Mahi Diha

paartey

Member
Jun 26, 2023
39
53
MAHI DIHA

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 01

MAWASILIANO: 0783642467

ANZA NAYO.........

"Unajua nini swaiba katika watu nimekutana nao halafu nikawazoea kuliko wote na kuwapenda kupitiliza basi ni wewe mwanamke wangu peke angu....."

Alizungumza kijana muhibu ambaye kwa wakati huo alikuwa amevalia sale za shule ya secondary, msichana swaiba alibaki akicheka kwa aibu na kuangalia chini tu hakuwa muongeaji alikuwa msikilizaji mzuri sana

"Kwanza ile siku tu umeletwa na baba yako pale shuleni nikasema mwanamke si ndo huyu sasa, ila lile jicho la baba yako wakati nakupokea zile ndoo na mifagio nikasema huyu baba atanimeza sio kwa huu mjicho "

Aliendelea kuongea kijana muhibu na swaiba aliendelea kucheka kwa aibu, muda huo nyuma yao walifatiwa na wanafunzi wengine na muhibu akuacha kuongea swaiba alinyanyua mkono wake na kumziba mdomo muhibu baada ya wanafunzi wenzao kupita ndipo akamuachia

"Ndo nini ulikuwa unataka kuniua au ??"

Aliuliza muhibu ikiwa ni sehemu ya kumtania

"We unaongeaga tu wala uangalii watu, unafikili wangesikia wale ingekuwaje ? Me naogopa ujue "

Alilalamika swaiba

"Unaogopa nini mke wangu mzuri "

"Halafu nimesema usiwe unaniita mke wangu, sema muhibu we mbishi sana baba yangu akija kujua atokuacha salama mimi nalindwa kila kona kaka zangu dada zangu wananiangalia kwa makini sana ukiangalia mimi ndo mtoto wa mwisho haya weeh endelea "

Aliongea swaiba na kuonesha kuchukia akatangulia mbele zaidi, muhibu hakuwa na budi Bali kuongeza mwendo ili aende sambamba na swaiba

"Kwahiyo umechukia ??"
Aliuliza muhibu baada tu ya kumfikia swaiba, lakini pia hakupatiwa jibu

"Swaiba umechukia mama ??" Muhibu hakukata tamaa aliendelea kuuliza mwisho swaiba alicheka tu

"Mahi " aliita muhibu

"Diha" aliitika swaiba uku akiwa ameachia tabasamu pana kabisa lililofanya dimpo zake za asili kuonekana

Walifika kwenye njia mbili zilizogawanyika na kila mtu aliingia kona yake.

SONGA NAYO.......

Niite swaiba binti wa mwisho kabisa kwenye familia ya watoto watano uku wanaume wakiwa watatu na wakike wawili. Maisha yetu yalikuwa ya kawaida Sana ambayo sio ya kitajiri wala masikini kaka zangu wawili walikuwa wameoa na walikuwa na Makazi yao. Dada yangu alikuwa akikaa nyumbani uku akiendelea na kazi zake kwani alikua ni mwalimu wa shule ya msingi, kaka yangu ambaye alianza kuzaliwa halafu nikafatia mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu huko dodoma hivyo hakuwa akikaa nyumbani.

Swaiba mimi ndio kwanza nimeanza kidato cha Tano nina mwezi mmoja na week 2 tu na tayali nimepata mchumba . Baba yangu ni mkali mno yaani sikuwai kuwa na mahusiano uko nyuma kabla haya ndio mahusiano yangu ya kwanza kabisa katika maisha yangu na najisikia amani kuwa na kijana huyu ambaye yeye nilimkuta akiwa kidato cha sita hapo shuleni.

Shule yetu ni shule ya mchanganyiko lakini pia ina day na boarding baba yangu alikataa kabisa mimi kuishi shuleni akiitaji kuniangalia na kunichunga kama ambavyo alifanya kwa ndugu zangu wote. Nyumbani kwetu analindwa mwanamke hadi mwanaume na ukitaka kuama nyumbani ujue umeoa au umeolewa la sivyo utazeekea hapo.

Basi baada ya kuachana na muhibu wangu nilitembea barabara nzima nikijichekea kama kiazi vile, kwa muda mfupi ambao nimeishi na muhibu nilianza kujiona kama namiliki kila kitu duniani, tulishapeana na majina ya utani aliniita Mahi nilimuita diha walahi nisiseme uongo huyu mkaka nimempenda sana.

Nilifika nyumbani nikiwa nimechoka sana na nina njaa ya kutosha kwanza kabisa nikaanzia jikoni ambapo nilikutana na mama akikosha vyombo ni wazi walikuwa wamemaliza kula Muda mfupi uliopita

"Shikamoo mama.." nilimsalimia

"Marahaba, mbona jikoni na nguo za shule na mabegi juu ??" Aliitika mama na kunitwanga swali hapohapo nilibaki nikishangaa na kujichekesha tu maana nilipanga nikachukue chakula niende nacho chumbani

"Jaaah nilikuwa nakutafuta nimekumisi " niliamua tu kudanganya maana ningemwambia kuwa nilifata chakula ningepigwa konzi

"Ebu kabadilishe nguo my friend umekaa kinjaa njaa tu na haunenepi " alinifokea mama ni wazi alishajua kuwa nilifata msosi ila me na kula ni ndugu nakula jamani halafu ukiangalia mwili wangu sasa ndo vichekesho .

