Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka

Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka

Watatafuta visingizio vingi ila hawatokubali kua tatizo ni lao, sa hivi Tanzania sio sehemu nzuri ya kuinvest hata kidogo, investing money bongo ni kupoteza hela tu, serikali inasumbua sana investors conditions zimekua nyingi mno nyingine ambazo ni unnecessary.
Hakika wawe wakweli. Serikali na sera zake zinazobadilika kila siku ndio kikwazo kwa wawekezaji. Leo hii kule Morogoro kwa mfano naambiwa mwajiri ambaye karibu kila wakazi kumi wa Morogoro wanane walishafanyakazi hapo Tumbaku TTPL wameshalipa wafanyakazi wote mafao yao na mwakani wanafunga kiwanda rasmi. Hawa ni wawekezaji toka Marekani na wamekuwepo tangu enzi za ubinafsishaji miaka ya tisini.
Serikali ijitathmini kuliko kutafuta visingizio visivyo na tija. Leo nani atakuja kuwekea kwetu toka Marekani akisikia mwenzao mzoefu hapa amefunga biashara baada ya kuwa frustrated.
 
Huu ni kwa upande wa watumishi, je kwa upande wa serikali je?
Bado tatizo lipo,ila sio kama kwenye awamu za pili tatu na nne.Na mind you,rushwa kwenye awamu ya tano ikiwepo serikalini haina nia ya kumnufaisha mtu binafsi,but rather ni kwa ajili ya kuinafaisha serikali labda na chama kwa ujumla,kwa maslahi mapana ya nchi.
 
Muhimu hapa waambiwe tu Jiwe and company waache roho ya kichawi baaaasi
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amesema vitendo vya rushwa, urasimu uliokithiri na vinavyoendana na hivyo kwa watumishi wa umma ni chanzo cha kufukuza wafanyabiashara na wawekezaji nchini
Amesema hali hiyo inasababisha kushindwa kufikia lengo la Taifa la ukuaji wa kibiashara.

Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifunga kongamano la kibiashara la nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika lililofanyika kwa siku tatu mjini hapa.

Alisema watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, kwa ufanisi na kuondoa urasimu usio wa lazima ili kuvutiwa wawekezaji.

Kairuki alisema hata kama Serikali ikitumia nguvu kubwa katika kutangaza wafanyabiashara na wawekezaji kuja kuwekeza nchini, kama vitendo hivyo visipokomeshwa watumishi wa namna hiyo wataendelea kuwakimbiza.

Alisema kila mtumishi wa umma anatakiwa ajitathmini katika utendaji wake kwani vitendo hivyo vikiendekezwa vitasababisha wawekezaji kwenda kuwekeza nchi nyingine.

Alisema Serikali itaendelea kupunguza changamoto ya tozo kwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kuboresha biashara.
Naye mkuu wa mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga alisema Serikali haitawavumilia watumishi wa umma mkoani humo watakaokwamisha shughuli za kibiashara kwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Rais wa chama cha wafanyabiashara kutoka Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Ndakala Emmanuel alisema mkutano huo uliomalizika usiwe bure, bali Serikali ya Tanzania ifanyie kazi mambo yote yaliyojadiliwa ili kila mmoja aweze kunufaika na makubalianao hayo.

“Kama tusipopata matokeo mazuri ya kikao hiki itakuwa tumekaa bure hapa na kupoteza muda, ila kama mapendekezo yatafanyiwa kazi tutapata mafanikio katika biashara zetu,” alisema.

Hilo ni kongamano la kwanza kufanyika mkoani Kigoma, ambapo baadhi ya mikoa iliyofanya makongamano kama hayo yanayolenga kuvutia uwekezaji ni pamoja Mwanza, Arusha, Lindi na Tabora.

Na Yeye pia anaweza kutueleza sababu za kwanini nae ' hajatimka ' hapo alipo kama Waziri mpaka sasa?
 
Na Yeye pia anaweza kutueleza sababu za kwanini nae ' hajatimka ' hapo alipo kama Waziri mpaka sasa?
Aende wapi kwa mfano? Kada mwenzio anaenda wapi?
Anyway siasa pembeni, tunahitaji mabadiliko ya kweli sio ujanja ujanja unaoendelea. Kama kitu kimeamriwa kifanyike, kifanyike kweli
 
Awamu ya ukifutu nani atarisk Pesa zake.Ila soon Mungu ataleta ukombozi.Yote sababu ya kutokumsikiliza Mwalimu alishatadharisha juu ya vifutu.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amesema vitendo vya rushwa, urasimu uliokithiri na vinavyoendana na hivyo kwa watumishi wa umma ni chanzo cha kufukuza wafanyabiashara na wawekezaji nchini
Amesema hali hiyo inasababisha kushindwa kufikia lengo la Taifa la ukuaji wa kibiashara.

Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifunga kongamano la kibiashara la nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika lililofanyika kwa siku tatu mjini hapa.

Alisema watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, kwa ufanisi na kuondoa urasimu usio wa lazima ili kuvutiwa wawekezaji.

Kairuki alisema hata kama Serikali ikitumia nguvu kubwa katika kutangaza wafanyabiashara na wawekezaji kuja kuwekeza nchini, kama vitendo hivyo visipokomeshwa watumishi wa namna hiyo wataendelea kuwakimbiza.

Alisema kila mtumishi wa umma anatakiwa ajitathmini katika utendaji wake kwani vitendo hivyo vikiendekezwa vitasababisha wawekezaji kwenda kuwekeza nchi nyingine.

Alisema Serikali itaendelea kupunguza changamoto ya tozo kwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kuboresha biashara.
Naye mkuu wa mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga alisema Serikali haitawavumilia watumishi wa umma mkoani humo watakaokwamisha shughuli za kibiashara kwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Rais wa chama cha wafanyabiashara kutoka Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Ndakala Emmanuel alisema mkutano huo uliomalizika usiwe bure, bali Serikali ya Tanzania ifanyie kazi mambo yote yaliyojadiliwa ili kila mmoja aweze kunufaika na makubalianao hayo.

“Kama tusipopata matokeo mazuri ya kikao hiki itakuwa tumekaa bure hapa na kupoteza muda, ila kama mapendekezo yatafanyiwa kazi tutapata mafanikio katika biashara zetu,” alisema.

Hilo ni kongamano la kwanza kufanyika mkoani Kigoma, ambapo baadhi ya mikoa iliyofanya makongamano kama hayo yanayolenga kuvutia uwekezaji ni pamoja Mwanza, Arusha, Lindi na Tabora.
mbaaza zikikauka hupakazia jua
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Anakwepa makosa ya serikali juu ya wawekezaji anaanza kusingizia watumishi wa umma kua ndo wanasababisha wawekezaji kusepa,hapana hii serikali sio ya uwajibikaji serikali ya uwajibikaji lazima ikili adharani kua sera za nchi hii juu wanuwekezaji si rafiki,Mosi hakuna mwekezaji ambae atakuja kuwekeza mali zake kwenye nchi ambayo ina hubiri mfumo wa vyama vingi wenye kiini macho,katiba inavunjwa na serikali,haki za binadamu hakuna,uhuru wa habari kuminywa haki za vyama vya upinzani,Wateule wa Rais kuwasumbua wawekezaji mbele ya vyombo vya habari kama vile hakuna kituo chanuwekezaji,wawekezaji kusumbuliwa na serikali rejea ishu ya Acasia na barick.
 
Babu yako ndio Gundu tupu Kesha tuharibia nchi hii..
Nenda katafutell jingine uje nalo lakini sio haya Matope
 
Kiongozi wa nchi yafaa awe tajiri au mfanyabiashara hivo kwake ni rahisi kuvuta Pesa maana ujua Pesa ziko wapi.Ushirikiana Na wenye Pesa,udumisha urafiki Na nchi zenye Pesa,hawezi kuwa Na chuki Na wenye Pesa,then nchi inajaa Pesa watoto wanashiba pesa ,wakishiba Pesa wanawekeza palipo Na Pesa masikini wanapata ajira wanalipa kodi,ujamaa unabakia kwenye mgawannyo wa kodi tu.
 
Kinachonishangaza ni kwamba kinachoongewa nankinachoendelea ni vitu viwili tofauti. Rushwa ndio sababu kubwa ya wafanyakazi wa baadhi ya mamlaka za umma kuleta ukiritimba katika kazi zao. Mamlaka za kodi kuna watu wala hawaogopi kuomba rushwa ili "wakupunguzie" madeni yako au hela unazotakiwa kulipa. Rushwa bado ipo sana. Mpaka ije kupungua, inatakiwa nguvu ya ziada
Kweli tunahitaji nguvu ya ziada mkuu.Mimi ni muumini mkubwa wa "The China Alternative," nadhani hiyo ndiyo lugha pekee Watanzania watakayoielewa.
 
Back
Top Bottom