Kama Biblia ingeendelea kuandikwa; je, wewe na mimi tungeandikwa kwa sifa gani ndani ya Kanisa?

Shemasi Jimmy

Member
Apr 23, 2021
93
104
Gutenberg_Bible,_Lenox_Copy,_New_York_Public_Library,_2009._Pic_01.jpg
unnamed.png

KAMA BIBLIA INGEENDELEA KUANDIKWA, JE WEWE NA MIMI TUNGEANDIKWA KWA SIFA GANI NDANI YA KANISA?

Na Shemasi Jimmy 0659 611 252

Hallelluya watoto wa Mungu, tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa wema na ukuu wake katika maisha yetu. Pamoja na uovu wote tunaomtenda lakini amezidi kutupa nafasi ya kujikagua na kujitafakari kama nuru tulioipokea bado ipo ndani yetu, basi sifa na utukufu vimrudie yeye.

Imempendeza yeye leo tufanye tafakari ya kina juu ya Imani yetu huku tukijiuliza maswali kadha wa kadha kwa lengo la kuimarishana na kupeana moyo juu ya mapito yote katika maisha ya Imani yetu.

Ni swali ambalo Kila mmoja anapaswa kujiuliza ndani ya moyo wake.

Wafuatao ni mifano ya wakrito walioandikwa kwa Mema yao ndani ya kanisa na wale walioandika kwa maovu pia.

Akila na prisila- wakarimu na wakaribishaji kwa ndugu wa kiroho.(mdo 18:26)

Apolo mwenye kumuhubiri Yesu pasipo kupokea ubatizo sahihi(mdo 18:24-25).Je nawewe unamuhubiri kristo kama alivyokua apolo bila kupokea ubatizo sahihi wa Yesu? Je tungeandikwa kama Apolo?

Barnaba aliyekua mwaminifu kwa Bwana hata mauti ilipomkuta pasipo kutenda dhambi wala kumuwazia Mungu kwa ubaya.(ufu 2:10 fil 1:21)

Demetrio mtu mwema na mkaribishaji ndani ya kanisa, mwenye kushudiwa na kila mtu ndani ya kanisa kwa matendo yake mema(3Yoh 1:12).Je tungeandikwa kama Demetrio?

Deotrefe mwenye kupenda kua wa kwanza kwa kila jambo la kanisa, asiyependa wengine waingie kanisani, mwenye kuligeuza kanisa kua mali binasi na sio mali ya kristo yesu(3Yoh 1:9-10).Je tungeandikwa kama Deotrefe?

Epafrodito mwaminifu sana, yupo tayari kufa kwa ajili ya wakristo wenzie.(Fil 2:25-30). Je tungeandikwa kama Epafrodito?

Simioni mchawi mwenye kuingia katika kanisa la Bwana ili kutafta faida za kimwili na si za kiroho, yupo tayari kutumia mali na pesa ili kufanikisha adhima yake(mdo 8:19-20).

Je tungeandikwa kama wakristo wenye kupenda mapato ya aibu(1thim 3:3)?tungeandikwaje

Je tungeandikwa kama wakristo wenye kupenda miujiza na ishara kuliko neno la Mungu(2kor 5:7)? Tungeandikwaje

Je tungeandikwa kama wazinzi na wenye kuharibu ndoa za ndugu zetu ndani ya kanisa?tungeandikwaje?

Je tunageandikwa kama watu wavivu na tusiojitoa kwa ARI na MALI katika ujenzi wa mwili wa kristo?tungeandikwaje?

Je tungeandikwa kama viongozi wa kanisa wenye kupendelea watu wenye pesa na vyeo bila kuwajali WAHITAJI(yatima, wajane na masikini(Yakobo 2:2-9)tungeandikwaje ndugu?

Je tungeandikwa kama watu tunaotumia nyumba za ibada kwa ajili ya kufanya biashara binafsi za maji, keki, vitambaa n.k

Hata hivo sisi wakristo wa sasa ambao tumezaliwa katika roho na kuukuta ushuda wa Yesu kristo katika maandiko matakatifu, bado tunanafasi ya kuandikwa kwa mema, ama maovu katika kitabu kile kitakatifu(taz ufu 20:12 Muh 12:14)

Ndugu yangu katika bwana, bado kitambo kidogo tu tumlaki mtakatifu, baada ya kulisoma chapisho hili naomba kila mmoja ajihoji nafsi yake, Je wewe ungeandikwa kwa mazuri au mabaya ndani ya kanisa. Ikiwa ni kwa mazuri basi shika sana ulichonacho kwa maana shetani hufanya vita na watakatifu, dumu katika kusoma neno na kuomba kila wakati.

Ikiwa ungeandikwa kwa mabaya basi tambua Mungu ametupa tena nafasi nyingine ya kurekebisha matendo yetu ili tuendelee kuishi maisha matakatifu na yenye ushuhuda kwa Mungu. Kumbuka Mungu wetu ni Mungu mwenye kusamehe na kubariki hakuna limshindalo. Yeye ni mwenye nguvu na uweza, yeye ni alfa na omega ni yeye mwenye kutoa Baraka na saburi. Usiache kumtegema Mungu kwa kila jambo.

Ikiwa kama ungeandikwa kama Apolo ndugu yangu nafasi iko upande wako,amua sasa ubatizwe ubatizo sahihi kwa mujibu wa maandiko(Yoh 3:3-7, mdo 2:38). Nipigie kwa namba hiyo juu nasi tutakufikia popote ulipo ndani ya mipaka ya Tanzania.

Mungu awabariki nyote mliotumia muda wenu wa thamani kusoma chapisho hili, hujapoteza kitu mtoto wa MUNGU bali umejichotea Baraka na fanaka tele kwa kuutafta uso wa Bwana(Isaya 29-12-13).
 
Nahis
View attachment 2410394View attachment 2410395

Nahisi nashindwa kutambua ubatizo sahihi ni nini/upi.
Nnafanya vipi kuupata na uko wapi, na faida zake ni nini?

Kutokana na taarifa hapo juu, inaonekana kuna Ubatizo usio sahihi , kama upo ni upi huo ili tusipishane na ufalme wa mbinguni.
 
shalom ndugu! ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi, kama alivyotangulia kutuonesha Bwana wetu Yesu kristo pindi alipobatizwa na Yohana mbatizaji. hata hivyo asili ya neno lenyewe yaani ubatizo limetoka katika lugha ya kiyunani BABTIZO likimaanisha ''ZAMISHA''
 
Sidhani kama kuna ulazima wa kufuata yale yote ya agano la kale.

Kanisa la mitume liliongozwa na agano jipya na ndilo chimbuko la Ukristo wote.

Maadhimisho ya sikukuu za kiyahudi yaliyafanyiwa maboresho na kuingizwa katika ukristo.

Skukuu kama Pentecost, Pasaka n. k

Sasa sidhani kama kilakitu kinaulazima wa kubaki kama kilivo, na si lazima vitu viwe kama vilivyokuwa kwani dunia inabadilika kwa kasi.
Na mageuzi haya yametuletea mtafaruku mkubwa sana katika imani hzi.

I think Bible need updates♦️
 
Back
Top Bottom