Nilitoka jikoni nikiwa nimechoka na ile njaa ndo kabisa nilishika begi langu mkononi na kuanza kuliburuza ile nafika sebuleni mzee hamisi huyu hapa chapu nikanyanyua begi na kulibeba vizuri

"Shikamoo baba" nilimsalimia, lakini hakuniitika akawa ananiangalia tu akatoa na miwani yake na kuweka pembeni

"Umerudi na usafiri gani ??" Aliniuliza baba

"Bajaji baba " nilijibu

"Sogea hapa" alizungumza baba sikuwa na budi Bali kusogea alipokuwa amekaa, nilimfikia akanikabizi simu yake nilishtuka sana kujiona mimi nikiwa barabarani tena nilikuwa na muhibu na tulikuwa tumeshikana mikono

"Baba...." nilitaka kuanza kuelezea lakini baba alinyoosha mkono wake kunistopisha sikuwa na budi Bali kukaa kimya

"Kabadili nguo na uendelee na shughuli zako " aliongea baba niliondoka nikiwa na wasiwasi sana niligeuka nyuma kila muda kumuangalia baba ambaye hakuonesha kuwa na muda na mimi kabisa.

Siku iliyofuata nilijiandaa asubuhi na mapema kama kawaida niliwai shuleni nilifika na kuchanganyika na wanafunzi wenzangu lakini nilikuwa na mawazo sana juu ya baba maana hakuonesha kuchukia lakini hakunigombeza alikaa kimya tu na baba yangu namjua akiwa na hasira au ukimkosea mnamalizana hapohapo 🥹 ata sijui kapanga nini.

Muda wa saa nne ulikuwa ni muda wa breakfast nilitoka nje na kwenda kujinunulia chakula sikuwa nikila chakula cha shule hivyo nilikuwa nikinunua kwenye duka la shuleni

"Mahi....." aliniita muhibu akiwa nyuma yangu

Niligeuka chap nikamshika mkono na kumsogeza pembeni kabisa nilisahau Ata na change yenyewe

"Eeeh swaiba jamani ndo kuvutana gani uku ??" Aliuliza na kujitoa mikononi mwangu baada ya kuona kuwa namvuta sana

"Kimenuka " nilizungumza

"Sijakuelewa " alijibu muhibu

"Ujaelewa nini nawe nakuambia kimenuka jana sijui ni nani katupiga picha tukiwa tunarudi nyumbani na kumtumia baba " nilizungumza

"Ni baba yako mwenyewe " alijibu muhibu akiwa hana wasiwasi ata kidogo

"Niliona gari yake jana lakini nilijua tu nikikuambia kuwa nimeona gari ya baba yako ungeniacha pale na ungeondoka ukiwa umechanganyikiwa " aliendelea kunielezea

"We unasema kweli ??" Nilimuuliza muda huo nilikuwa sijui natakiwa kulia au kucheka maana daah

"Muhibu unaitwa ofisini " alikuja kijana ambaye alikuaa kidato cha tano kama mimi lakini tulikuwa comb tofauti nilimfahamu kwani nilimuona siku ya usajili

"Nakuja " alijibu muhibu kisha akaniaga na kuondoka

Nilibaki nikiwa nimeshikilia keki zangu na juice nikiwa sielewi cha kufanya mwisho wa siku muda wa break uliisha na tukaitajika kuingia tena darasani sikuwa na budi Bali kuingia darasani nikiwa na chakula changu.

"Mbona haukula au ndo ulikuwa na baba yako ofisini ??" Aliuliza shoga yangu ambaye pia nilimpata hapo hapo shuleni ambaye alikuwa akitwa meena.

Kwanza kitendo cha yeye kumtaja baba yangu kilishtua sana moyo wangu nilimgeukia vizuri na kumuuliza

"Umesema baba yangu ofisini ?"

"Si ndio nawe unataka kusema hujamuona au ?" Alinijibu meena na kuuliza swali hapo hapo

Sikutaka tena kusubili majibu yake haraka nikainuka na kukimbilia ofisini kabla sijaingia nilifika dirishani na kusikia mtu akichapwa viboko .

"Yaani kwanini uchukue pesa yake ya nauli na kumfanya mwenzio atembee ??" Ilikuwa ni sauti ya mwalimu wa kike ambayo sikujua ni nani lakini muda huo huo milisikia sauti ya muhibu akipiga kelele za vilio baada ya kiboko tukua mwilini mwake.

"Ndo ukome yaani nyie kidato cha sita mnaonea sana wenzenu, mmalize tu shule tupumue"

Roho iliniuma sana yaani ni wazi kuwa baba yangu alienda kubadilisha mada kwa walimu na kumfanya muhibu kuadhibiwa niliendelea kusimama pale nje mwisho niliondoka maana niliofia kama nitaonekana inaweza kuwa tatizo zaidi. Nilirudi darasani lakini sikuwa na amani nilibaki muda wote nikimuwazia muhibu wangu 🥹.

Muda wa kuondoka nyumbani uliwadia nilizunguka uku na uku kumtafuta muhimu lakini sikumuona. Sikukata tamaa nikaendelea kumtafuta kwenye mazingira ya shule lakini pia sikufua dafu nilijua kabisa kuwa ameniacha na amechukia baada ya kile ambacho amefanyiwa na baba yangu. Kwa unyonge nilishika njia na kusogelea geti la kutoka nje ya shule. Ile natoa tu mguu getini nilishtuka sana kuvutwa kwa nguvu sana lakini sikuanguka na hapo hapo nikapigwa busi Zito kabisa kwenye shavu langu nilituliza akili kwanza na kumuangalia vizuri hakuwa mwingine Bali ni Muhibu nyie huyu kaka akomi....

ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom