Time travel inaenda sambamba na cosmology

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Hakika kama utakuwa huna hufahamu wowote ule wa kipengele cha Cosmology basi hutaweza kuelewa chochote kuhusu concept ya time travel nazungumzia ile theory ya kusafiri katika kipindi fulani cha muda huko katika space and time

Cosmology ni moja ya tawi la astronomy ambapo katika eneo hili tunaweza kujifunza mengi sana kuhusu asili yote ya chimbuko la ulimwengu wetu na maendeleo yake kutokea ulimwengu ulipo anza mpaka ulipo na unapoelekea

Moja kwa moja tukianza kuzungumzia suala zima la cosmology moja kwa moja tutakuwa tunazungumzia kitu kinachoitwa muda yaani vipindi vingi au mbalimbali vya muda kutoka wakati ule uliopita na huu wakati wa sasa na ule wakati ujao , kwa lugha laini huo ndio muda unaozungumziwa katika concept mbalimbali za muda katika ulimwegu wetu

Kwa lugha nyengine elimu ya cosmology hujaribu kuelezea ni namna gani ndoa kati ya Space and time ilivyo kwasababu tangu ulimwengu ulipoanza kuwepo basi space ilianza ule ushirikiano mama na muda yaani tangu muda huo kokote kule kutakapo kuwa na space basi kuna muda kwakuwa ulimwengu unatoka eneo fulani au tuseme unatanua kutokea eneo fulani na kuelekea eneo lisilojulikana , hivyo unasafiri kutokea katika kipindi cha awali na kuelekea katika kipindi kijacho ambacho mimi na wewe hatukifahamu au huenda kipo

Nawezaje kusafiri au nawezaje kuwa msafiri kwa kufuatiliza nadharia hii ya Time travel

kama nitataka kurudi katika baadhi ya makundi ya nyota yaliyoko umbali mrefu sana kuelekea katik kiini cha cha ulimwengu wetu basi ni wazi nitakuwa naendea matukio ya nyuma yaliyopita kwakuwa kwa mujibu wa wanasayansi wanasema kundi letu la nyota lipo katika hali ya usasa sijui niseme labda hali ya katikati katika muda wa ulimwengu wetu

Moja kwa moja kama nitayarudia hayo makundi mengine ya nyota yaliyoko nyuma basi nitakuwa nimesafiri kurudi katika kipindi kile kilichopita na kama nitasafiri tena kurudi duniani basi nitakuwa nimerudi katika muda wa mbele kutokea katika muda wa uliyopita

Kwa hali yetu sisi wanadamu wa duniani ni ngumu kuweza kufanikisha tekinolojia hii kwakuwa tuna uhaba wa vitendelea kazi kama vile time machine na kwa mujibu wa mwanasayansi Albert Eistein alisema hata kama hautokuwa na time machine basi unaweza kufanikisha suala hili pale pindi utakapoweza kuona yale matobo yaliyopo katika spacetime ambayo moja kwa moja huonganisha baina ya sehemu moja hadi nyengine katika spacetime

Nimejaribu kuelezea kwa Maelezo laini sana ambayo hayatakuwa na shida kwa wasomaji mbalimbali ..
 
Hapa JF hizi mada sio mahali pake siku hizi, wanatakwambia hii ni chai bila vitafunwa.
Ndio maana wanapita juu kwa juu

Lets take a trip to infinity...
 
Back
Top Bottom