#COVID19 Kaka yangu amefariki kwa ugonjwa wa CORONA

Kaka yangu kafariki jioni hii kwa covid 19 hospital ya Bugando Mwanza hakika ni majonzi makubwa sana.

Alifikishwa hapo kwa matatizo ya uchovu tu na kwenda kucheki na hakupelekwa na mtu alienda akiendesha gari yake mwenyewe ila badae walimpima na kukuta ana corona akawekwa pale toka juzi Leo kazidiwa mchana Leo na jioni amelala akiwa bado ajawekwa kwenye oxygen.

Hakika ni majonzi makubwa.

He was a really man ameacha watoto wadogo na mke very sad indeed.
Dah .... isije kuwa baada ya kuambiwa ana corona...akapata hofu....kinga ikashuka....msukumo wa damu ukavurugika...akafariki...... wazo tu 😷
 
Kwanini uhisi kuumwa ukapime Corona? Badala ya Malaria,Uti,Tb n.k ujue vitu vingine bhana Ni kujitia wasiwasi
 
Gharama za matibabu ya Corona ni kubwa sana ,my relative ametumia zaidi ya milioni 7 ICU akiwa kwenye oxygen support hospitali. Sisi makapuku tunaojifanya tunda tunaweza kumudu hizo gharama? Hiyo ni hospitali ya serikali sijui kuhusu private hospitals, tuchukue hatua na tupate chanjo ndugu zangu.
 
Utakufa kwa hofu zako mjinga!

Machinga wa Kariakoo, Makondakta, bodaboda wangekuwa wanapukutika kama wangekuwa na mihofu kama yenu.
Angalieni huyu takataka ..Kikikupata kijimdudu kile ukipona uje hapa kutupa ushuhuda.
 
Mimi nimempa mtu aliyepoteza kakake pole, wewe unanitukana. Mjinga hapo atakuwa ni mama yako. Na hasa babu yako ambaye amekwisha kufa. Mimi ni mzima.
Mnakufa kwa hofu zenu wajinga!

Machinga wa Kariakoo, Makondakta, bodaboda wangekuwa wanapukutika kama wangekuwa na mihofu kama yenu.
 
Mkuu, mimi nimepata hii kitu. Niliumwa homa kwa wiki nzima, siku ya 9 miguu ikaanza kuvimba moyo kwenda mbio na Kukosa nguvu, wife wangu ni daktar alipoona hivo akasema Twende hospital, kutoka nyumban mpaka Agha Khan mjini niliendesha mwenyewe gari. Nimefika pale Nipo na uchovu haswaaa na moyo kwenda mbio, kuchek SPO2 tayari ishashuka to 90%, pia breathing ipo ya fasta fasta . X-ray ikaonyesha mapafu yote yana pneumonia na pia CRP ipo juu. Nikalazwa na ikalazimu kuwekwa kwa Oxygen. Aisee nakuambia isikie Corona kwa watu, usiombe yakukute. Nawatizama sana wanaobeza chanjo na kuwasikitikia. Hakika hawajui walisemalo. And kwa taarifa tu, Nipo kwenye miaka ya 30’s sina sukari, pressure or any underlying disease but cha moto nilikipata. Over 7 days ndani ya Oxygen. Kwa hiyo nawashaur chukueni tahadhari Corona ipo na inaua sana na matibabu ni gharama sana.
God bless you.
Mkuu kama ilikufua vya kutosha itoshe kusema hivyo,lakini chanjo sio kinga ya kutopata corona.

Au huna taarifa kwamba hata waliochanja inawahusu bado??
 
Maskini labda angekaa nyumbani asingekufa. Akanywa dawa tulizoea..Hospital.hofu na kutengwa kunafanya wengi wafariki.
 
Mkuu kama ilikufua vya kutosha itoshe kusema hivyo,lakini chanjo sio kinga ya kutopata corona.

Au huna taarifa kwamba hata waliochanja inawahusu bado??
Mkuu chanjo ni Kinga tosha ya Corona. Kuhusu waliochanja na bado wakapata; Kiutaalamu kuna Kitu kinaitwa seroconversion, Hii ni kwa kiswahili tunaweza sema ni kiwango cha utengenezaji wa Antibody maalimu iliyokusudiwa katika mwili baada ya kupata chanjo husika. Kwa kiingereza “In immunology, seroconversion is the development of specific antibodies in the blood serum as a result of infection or immunization.”
sasa kama mwili wako uliseroconvert kwa 20% au 30% au 50% ndo unapata ugonjwa kirahisi. Kumbuka pia Hata unapomeza Dawa wakati mwingine hazikusaidii au zinakusaidia kwa kiwango kidogo kadiri ya mwili wako unavorespond kwenye Dawa husika.
Natumaini umenielewa mkuu.
 
Chanjo ndo huugui sio?
Matelimika lini?

IMG_20210729_151052_559.jpg


Huko tulishatoka muda mrefu.

Tulipo wapi chanjo na lini. Ugonjwa unapungua tunaweza kuhangaika na mliowauwa ndugu zetu kwa porojo zenu.
 
Back
Top Bottom