Kama dhana ya Time travel ingekuwa kweli, na ukapata nafasi ya kurudi nyuma ya muda ungemuonya au kumshauri nini (wewe-mdogo) kwa kile unachokiishi?

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,732
10,037
images.jpeg

Dhana ya Muda ni pana sana. Dhana hii inazidi kuchanganya zaidi wanasayansi na watafiti mbalimbali ili kujua muda unafanya vipi kazi. Je kuna uwezekano wa kusafiri mbele ya muda uliopo au nyuma ya muda uliopo? Mambo bado ni magumu.

Lakini kama dhana hii ingefanikiwa na binadamu wakawa na uwezo wa kurudi nyuma ya muda au kwenda mbele ya muda na wewe ukapata nafasi hiyo adhim kurudi nyima ya muda ukakutana na wewe mdogo (wewe kipindi cha udogo wako).

Je ni ungefanya au ungemwambia kitu gani ambacho katika enzi zako uliteleza, au hukujua unafanya nini na mwisho wa siku kikaja kukuletea matokeo hasi mbele ya maisha yako?
 
Kama una kipaji kitunze & Kaza...!
Sikuweza kukaza kwenye mpira n Kujitunza
 
Kupiga sana chini! That was awful! Historia inanikeraga sana hiyo to be honest
 
View attachment 2653196

Dhana ya Muda ni pana sana. Dhana hii inazidi kuchanganya zaidi wanasayansi na watafiti mbalimbali ili kujua muda unafanya vipi kazi. Je kuna uwezekano wa kusafiri mbele ya muda uliopo au nyuma ya muda uliopo? Mambo bado ni magumu.

Lakini kama dhana hii ingefanikiwa na binadamu wakawa na uwezo wa kurudi nyuma ya muda au kwenda mbele ya muda na wewe ukapata nafasi hiyo adhim kurudi nyima ya muda ukakutana na wewe mdogo (wewe kipindi cha udogo wako).

Je ni ungefanya au ungemwambia kitu gani ambacho katika enzi zako uliteleza, au hukujua unafanya nini na mwisho wa siku kikaja kukuletea matokeo hasi mbele ya maisha yako?
Ingetokea nimesafiri nyuma ya muda na kukutana na Mimi mdogo ningemshauri asioe,tunakaa na mi mwanamke kumbe inatalaka tayari bila mume kujua,mm lakwangu nimeligundu,na nimeificha halijui,haya makitu hayajui nn yanahtaji in life,wanaume stukeni,wake zetu wanatalaka mkononi
 
mimi ningejishauri kutochukulia poa TATIZO hasa linalohusu afya. Macho yangu yamepata changamoto kutokana na kuchukulia poa .....kuja stuka Hali imekuwa mbaya japo nashkur Mungu naweza kuona mpaka sasa Kwa kiasi ambacho amenijaalia kuona.🙏
 
Back
Top Bottom