Kama CCM wakifuata utaratibu wao wa kutompinga Rais aliyepo katika kuteua mgombea, basi Samia Suluhu anaweza kuwa Rais wa Tanzania kwa miaka 14

Hata mimi nashangaa kayatoa wapi haya maneno?

Manaake katiba unasema kabisa kama Makamu wa Rais atapata urais kwa sababu yoyote ile ya Rais kufa/kujiuzulu au kuacha kutokana na ugonjwa katoka kipindi kisichozidi miaka 3 ndo anaweza kugombea term 2 ila SSH amepata urais kwa miaka 4 kwahiyo anaruhusiwa kugombea mara moja tu(2025-2030) kwahiyo sana sana anaweza kufikisha miaka 9 tu si zaid ya hapo
Atake asitake ataongezewa muda tu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ungepitia katiba kwanza kabla ya kutoa maoni haya.

40.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti hicho.

(2) Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais.

(3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar hatapoteza sifa za kuweza kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa
sababu tu kwamba aliwahi kushika madaraka ya Rais Zanzibar.

(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.

Ibara ya 37(5) inayorejelewa hapo kwenye ibara ndogo ya 4 inasema hivi:

(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu
kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwakutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Raisataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindicha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopunguaasilimia hamsini ya Wabunge wote.

Rais Samia kachukua madaraka mwezi March 2021, Magufuli alichaguliwa na kuapishwa November 5, 2020, hivyo amekuwa rais kikatiba miezi 4 na siku 17 assuming alikufa tarehe 17 March 2021. Kwa hiyo Rais Samia ana miaka 4 na miezi 8 na siku 13 za kutawala, kipindi ambacho tayari kinazidi muda uliotajwa katika ibara ndogo ya 4 hapo juu. Kikatiba hiki ni kipindi sawa na miaka 5 na hivyo Rais Samia ataruhusiwa (kama atataka) kugombea kipindi kingine kimoja tu.

Nashauri watanzania tuisome katiba yetu hata kama ni mbovu kwa sababu ndiyo inayotuongoza kwa sasa.
Shukran sana
 
Kumekuwa na ubishi kuhusu kama kwa sasa Samia Suluhu anaongoza awamu ya tano au ya sita. Labda hilo sio jambo la maana. Jambo la msingi ni kwamba rais Samia Suluhu anaongoza awamu ambayo haitambuliki kikatiba kama ni awamu yake ya kwanza ya uongozi, bali amechukua madaraka ya uraisi kutokana na kifo cha rais aliyekuwapo madarakani. Samia hakuchaguliwa kwa kura, hivyo uraisi wake wa sasa ni wa kuziba pengo tu.

Kwa jinsi hiyo basi, awamu ya kwanza ya Samia Suluhu itakuwa mwaka 2025 ikiwa CCM watampitisha kuwa mgombea wao wa uraisi. Na tukumbuke kwamba CCM wana utaratibu wa kumpitisha raisi aliyepo madarakani kuendelea kuwa chaguo lao la mgombea urais.

Ikiwa Samia atagombea urais mwaka 2025 na kupita, itakapofika uchaguzi wa 2030 atakuwa tena na haki ya kikatiba ya kugombea uraisi kwa awamu yake ya pili, na akipita atakuwa raisi hadi mwaka 2035.

Kwa hiyo basi, Samia anaweza kuwa Mtanzania wa kwanza kuwa rais kwa muda wa miaka 14 kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Hiyo ni habari njema kwa Watanzania wengi, na habari mbaya kwa wengine, lakini ndio ukweli uliopo.
Katiba inasema nafasi yake kugombea urais ni moja tu baada ya kupokea kijiti full stop.

Hata, hiyo kesho unaijua ina rangi gani?

As we converse on the platform the majority are disarrayed
 
Hata mimi nashangaa kayatoa wapi haya maneno?

Manaake katiba unasema kabisa kama Makamu wa Rais atapata urais kwa sababu yoyote ile ya Rais kufa/kujiuzulu au kuacha kutokana na ugonjwa katoka kipindi kisichozidi miaka 3 ndo anaweza kugombea term 2 ila SSH amepata urais kwa miaka 4 kwahiyo anaruhusiwa kugombea mara moja tu(2025-2030) kwahiyo sana sana anaweza kufikisha miaka 9 tu si zaid ya hapo
shukran.

Tahadhari tu ni kutokea kwa janja kama ya Cote d'Ivoire ambapo wanachangamkia mabadiliko ya Katiba kama wapinzani wanavyopenda na baadaye kudai kuwa 2025-... itambuliwe kama awamu ya kwanza kwa Mama kwa mujibu wa katiba mpya. Yote yanawezekana katika nchi zetu hizi. Na yote yanategemea matakwa ya watakaokuwa wameshika mpini huko CCM.
 
Kwa mujibu wa katiba Samia Suluhu hawezi kugombea tena awamu 2 . Hivyo anaweza kuwa Rais kwa miaka 4 au 9 tu.
 
Duuhhh mkuuu umepitia katiba??

Kama makamo wa Rais, kawa Rais kukiwa kumebaki miaka zaidi ya mitatu

Basi ataruhusiwa kugombea mara moja tu
 
Back
Top Bottom