Kaka jambazi eeh!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Hiki ni kisa cha kweli:

kikundi cha majambazi kilivamia nyumba moja ambapo wanafunzi wa Chuo Kikuu kmoja nchini walikuwa wamepanga. Baada ya kuwapora vitu mbalimbali vikiwemo simu za mkononi, wakati wa kuondoka mazungumzo yalikuwa hivi:

"Samahani kaka jambazi" mmoja wa wanafunzi wa kike aliyekuwa bado amelala chini aliita kabla jambazi wa mwisho hajatokomea gizani

"Unataka nini wewe" aliuliza jambazi huku akimmulika kwa tochi

"Sasa nyinyi si mnata simu?" alisema mwanafunzi

"unayo nyingine?" aliuliza jambazi

"hapana sina nyingine" alijibu mwanafunzi huku ameinua kichwa chake kumuangalia yule jambazi

"sasa unataka nini?" kwa hasira aliuliza jambazi

"Kaka jambazi miye naomba unirushie line yangu, ila simu chukua" alilia yule dada.

Yule jambazi kwau ukarimu wake akafungua zile simu na kuchomoa sim cards na kuwarudishia wanafunzi. Wakatokomea.

Tangu siku ile majambazi wale wanajulikana kwa ukarimu wao.
 
Lazima watakuwa hapa bongo Dar maana ukarimu huo ni wa nadra sana.Lol
 
Kaka jambazi = ra and company, dada mwanafunzi = kaka mkubwa.
Ngoja niwape vijicent vya "kilmo hewa" msahau shida zenu, kwani
Nyie wanafunzi lichuo hili ni wasahaulifu sana. Mtasahu tu na kuutangaza
Ufalme wangu popote muendapo.

Respect mmj.
 
Ni kama yule ambaye alikimbia na hela za wananchi kwa ufisadi, lakini akatuachia uwaziri mkuu! Sasa hivi eti anaonekana ni mkarimu.
 
Mnasifia mtu aliye rape, ila kabla ya ku rape kaambiwa basi afadhali uvae ndomu, akavaa.

Mnamsifiiiiiia.

Mnaminimize ushenzi wa rape kwa sababu rapist alivaa condom?

Mi sijaelewa hili. Ni mentality hii hii inayotufanya tukubali uongozi mbovu eti kisa tuna "amani"

Watu wantuibia simu kwa ma EPA na ma Richmondi na kutuachia "line" ya amani, halafu tunawasifu majambazi wakarimu kweli, wametuibia simu lakini wametuachia line.

Hogwash bin Balderdash.
 
Kumbe ipo sathili nyingine ya "Kaka Jambazi" zaidi ya ile ya BWABWA?...Kweli hii inji chipoko!.Hatukawii kusahau matatizo kwa kuwa tumezaliwa na huruma kuliko "YESU MNAZARETI!"

Tulipoanza tu awamu ya Nne, kelele zilikuwa nyingi sana kuwa chama tawala kimetumia fedha nyingi za umma kwenye kampeni, tukapigwa na changa la macho la "MABILIONI YA JK" ambayo yalipelekea kwa wanyonge kwa staili ya aina yake, yakapelekea kuanzishwa kwa " SACCOS" hewa zenye mfumo tofauti na zile za kawaida za kiushirika, ambazo zilipelekea wajanja "KUKOPA KABLA YA KUWEKA na hatujui sasa kama wamerejesha na uhai wa SACOSS hizo upoje sasa . Wote tupo kimya, hakuna ajue hatima ya hizo fedha za umma zimeipatia jamii faida gani kwa kuwa zilitolewa kwa kivuli cha jina lililojema la Mheshimiwa mwenyewe.

Hatukuweza kuhoji DSA alizotumia mzee wa "RICHI MONDULI" na wapambe wake waliokwenda kutafuta "mvua ya kutengeneza" kule Thailand, na mvua yenyewe isionekane mapka kesho...

Hatujahoji ni vipi "tutafidiwa kwa fedha zilizopotea kwenye ulaghai wa wazi wa RICHMOND na DOWANS kupitia malipo ya gharama za uwezo wa genereta (Capacity charges) ambazo zimetoka na umeme haukuonekana? Tuliambiwa Serikali yetu inalishighulikia na hatima yake imefika kikomo, mjadala umefungwa sasa!....

BEA wamekubalui kurejesha chenji taslimu bila riba. Tumekubali na kuanza kujisifia "kwa hili tumefanikisha" fedha zitaenda kwenye miradi ya maendeleo (hatutaki tena rada wala zana za kijeshi).

Kagoda, MEREMETA na wenzake wamerejesha zile za EPA, tukasema ziende kwenye KILIMO na hapo hapo Mafedhuli wa EPA wakaja na aandiko la Kimradi kwa jina la "KILIMO KWANZA" kwa kivuli cha "MAPINDUZI YA KIJANI (Green Revolution) ambao unahitaji mabilioni ya shilingi ambazo haziwezi kumfikia mkulima zaidi ya hao wabwenyenye!...
 
Ndio majambazi wakarimu ni afadhali kuliko jambazi asiye na huruma. Sisi ni wa mepesi mepesi!!!!!!

Kaka jambazi hakutaka kumtoa uhai dada yule zaidi ya kukwibaa simu na vingine.

Hata viongozi tulionao wanatuibia fedha na rasilimali zetu ila bado wanatujali kwenye chaguzi na kutuaminisha kuwa umoja na amani ya kitaifa wanaisimamia..Kumbuka 1995wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na vuguvugu la Mrema tulionyeshwa picha za mauji ya Rwanda ni kutokana na kuchagua upinzanii...TULIOGOFYA SANA...na tuliwaaminii..

Hata leo maandamano bado ni sumu kwani Polisi wakitokea tuu na mabomu, marungu na maji ya kuwashwaaa tunatawanyikaa kabla hata hawajavitumiaa..

Ndio sisi ni kisiwa cha amani ila sijui ni msingi wa Mwalimu Kama historia inavyotuaminisha kwenye maandiko au ni hulka ya asili ya Watanzania????

Kaka jambazi jamaniii bora yeye kuliko jambazi muuaji.
 
Hii Mwanakijiji Ilitokea SAUT Chuo Kikuu Mwanza..Maeneo ya kijiweni...Umeispot kiukweli.Eneo hilo linakuwaga maarufu sana wakati boom likitoka wanafunzi huwa na matanuzi kwenda mbele na kununua vitu vya thamani sasa hapo ndio uvamizi unaanza.Kwa Kumalizia mwingine alimwambia kaka jambazi amwachie simu boom likitoka aijie chake..kama shida ni mapato.
Regards
Buswelu
 
Alichofanya ni kuwakumbusha manake sim cards kimsingi haziwasaidii majambazi baada ya kuiba
handsets
 
Hii Mwanakijiji Ilitokea SAUT Chuo Kikuu Mwanza..Maeneo ya kijiweni...Umeispot kiukweli.Eneo hilo linakuwaga maarufu sana wakati boom likitoka wanafunzi huwa na matanuzi kwenda mbele na kununua vitu vya thamani sasa hapo ndio uvamizi unaanza.Kwa Kumalizia mwingine alimwambia kaka jambazi amwachie simu boom likitoka aijie chake..kama shida ni mapato.
Regards
Buswelu


buswelu.. its true.. ni SAUT
 
Hao majambazi watakuwa wapya katika hii field,sio wale wa kutoka nyanda za juu kusini au mikoa ya kanda ya kaskazini,maana wao kila kitu deal,hata hizo line wangekomba tuu!!
 
Huu ndo wizi wa kibongo... tunaibiwa ila tunawasifia kwa kurudisha laini na tunawaita kaka... mafisadi,wezi jambazi.....SIKUBALI KUWAITA HAWA MAKAKA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom