Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,010
Hiki ni kisa cha kweli:
kikundi cha majambazi kilivamia nyumba moja ambapo wanafunzi wa Chuo Kikuu kmoja nchini walikuwa wamepanga. Baada ya kuwapora vitu mbalimbali vikiwemo simu za mkononi, wakati wa kuondoka mazungumzo yalikuwa hivi:
"Samahani kaka jambazi" mmoja wa wanafunzi wa kike aliyekuwa bado amelala chini aliita kabla jambazi wa mwisho hajatokomea gizani
"Unataka nini wewe" aliuliza jambazi huku akimmulika kwa tochi
"Sasa nyinyi si mnata simu?" alisema mwanafunzi
"unayo nyingine?" aliuliza jambazi
"hapana sina nyingine" alijibu mwanafunzi huku ameinua kichwa chake kumuangalia yule jambazi
"sasa unataka nini?" kwa hasira aliuliza jambazi
"Kaka jambazi miye naomba unirushie line yangu, ila simu chukua" alilia yule dada.
Yule jambazi kwau ukarimu wake akafungua zile simu na kuchomoa sim cards na kuwarudishia wanafunzi. Wakatokomea.
Tangu siku ile majambazi wale wanajulikana kwa ukarimu wao.