Hadithi: Mpangaji (1)

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
17,796
32,148
Chombezo : Mpangaji Sehemu Ya Kwanza (1)

15 Feb

IMEANDIKWA NA : FRANK MASAI

*****************

Naitwa Prince au Prince Mukuru kwa jina langu lote kwa ujumla. Baba yangu alikuwa ni mfanyakazi katika shirika la reli la Tanzania ila sasa hivi ni mfanya biashara za binafsi zinazo muingizia fedha kwa ajili ya kujikimu maisha yake binafsi,hiyo ni baada ya watoto wake nikiwemo mimi kila mmoja kuanza kujitegemea.

Baba yangu kwa uwezo wake aliweza kutupa elimu ya kutosha mimi na kaka zangu watatu ambao sasa hivi ni watu wakubwa tu! hapa nchini. Mimi binafsi, sasa hivi nafanya zangu biashara ya kusafirisha bidhaa ghafi za hapa nchini na kuzipeleka nje ya nchi. Nina watoto watano, wawili niliyowapata enzi za ujana wangu na watatu niliwapata baada ya kuoa.

Watoto hao wawili niliyowapata enzi za ujana wangu,ndio hasa sababu ya mimi kuhadithia mkasa huu ambao kiukweli unatakiwa kuufatilia ili upate mengi ya kujifunza.

Mnamo mwaka 2008,nilimaliza kidato cha nne katika shule ya Tabora Boys. Baada ya kumaliza shule,nilirudi zangu nyumbani Morogoro kwenye nyumba ya baba na kuanza maisha mengine kama raia wa kawaida. Nyumba ile ilikuwa kubwa sana, na ilionekana kubwa zaidi baada ya kaka zangu kuondoka na kwenda kuanza maisha ya kujitegemea. Kaka yangu wa kwanza alienda Arusha, wa pili akaenda Dar na wa tatu yeye alienda Dodoma,hiyo yote ni katika saka za maisha.

Shule niliyotoka yaani Tabora Boys, kwa kifupi ilikuwa haina wanawake. Wanawake tulikuwa tunaonana nao Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo tulijumuika nao pamoja katika ukumbi wa chuo cha Uhaziri kilichopo pale pale Tabora. Yaani namaanisha kuwa, kila ilipofika Ijumaa ya mwisho wa mwezi, zile shule zilizokuwa na jinsia moja pale Tabora ,zilikutana na kubadilishana mawazo huku wale wenye wapenzi wakienda mbali zaidi kwa kubadilisha na kukabidhiana viungo vyao vya mwili.

Mimi nilikuwa msanii tu! Yaani sina demu wala nini, tabia yangu ilikuwa ni kuchukua wasanii wenzangu wale wasiokuwa na wanaume. Kwa siku hiyo moja ya Ijumaa, niliweza “kugonga” watoto si chini ya wawili,kila mmoja kwa wakati wake. Tabia hiyo ilikomaa sana katika mwili wangu,kitu ambacho kilisababisha niwe kila wakati nataka “kula mizigo” . Hivyo pindi hamu ilipokuwa inanikamata sana,nilijifanya naugua ili wanitoe nje ya shule eidha kwa kunipeleka hospitali au kunipa rikizo ya muda mfupi. Kitendo cha wao kunipa nafasi hiyo, kilinifanya niwe natoroka mahala wanaponiacha na kwenda zangu sehemu zangu maalum kwa ajili ya kujichukulia “mizigo” ya “kugonga”, na pindi nilipokuwa nakosa sana mizigo hiyo, basi nilihamishia majeshi yangu kwa yeyote nitakaye kutana naye lakini wa jinsia ya kike.

Nakumbuka siku hiyo nilishikwa na hamu ya kufanya ule upuuzi kiasi kwamba nilishindwa hata kwenda darasani. Kitendo kile kilifanya yule msimamizi wa wanafunzi pale shuleni kuniona kama naumwa,hivyo aliniongoza hadi hospitali moja ya pale Tabora na nilipofika, ndipo nikajidai naumwa zaidi. Nilijiregeza kiasi kwamba nilishindwa hata kutembea,hivyo nikaletewa kile kiti cha wagonjwa wasiyojiweza ili kinisaidie kuingia hospitali. Baada ya kuniingiza mle, yule mwalimu akabaki nje kwa ajili ya kusubiri majibu yatakayotoka kwa yule aliyenipokea. Ile kufunga ule mlango niliyoingilia, nilinyanyuka haraka na kuanza kuongea na yule muuguzi aliyenipokea huku nikimshawishi kwa uongo mwingi ili asinidunge sindano zao,hasa diripu.

“Kaka, unataka hela hutaki?”. Nilinyanyuka na kumtupia swali yule jamaa aliyekuwa anahangaika kunisukuma na kile kiti cha wagonjwa. Kitendo cha mimi kunyanyuka vile ghafla,kilimfanya kidogo ashtuke na kuhisi kuwa nimechanganyikiwa.

“Wewe si unaumwa wewe? Au ndiyo Malaria inakupanda kichwani?.Aliuliza yule kaka.

“Tulia kaka, skonga kuna ukame sana. Hapa bila kuzuga naumwa basi kule skonga ningebaka wenzangu. We sema, unataka hela au hutaki”.Nilijitetea kidogo na kurudi kwenye mada yangu.

