA NDEGE ILIKUWA INAZUNGUKA.
 
kweli elimu yetu ya Tanzania ni bure kabisa.. huyu mtu msikute kamaliza mpaka form four.. ila tu concept ndogo sana kama hio kashindwa kuifahama hata google haimsaidii
 
Kwa sababu Dunia ni flat ndo mana hatumwagiki.

Kuna theory nyingi zinazozungumzia juu ya shape ya dunia
- dunia ni flat
- dunia ni oblate spheroid


Jiulize dunia ingekua flat usiku na mchana unatokea vipi?
Theory yenye nguvu kubwa na evidences nyingi ni iyo ya dunia ni oblate spheroid
 
Mda mwingn naona sayansi inatudanganya vingi tu japo kuna watu watabisha kwa kutumia maandiko waliyokariri kutoka kwa wqzungu

Wewe unamatatizo tena makubwa tu.
Kama huiamini sayansi ukiumwa huwa unaendaga wapi?
 
lwiva NILIVYOSEMA DUNIA SYO KAMA MWENDO WA GARI NIMEMAANISHA MWENDO WA DUNIA NI COSTANT.. GARI HUTEGEMEA DEREVA, BARABARA, UBORA WA CHOMBO N.K! KWA MFN DEREVA ANAWEZA FUNGA BREK GHAFLA HUMO NDAN MKAANZA KUANGUKIANA OVYO, ILA DUNIA HAIWI HVYO.
 
prenge DUNIA HAISIMAMI, IWE MCHANA AU USIKU KWA SABABU KWA SIKU DUNIA HUJIZUNGUSHA KTK MHIMILI WAKE KWA MASAA 24. KWA HYO WAKAT WEWE HUKO KWAKO NI USKU, KUNA MAENEO NI MCHANA, ASUBUH NA HATA JIONI, KUNAVYOPAMBAZUKA TAFSIRI YAKE NI KUWA DUNIA KWA UPANDE AMBAO WEWE UPO, IMEFKA SEHEMU YA USAWA WA JUA... NA HAPO NDPO UNAPOCONFIRM PIA KUWA DUNIA NI DUARA KWA 7BU DUNIA INGEKUWA FLAT, BS MUDA UNGEFANANA NA KUSIKNGEKUWA NA GIZA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom