Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka

Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka

Je hawa wa ndani wanaofunga viwanda vyao na kukimbilia nje sababu ni nini Mh. Waziri?
 
Kama tunaitakia mema nchi yetu, mtazamo wetu wa wafanya biashara wa ndani na wawekezaji wa kutoka nje ya nchi na wazawa lazima ubadilike.
Hii ya kufikiria wafanya biashara ni watu wezi inatoka wapi? Hivi kuna watu wanaodhulumu kama watu wenye ofisi za huduma kwa umma? Kila kitu kinaonekana kama ni favor kutoka kwao
 
Tuwe wakweli jamani,bado tatizo la rushwa na ukiritimba kwa nia ya ku-solicit rushwa lipo kwa watumishi wa umma.Lipo pia tatizo la kuikwamisha serikali ya awamu ya tano kwa makusudi.Anayekataa kwamba matatizo haya hayapo ni part of the problem.
Tunaambiwa kila siku nidhamu ya watumishi iko juu, hayo yanatoka wapi?
 
Kuna double standards nyingi kwenye namna wanavyowasimamia wafanyabiashara na uelewa wa biashara zenyewe.
Huku TRA ndio balaa....kwenye mabaraza wanasema mfanya biashara asifungiwe biashara....kwenye mikoa wanafunga accoubt za wafanya biashara tena kwa ubabe tu. Najiuliza, kuna mamlaka ngapi zinazoendesha mambo Tanzania? Kufunga account si ndio kufunga biashara na kuchochea njia za mkato za kufanya biashara?
Tanzania, ukishaajiriwa na serikali ina maana hakuna kujari lolote linaloendelea?

Huko ndo kumeoza kabisa,hata investors wanakiri kodi si rafiki kulingana Na nchi zingine.
 
Ukimruhusu mwekezaji awekeze nchini kwa kutolipa capital goods tax na corporate tax kwa miaka kumi ni bora zaidi kuliko kutokuwa na huo uwekezaji let say anawekeza kwenye kiwanda kitakacho zalisha ajira za watu 1000.

Mwekezaji huyo atanunua umeme, atanunua maji, atanunua mafuta ya magari, atanunua consumables mbalimbali na vitu vyote hivyo vitasaidia mzunguko wa pesa sokoni. Kingine nikuwa wafanyakazi watakao ajiriwa watalipa kodi ya PAYE na pia watakuwa na pesa(income) ya kununua mahitaji yao mbalimbali na kwa hiyo kushamirisha biashara za watu wengine kama za vyakula, mavazi, nyumba za kupanga, watalipa bills za umeme na maji, watapeleka watoto shule, hospitali nk.

Kwa ufupi serikali inatakiwa kutazama vikwazo vya uwekezaji ili kuongeza wawekezaji na kupanua uchumi badala ya kuweka vikwazo vingi ambavyo havitusaidii sana kukuza uchumi wetu.

ulosema ni kweli tu mkuu.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amesema vitendo vya rushwa, urasimu uliokithiri na vinavyoendana na hivyo kwa watumishi wa umma ni chanzo cha kufukuza wafanyabiashara na wawekezaji nchini
Amesema hali hiyo inasababisha kushindwa kufikia lengo la Taifa la ukuaji wa kibiashara.

Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifunga kongamano la kibiashara la nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika lililofanyika kwa siku tatu mjini hapa.

Alisema watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, kwa ufanisi na kuondoa urasimu usio wa lazima ili kuvutiwa wawekezaji.

Kairuki alisema hata kama Serikali ikitumia nguvu kubwa katika kutangaza wafanyabiashara na wawekezaji kuja kuwekeza nchini, kama vitendo hivyo visipokomeshwa watumishi wa namna hiyo wataendelea kuwakimbiza.

Alisema kila mtumishi wa umma anatakiwa ajitathmini katika utendaji wake kwani vitendo hivyo vikiendekezwa vitasababisha wawekezaji kwenda kuwekeza nchi nyingine.

Alisema Serikali itaendelea kupunguza changamoto ya tozo kwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kuboresha biashara.
Naye mkuu wa mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga alisema Serikali haitawavumilia watumishi wa umma mkoani humo watakaokwamisha shughuli za kibiashara kwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Rais wa chama cha wafanyabiashara kutoka Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Ndakala Emmanuel alisema mkutano huo uliomalizika usiwe bure, bali Serikali ya Tanzania ifanyie kazi mambo yote yaliyojadiliwa ili kila mmoja aweze kunufaika na makubalianao hayo.

“Kama tusipopata matokeo mazuri ya kikao hiki itakuwa tumekaa bure hapa na kupoteza muda, ila kama mapendekezo yatafanyiwa kazi tutapata mafanikio katika biashara zetu,” alisema.

Hilo ni kongamano la kwanza kufanyika mkoani Kigoma, ambapo baadhi ya mikoa iliyofanya makongamano kama hayo yanayolenga kuvutia uwekezaji ni pamoja Mwanza, Arusha, Lindi na Tabora.

Waziri amekuwa muazi na huu ni ukweli mtupu. Katika hili hatuhitaji siasa kama tunataka nchi yetu isonge mbele. Binafsi nakupongeza Waziri Kairuki. Personally nimekutana na Changamoto nyingi ndani ya TIC na Wizara ya Ardhi. Big up and keep it up hakika Mungu atakusimamia.
 
Watumishi walikiwepo tangu enzi na enzi... Mpya hapa ni huyu jiwe.... Sababu kibwa ni yeye wala si vingine.. huko kwingine tutatafuta MCHAWI tu
Tumia lugha ya kistarabu utaeleweka - sema udhaifu wake uko wapi kama taasisi na toa mapendekezo
 
Kama Masha tu wa fasjet alipigwa figisu figisu nani wa nje atachezea upatu fedha zake.Kwa Manji Pugu pana tia hadi huruma panaota majani sababu ya alichofanyiwa na makolomije nani wa nje atathubutu.Watu wamehamisha biashara zao nje kuepuka kuishi kishetani.Usitafute mchawi,msitupie lawama Watumishi, kauli Na matendo yenu ndivo ukimbiza wawekezaji. Ngoja awamu hii ipigwe chini mkae kando muone watakavorudi Kwa kasi.
 
Tumia lugha ya kistarabu utaeleweka - sema udhaifu wake uko wapi kama taasisi na toa mapendekezo
.Kama wazawa tu tena weusi wanalala mbele wanavuka nchi Jirani hao wawekezaji ni nani.Wanakimbia Sera za kijamaa kwenye ulimwengu wa kisasa
 
Ningekuwa na mamlaka ningetoa Tax holiday ya 10 years kwa mwekezaji kutoka nje akija hapa. Ningependekeza bunge lipitishe sheria za kuwalinda zenye kifungu cha kutobadilika kila baada ya 10years. Kwanini?

Tusitoke sana nje' hapa hapa ndani tujiulize, mikoa yetu ambayo angalau kibiashara ipo vizuri, waliowezesha hizi biashara ni wenyeji? Utagundua kuwa mikoa ambayo haina watu kutoka maeneo mengine kuja kufanya biashara bado ipo nyuma kimaendeleo. Ujamaa tuutumie kwenye mgawanyo wa mapato ya serikali Ila kwenye uwekezaji na biashara tuache market forces zifanye kazi na ss tuwe na Sera na sheria endelevu zinazowalinda wafanyabiashara.

30% pamoja na ukubwa wake bado kuna PAYE, SDL, WCF etc ambazo ni vipato vya serikali. Halafu waajiriwa wengi watakuwa na kipato wataongeza consumption na indirect tax itaongezeka sana. Kisiasa itakuwa na manufaa kwani ntakuwa nimepunguza tatizo la ajira.

Upinzani nao umekuwa ukifanya makosa sijui ni bila kujua au ndio tafsiri ya neno upinzani. Awamu iliyopita walipiga kelele kuhusu Tax holidays za makampuni na namna wanavyoacha kulipa kodi kwa kubadili majina, walitaka sheria iwabane walipe kodi yote. Sasa hivi wanasema tena sheria za kodi zinakimbiza wawekezaji. Hii nchi tunawahitaji sana wapinzani kuweka mambo sawa tafadhalini kabla ya kupigania jambo Utlist mjue matokeo yake endapo litatekelezwa. Sio mambo ya tunataka raisi atulie nyumbani ajenge nchi halafu anapatikana mnatuonyesha tena madhara ya kutokutoka nje na kupiga kelele. Piganieni mambo baada ya kuyachuja na kufahamu matokeo yake kama mtasikilizwa.
 
.Kama wazawa tu tena weusi wanalala mbele wanavuka nchi Jirani hao wawekezaji ni nani.Wanakimbia Sera za kijamaa kwenye ulimwengu wa kisasa

Ni mwekezaji yupi na yupi aliyelala mbele
 
Tumia lugha ya kistarabu utaeleweka - sema udhaifu wake uko wapi kama taasisi na toa mapendekezo
Lugha gani mbaya nimeotumia hapo? Unajuwa kama hupendi point ya mtu mkosoe kwa hoja....
Alishasema hapangiwi, hajaribiwi.... Nenda deep na hayo maneno utaelewa tu...
Huyu wetu anaogopwa SANA kiasi kwamba hakina anayethubutu kushauri tofauui na anavyotaka yeye... Na watu wakishafiata anayoyataka na yakabuma watalaumiwa watekerezaji... Kumbuka TRA walilaimiwa pia
 
Ningekuwa na mamlaka ningetoa Tax holiday ya 10 years kwa mwekezaji kutoka nje akija hapa. Ningependekeza bunge lipitishe sheria za kuwalinda zenye kifungu cha kutobadilika kila baada ya 10years. Kwanini?

Tusitoke sana nje' hapa hapa ndani tujiulize, mikoa yetu ambayo angalau kibiashara ipo vizuri, waliowezesha hizi biashara ni wenyeji? Utagundua kuwa mikoa ambayo haina watu kutoka maeneo mengine kuja kufanya biashara bado ipo nyuma kimaendeleo. Ujamaa tuutumie kwenye mgawanyo wa mapato ya serikali Ila kwenye uwekezaji na biashara tuache market forces zifanye kazi na ss tuwe na Sera na sheria endelevu zinazowalinda wafanyabiashara.

30% pamoja na ukubwa wake bado kuna PAYE, SDL, WCF etc ambazo ni vipato vya serikali. Halafu waajiriwa wengi watakuwa na kipato wataongeza consumption na indirect tax itaongezeka sana. Kisiasa itakuwa na manufaa kwani ntakuwa nimepunguza tatizo la ajira.

Upinzani nao umekuwa ukifanya makosa sijui ni bila kujua au ndio tafsiri ya neno upinzani. Awamu iliyopita walipiga kelele kuhusu Tax holidays za makampuni na namna wanavyoacha kulipa kodi kwa kubadili majina, walitaka sheria iwabane walipe kodi yote. Sasa hivi wanasema tena sheria za kodi zinakimbiza wawekezaji. Hii nchi tunawahitaji sana wapinzani kuweka mambo sawa tafadhalini kabla ya kupigania jambo Utlist mjue matokeo yake endapo litatekelezwa. Sio mambo ya tunataka raisi atulie nyumbani ajenge nchi halafu anapatikana mnatuonyesha tena madhara ya kutokutoka nje na kupiga kelele. Piganieni mambo baada ya kuyachuja na kufahamu matokeo yake kama mtasikilizwa.

Ngoja tulimie meno kwanza hayo achia awamu ijayo
 
Lugha gani mbaya nimeotumia hapo? Unajuwa kama hupendi point ya mtu mkosoe kwa hoja....Alishasema hapangiwi, hajaribiwi.... Nenda deep na hayo maneno utaelewa tu...Huyu wetu anaogopwa SANA kiasi kwamba hakina anayethubutu kushauri tofauui na anavyotaka yeye... Na watu wakishafiata anayoyataka na yakabuma watalaumiwa watekerezaji... Kumbuka TRA walilaimiwa pia

Pole kwa kutotunza kumbukumbu - sehemu fulani uliandika neno JIWE, ndiyo nikakuomba kutumia maneno yasiyokuwa na ukakasi
 
Pole kwa kutotunza kumbukumbu - sehemu fulani uliandika neno JIWE, ndiyo nikakuomba kutumia maneno yasiyokuwa na ukakasi
Kama umekwazika na neno hilo nisamehe bure. Angalia tu hoja zingine hapo kwenye hilo neno weka jingine
 
Back
Top Bottom