“We unataka ufanye nini? We mwenyewe kwanza ni mwanafunzi,halafu unaniulizia mfanya kazi kama nataka hela. Inakuwaje hiyo?”.Jamaa alikuwa mbishi kuelewa,ila nikamsawazisha.

“Sikiliza Bro, mimi hapa siumwi. Cha msingi, wewe nibandike bandike hayo madiripu halafu muite huyo ticha aje kuniona. Usimruhusu aende kwa daktari,kwani ukifanya hivyo utakosa hela”.Nilimwambia hayo huku nikimwangalia usoni nikisubiri jibu lake.

“Ehee, nakusikiliza dogo. Au ndo umemaliza?”.Yule muuguzi akauliza tena.

“Kwani Bro hujanielewa wapi? Mbona unakuwa na fuvu gumu?”.Nilimuuliza kwa jazba kidogo huku nasukuma kichwa chake kwa kidole cha shahada.

“Dogo sikiliza, hapa tunasaidiana. Mimi nikikuwekea hayo madiripu,nitapataje hiyo hela?”. Jamaa aliniuliza swali hilo.

“Kumbe tatizo ni hilo. Akija we zuga kuwa unanihurumia sana,halafu mwambie bei ya haya madiripu pamoja na hela ya msosi wangu nitakao kula nikiwa hapa. Usimruhusu aende kwa daktari mkuu, maliza hapa hapa. Mwambie wewe utapeleka taarifa zote ofisini”.Nilimaliza na yule muuguzi kwa tabasamu,akachukua maplasta na kuanza kubandika ile mirija mikononi mwangu bila ya zile sindano, wakati huo ilikuwa ni mida ya saa saba mchana.

“Sasa dogo, aking’ang’ania kwenda kufanya malipo ofisini je?”.Yule jamaa muuguzi aliniuliza baada ya kumaliza kunitundikia zile diripu uchwara.

“Lile ticha siyo janja, halijui lolote. Yaani pale skuli kazi yake kusimamia makazi tunayolala na siyo kufundisha. Halafu mimi nina kadi hii ya bima ya afya, hivyo wewe usiwe na wasi. Mimi matibabu yangu ni bure.

“Ha ha haa, hapo sawa nimekuelewa. Sasa ngoja niende kwa ticha lako”.Jamaa akawa anaondoka kwenda kumuita mwalimu yule niliyekuja naye.Baada kama ya nusu dakika,waliingia huku mimi nikiwa kama sijielewi pale kitandani.

“Ticha, aisee dogo anaumwa sana”.Nilimsikia jamaa akianza kuongea na ticha wangu.

“Kwa hiyo ni nini kinamsumbua?”.Akauliza ticha.

“Nimecheki mapigo yake ya moyo ndiyo yanaenda kasi sana,hivyo yaonekana ni BP. Ila usiwe na shaka sana. Wewe niachie elfu hamsini za matibabu pamoja na tupesa kidogo kwa ajili ya chakula cha mgonjwa akihamka. Siwezi kuendelea na matibabu bila kupata msaada wa kifedha ili tununue dawa zake na vitu vingine muhimu kama hizo diripu ambazo anatakiwa atundikiwe tatu”.Jamaa muuguzi alijielezea nia yake,na bila kipingamizi,yule ticha aliingiza mikono yake kwenye mfuko wa suruali na kuibuka na waleti iliyonona kiasi chake.

Wakati huo mimi nilikuwa namuangalia kwa jicho moja la kuiba, na nilishuhudia akitoa noti saba za elfu kumi na kumkabidhi yule jamaa.

“Sasa dokta, fanya harakati huyu mtoto apone. Mimi nitakuja kesho ili nijue ni nini kinaendelea, sawa dokta?Akihamka mpe salaam zangu”.Ticha alimalizana na yule jamaa muuguzi na kuanza kuondoka huku akisindikizwa na yule muuguzi ambaye kwa kumuangalia alikuwa ana ukame sana kifedha,hivyo zile hela kwake ilikuwa kama bahari kutokea jangwani.

“Dogo tumewin. Kweli ili ni bonge la boya. Sasa sikiliza, kanipa elfu sabini, wewe chukua hii thelathini halafu pitia huo mlango kafanye yako. Huu wa kuingilia mimi naufunga, we ukirudi pitia mlango huo huo halafu njoo ile ofisi yangu kunipa taarifa,iwe saa kumi na mbili, sawa?”.Yule jamaa muuguzi alinipa maelekezo ya nini cha kufanya baada ya kuhakikisha yule ticha katokomea kabisa pale hospitali. Nilimjibu kwa kuitikia poa huku nazitoa zile diripu na kuanza kutoka nje.

Niligundua kuwa yule jamaa alikuwa ni muuguzi wa zamu ambaye ana cheo kidogo,na katika hospitali ile,wanafunzi walikuwa wana sehemu zao maalum kwa ajili ya kulazwa na siku hiyo kulikuwa hakuna mwanfunzi aliyeletwa zaidi yangu.

Niliingia viwanjani na kuanza kutafuta mwanamke wa kutuliza maumivu yangu huku nikiwa na hamasa kubwa ya ujana wangu ambao sikufahamu kuwa ni maji ya moto.
 
Ahahahah
Nimeenda kuponea Kwa mganga wa Hadi akasema nilipiga jini subiani😂😂🙆 SEMA lilikua tamu sana😋😋😋
Akasema ningechelewa ningeanza kukojoa sembe😂😂
tungesafirisha mpanuyole iyooo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom