Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka

Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka

Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka
Sunday May 12 2019

pic+kairuki.jpg

By Happiness Tesha, Mwananchi htesha@mwananchi.co.tz
Kigoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amesema vitendo vya rushwa, urasimu uliokithiri na vinavyoendana na hivyo kwa watumishi wa umma ni chanzo cha kufukuza wafanyabiashara na wawekezaji nchini
Amesema hali hiyo inasababisha kushindwa kufikia lengo la Taifa la ukuaji wa kibiashara.
Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifunga kongamano la kibiashara la nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika lililofanyika kwa siku tatu mjini hapa.

Alisema watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, kwa ufanisi na kuondoa urasimu usio wa lazima ili kuvutiwa wawekezaji.

Kairuki alisema hata kama Serikali ikitumia nguvu kubwa katika kutangaza wafanyabiashara na wawekezaji kuja kuwekeza nchini, kama vitendo hivyo visipokomeshwa watumishi wa namna hiyo wataendelea kuwakimbiza.

Alisema kila mtumishi wa umma anatakiwa ajitathmini katika utendaji wake kwani vitendo hivyo vikiendekezwa vitasababisha wawekezaji kwenda kuwekeza nchi nyingine.

Alisema Serikali itaendelea kupunguza changamoto ya tozo kwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kuboresha biashara.
Naye mkuu wa mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga alisema Serikali haitawavumilia watumishi wa umma mkoani humo watakaokwamisha shughuli za kibiashara kwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Rais wa chama cha wafanyabiashara kutoka Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Ndakala Emmanuel alisema mkutano huo uliomalizika usiwe bure, bali Serikali ya Tanzania ifanyie kazi mambo yote yaliyojadiliwa ili kila mmoja aweze kunufaika na makubalianao hayo.
“Kama tusipopata matokeo mazuri ya kikao hiki itakuwa tumekaa bure hapa na kupoteza muda, ila kama mapendekezo yatafanyiwa kazi tutapata mafanikio katika biashara zetu,” alisema.

Hilo ni kongamano la kwanza kufanyika mkoani Kigoma, ambapo baadhi ya mikoa iliyofanya makongamano kama hayo yanayolenga kuvutia uwekezaji ni pamoja Mwanza, Arusha, Lindi na Tabora.

Pia amesahau kuhusu Tanzania kujitoa kwenye mahakama za kibiashara kimataifa. Mwekezaji makini hawezi kwenda kuichezea kamari pesa yake, hasa kwenye nchi ya dunia ya tatu bila ya vyombo vya kimataifa kujihusisha.
 
Kama haya maneno ni kweli yameongelewa na Waziri mwenye dhamana,kwa kweli kazi tunayo.

Mtumishi wa Umma ana mamlaka gani ya kumzuia mwekezaji na yeye si mwamuzi zaidi ya Wizara husika kupitia Waziri mwenye dhamana?

Viongozi wanawalalamikia watumishi,watumishi nao wanawalalamikia viongozi,kipi ni kipi sasa??
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Rushwa ipo inalelewa na Serikali kutoa rushwa kwa Wabunge ccm ili kupitisha miswaada ya kuminya demokrasi nchini pia rushwa ya kununua wabunge na madiwani wa upinzani. Pia usisahau rushwa ndani ya TRA pia kuwabambikia wawekezaji/wafanyabiashara kodi kubwa kuliko inavyostahili ma kusababisha baadhi kuamua kuhama nchi au kufunga biashara zao maamuzi ambayo yanalikosesha Taifa kodi ya mapato.

Tuwe wakweli jamani,bado tatizo la rushwa na ukiritimba kwa nia ya ku-solicit rushwa lipo kwa watumishi wa umma.Lipo pia tatizo la kuikwamisha serikali ya awamu ya tano kwa makusudi.Anayekataa kwamba matatizo haya hayapo ni part of the problem.
 
Hiv muwekezaji gani atakubali kufungua biashara kwenye mazingira mabovu namna hii unafungua leo biashara kesho mwana siasa anakuja kukupa hasara kwa matamko yakijinga tu mfano maduka ya forex mnajua hali zao sasa hivi zilivyombaya
 
Ukimruhusu mwekezaji awekeze nchini kwa kutolipa capital goods tax na corporate tax kwa miaka kumi ni bora zaidi kuliko kutokuwa na huo uwekezaji let say anawekeza kwenye kiwanda kitakacho zalisha ajira za watu 1000.

Mwekezaji huyo atanunua umeme, atanunua maji, atanunua mafuta ya magari, atanunua consumables mbalimbali na vitu vyote hivyo vitasaidia mzunguko wa pesa sokoni. Kingine nikuwa wafanyakazi watakao ajiriwa watalipa kodi ya PAYE na pia watakuwa na pesa(income) ya kununua mahitaji yao mbalimbali na kwa hiyo kushamirisha biashara za watu wengine kama za vyakula, mavazi, nyumba za kupanga, watalipa bills za umeme na maji, watapeleka watoto shule, hospitali nk.

Kwa ufupi serikali inatakiwa kutazama vikwazo vya uwekezaji ili kuongeza wawekezaji na kupanua uchumi badala ya kuweka vikwazo vingi ambavyo havitusaidii sana kukuza uchumi wetu.
Ukimsikiliza Mwambe wa TIC utamhurumia. Jiwe na sera na sheria zake ndio tatizo. Jana wamepokea Wachina zaidi ya 300 kama tour Operators na agencies za utalii. Kama mazingira ya uwekezaji siyo rafiki ni bure kabisa.
 
Rushwa ipo inalelewa na Serikali kutoa rushwa kwa Wabunge ccm ili kupitisha miswaada ya kuminya demokrasi nchini pia rushwa ya kununua wabunge na madiwani wa upinzani. Pia usisahau rushwa ndani ya TRA pia kuwabambikia wawekezaji/wafanyabiashara kodi kubwa kuliko inavyostahili ma kusababisha baadhi kuamua kuhama nchi au kufunga biashara zao maamuzi ambayo yanalikosesha Taifa kodi ya mapato.

Mkuu baadhi ya viongozi wetu ni watupu mno vichwani,hayo yote uliyoyaainisha hawayaoni,wanajifanya wao ni wasafi,hawataki kuwajibika kwa ujinga wao wanataka kuwasingizia upuuzi watumishi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tuwe wakweli jamani,bado tatizo la rushwa na ukiritimba kwa nia ya ku-solicit rushwa lipo kwa watumishi wa umma.Lipo pia tatizo la kuikwamisha serikali ya awamu ya tano kwa makusudi.Anayekataa kwamba matatizo haya hayapo ni part of the problem.
Ndiyo vipo toka zamani, sasa hivi kuna taratibu zisizo tabirika. Una amka leo unakuta matamko kadhaa, mara marufuku kufanya kile,..............vitu halali vina haramishwa within no time.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mtumishi mwaminifu si yupo, Makondakta wa mabasi ya Daresalama.
Wamtumie huyo kukirimu Wawekezaji.
Maana ni ndiye mtumishi peke yake anayejisifia hadharani kuwa anamaisha mazuri katika awamu hii.
Wengine subirini hadi miundombinu itakapo kamilika kujengwa nchi nzima.
Watakao staafu mapema basi waridhike na watakacho ambulia kwenye mafao yao.
 
Uozo unaanzia bandarini, ukitua na mzigo, imetokea mtu katuama mashine zake ndani ya kontena kwa sababu ya upakiaji na usalama wa vyombo mtumaji akaamua kufungua baadhi ya vitu katika hizo mashine vitu kama feni, selfu na exzozi nakuviweka pembeni watumishi wa bandarini au mkaguzi anakwambia hivi vitu hujavitia kwenye listi lazima ulipie na anajifanya haelewi anatumia ubabe ili apate kula, afu mzigo unashushwa wote na kuvuruga upangaji na kusababisha hasara ya uharibifu na uvunjaji wa mizigo kwa zile careless zao bandarini mambo ambayo ni unnecessary kabisa. namna hii watu wataacha kukata tamaa?.
 
Watatafuta visingizio vingi ila hawatokubali kua tatizo ni lao, sa hivi Tanzania sio sehemu nzuri ya kuinvest hata kidogo, investing money bongo ni kupoteza hela tu, serikali inasumbua sana investors conditions zimekua nyingi mno nyingine ambazo ni unnecessary.
Una Ushahidi wa investor aliyesumbuliwa?
 
Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka
Sunday May 12 2019

pic+kairuki.jpg

By Happiness Tesha, Mwananchi htesha@mwananchi.co.tz
Kigoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amesema vitendo vya rushwa, urasimu uliokithiri na vinavyoendana na hivyo kwa watumishi wa umma ni chanzo cha kufukuza wafanyabiashara na wawekezaji nchini
Amesema hali hiyo inasababisha kushindwa kufikia lengo la Taifa la ukuaji wa kibiashara.
Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifunga kongamano la kibiashara la nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika lililofanyika kwa siku tatu mjini hapa.

Alisema watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, kwa ufanisi na kuondoa urasimu usio wa lazima ili kuvutiwa wawekezaji.

Kairuki alisema hata kama Serikali ikitumia nguvu kubwa katika kutangaza wafanyabiashara na wawekezaji kuja kuwekeza nchini, kama vitendo hivyo visipokomeshwa watumishi wa namna hiyo wataendelea kuwakimbiza.

Alisema kila mtumishi wa umma anatakiwa ajitathmini katika utendaji wake kwani vitendo hivyo vikiendekezwa vitasababisha wawekezaji kwenda kuwekeza nchi nyingine.

Alisema Serikali itaendelea kupunguza changamoto ya tozo kwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kuboresha biashara.
Naye mkuu wa mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga alisema Serikali haitawavumilia watumishi wa umma mkoani humo watakaokwamisha shughuli za kibiashara kwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Rais wa chama cha wafanyabiashara kutoka Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Ndakala Emmanuel alisema mkutano huo uliomalizika usiwe bure, bali Serikali ya Tanzania ifanyie kazi mambo yote yaliyojadiliwa ili kila mmoja aweze kunufaika na makubalianao hayo.
“Kama tusipopata matokeo mazuri ya kikao hiki itakuwa tumekaa bure hapa na kupoteza muda, ila kama mapendekezo yatafanyiwa kazi tutapata mafanikio katika biashara zetu,” alisema.

Hilo ni kongamano la kwanza kufanyika mkoani Kigoma, ambapo baadhi ya mikoa iliyofanya makongamano kama hayo yanayolenga kuvutia uwekezaji ni pamoja Mwanza, Arusha, Lindi na Tabora.
Waziri anaongelea nadharia, sisi tuliopo kwenye uwekezaji, tunaongelea uhalisia.

Aliyoyasema ni baadhi ya sababu, lakini kwa sasa sababu kuu ni vitendo/amri za viongozi na uvunjwaji wa sheria unaofanywa na viongozi, hasa:

1) Wakuu wa mikoa
2) Wakuu wa Wilaya
3) Mawaziri
4) Rais

Sababu nyingine ni uwingi wa kodi na ukubwa wa kodi.

Hakuna mwekezaji anayeweza kwenda kuwekeza mahali ambapo hakuna utawala wa sheria. Kwa mfano, kwenye madini, Sheria inasema, mtu pekee mwenye mamlaka ya kusimamisha shughuli za uchimbaji madini ni Tume ya Madini lakini sasa hivi, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, waziri na Rais, wote, wanaweza kusimamisha, na mara nyingi bila sababu za msingi. Hawajali huyo mwekezaji ana wafanyakazi, anatakiwa kulipa mikopo, bill za umeme, kodi mbalimbali, n.k.

Mazingira ya uwekezaji kwa sasa ni mabaya sana kwa sababu kila kiongozi anaweza kuingilia uwekezaji wako hata kama hana mamlaka kisheria.
 
Tuwe wakweli jamani,bado tatizo la rushwa na ukiritimba kwa nia ya ku-solicit rushwa lipo kwa watumishi wa umma.Lipo pia tatizo la kuikwamisha serikali ya awamu ya tano kwa makusudi.Anayekataa kwamba matatizo haya hayapo ni part of the problem.

Kinachonishangaza ni kwamba kinachoongewa nankinachoendelea ni vitu viwili tofauti. Rushwa ndio sababu kubwa ya wafanyakazi wa baadhi ya mamlaka za umma kuleta ukiritimba katika kazi zao. Mamlaka za kodi kuna watu wala hawaogopi kuomba rushwa ili "wakupunguzie" madeni yako au hela unazotakiwa kulipa. Rushwa bado ipo sana. Mpaka ije kupungua, inatakiwa nguvu ya ziada
 
Kwa kiasi kikubwa katika utawala huu, vitendo vya rushwa na urasimu vimepungua. Urasimu na rushwa uliokuwepo katika Awamu iliyopita ulikua mkubwa sana lakini bado wawekezaji walikuwepo wengi, mishahara ilikua ikiongezeka na ajira kibao.

Mh. Waziri jaribu kuupitia tena huo utafiti ulioletewa.
Kwemdimu, kakwambia nani rushwa imepungua
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huu ni kwa upande wa watumishi, je kwa upande wa serikali je?
Tuwe wakweli jamani,bado tatizo la rushwa na ukiritimba kwa nia ya ku-solicit rushwa lipo kwa watumishi wa umma.Lipo pia tatizo la kuikwamisha serikali ya awamu ya tano kwa makusudi.Anayekataa kwamba matatizo haya hayapo ni part of the problem.
 
Pia tunajua tunahitaji pembejeo, trecta, irrigation equipment, dawa, mbolea, elimu ya kilimo kwa wakulima.

Hivi vitu tunaweza kuviruhusu kwa zero tax.

Serikali inaweza kuwapa tax holiday for 10 years plus guarantee to buy 1000 trecta kila mwaka.

Haya matrekta yatasaidia kulima, kutoa mazao ya wakulima shamba ambapo barabara hazipitiki
kuyaleta mjini.

Baada ya miaka mitano unawauzia wakulima haya matrekta.
Ndugu kiukweli hapo ndipo kama nchi ingeweza kupiga hatua kubwa sana.just imagine solo LA mahindi liko wazi lakini Kwa akili za kijinga wanazuia yasitoke yanaozea Kwa mkulima.wakati wangeyaruhusu mkulima angepata fedha nyingi na msimu unaofuata angepanua mashamba kuongeza mavuno na hapo kama serikali kweli inapenda maebdeleo wangesaidia sana kwenye nyenzo za kilimo na pembejeo
 
Back
Top Bottom