Kaini alipata wapi mke wake?

Kaini alipata wapi mke wake?

.
Leta ushahidi kutoka kwenye vyanzo vya dini
Screenshot_20210325-100647.jpg
 
Dhambi ni nini kwa lugha rahisi kabisa yenye mantiki? Dhambi kiasi mpaka hata mtu anafikisha umri wa miaka 60 kiuno kama kimwekwa super glue, miguu utazani imegongwa na nyundo? Enzi za Nabii Ibrahimu naona mzee ana miaka 100+ na anapiga mzigo kama 20s fulani hivi.
Dhambi ni msukumo wenye nguvu ambao unatufanya sisi tupende kuziendea njia ambazo ni kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo, badala ya kubarikiwa kwa kuyafuata mapenzi ya Mungu, tunaadhibiwa kama tutaishi kwa kuzifuata na kuishi kwa kufuata tamaa za Shetani, ambazo ndizo dhambi. Njia na matendo ya Shetani ni kinyume kabisa na zile za Mungu. Mungu anazichukia dhambi (Mithali 6:16-19). atendaye dhambi ni wa Ibilisi; (au Shetani) kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. (1Yohana 3:8).
 
UNCLE USIJARIBU KUFIKIRI KUOA DADA YAKO AU NDUGU WA DAMU UTAJILETEA MATATIZO KIBAO KWANI NAONA UNATAFUTA UHALALI WA KUMWEKA NDUGU KINYUMBA UKIENDELEZA UBAZAZI NA USHETWANI ULIOKUJAA KATIKA FIKRA ZAKO. KWANI SIONI MANTIKI YA SWALI LAKO.Kesho ubwabwa utakuwepo kwa mtaalamu wa kucheza na koboko.
Mkuu bado sijaona jibu hapo zaidi ya maneno yasiyo na msingi
 
Mkuu bado sijaona jibu hapo zaidi ya maneno yasiyo na msingi
Kwa mazingira yaliyopo hapo kale walioana ndugu na hapakuwa na shida. Kwani wao kama ni shamba ndo walikuwa mbegu, kulana na kutafunana ilikuwa sio shida. Ndo maana katika vitabu idadi ilikuwa ni ya wanaume tu, na hata leo misemo iliyopo katika jamii zetu ni kuwa "mwanaume, nduguyo ni mwanaume mwenzio".Sababu wanawake walionekana kama bidhaa zaidi pasipo kujali utu wao. Lakini sasa mambo yamebadilika sana kutokana na idadi ya watu na maendeleo kuongezeka.
 
Kwa mazingira yaliyopo hapo kale walioana ndugu na hapakuwa na shida. Kwani wao kama ni shamba ndo walikuwa mbegu, kulana na kutafunana ilikuwa sio shida. Ndo maana katika vitabu idadi ilikuwa ni ya wanaume tu, na hata leo misemo iliyopo katika jamii zetu ni kuwa "mwanaume, nduguyo ni mwanaume mwenzio".Sababu wanawake walionekana kama bidhaa zaidi pasipo kujali utu wao. Lakini sasa mambo yamebadilika sana kutokana na idadi ya watu na maendeleo kuongezeka.
Hapo sawa
 
Haya jibu niliyouliza sasa kwenye komenti yangu ilikuwaje weae uwe na nyewel kipilipili huku wengine wakiwa vile walivyo ngozi n.k
Akijibu nitag
 

Mahali pa bustani ya Edeni ni wapi haswa?​

Kitu pekee ambacho Biblia inatuambia kuhusu eneo la bustani la Edeni linapatikana katika Mwanzo 2: 10-14, " Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ikagawanyika katika maji ya kichwa vinne. Jina la kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yoye ya Havila, ambako kuna dhahabu ... Jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi. Jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati. "Utambulisho halisi wa Mito ya Pishoni na Gihoni haujulikani, lakini Mito ya Hidekeli na Frati inajulikana.

Ikiwa Hidekeli na Frati iliyotajwa ni mito sawa na mito inayojulikana kwa majina hayo leo, inaweza kumaanisha bustani la Edeni ni mahali fulani huko Mashariki ya Kati, inawezekana kuwa huko Iraqi. Haiwezi kuwa tu kwa bahati ya kwamba kanda ya Mashariki ya Kati ni mahali ambapo sayari ilikuwa nzuri zaidi-mahali ambapo bustani la Edeni lilikuwa. Ikiwa mafuta ni inatoka kwa mimea na miili ya wanyama iliyooza kama wanasayansi wengi wanavyoamini, basi hili ndio eneo ambalo tunaweza kutarajia kupata amana kubwa zaidi ya mafuta. Kwa kuwa Bustani ilikuwa ni mfano wa ukamilifu, inasisitiza kuwa kuoza kwa vifaa vya kikaboni vilivyo bora zaidi duniani vinaweza kuzalisha akiba kubwa ya mafuta bora duniani.

Watu wametafuta bustani ya Edeni kwa karne nyingi bila kufanikiwa. Kuna maeneo mbalimbali ambayo watu wanadai kuwa eneo la awali la Bustani la Edeni, lakini hatuwezi kuwa na uhakika. Nini kilichotokea katika bustani ya Edeni? Biblia haijasema haswa ni nini kilichotokea. Inawezekana kwamba bustani ya Edeni iliharibiwa kikamilifu katika Mafuriko au kwamba inakaa kupungua na kubadilika kuwa mafuta ambayo imezikwa chini ya amana za mchanga, karne zilizopita.
 
Si nimetoa AYA HIZO SOMA ZOTE.
za biblia kuanzia aya ya 10.
Bustani ya Edeni ipo nchi gani kwa sasa duniani?


Mungu alipoiumba dunia, alichagua eneo moja, na kulifanya kuwa la kipekee na la kitofauti na maeneo mengine yote aliyoyaumba duniani. Eneo hilo akaliita Edeni. Edeni maana yake ni eneo la furaha kuu, utulivu,paradiso ya Mungu.

Lakini hakuishia hapo tu bali ndani ya hiyo Edeni upande wa mashariki alitengeneza bustani nzuri sana, ambayo inajulikana na wengi kama bustani ya Edeni. Bustani hii ndiyo Mungu aliyomweka mwanadamu wa kwanza hapo aishi (yaani Adamu na uzao wake.)

Lakini kama tunavyosoma biblia, wazazi wetu wa kwanza walipoasi, walifukuzwa kutoka katika bustani ile, na kuanzia hapo, hakuna aliyejua makao halisi ya bustani ya Edeni yalikuwa wapi, vifunguu pekee vinavyotupa taswira ya eneo la bustani ya Edeni ni hivi;

Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne.
11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;
12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.
13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.
14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati”.
Kama tunavyoona hapo, kulikuwa na mto uliokuwa unatoa maji kutoka bustanini na baadaye ukagawanyika katika vichwa vinne, na viwili kati ya hivyo (yaani Hidekeli na Frati) vinajulikana mpaka sasa na vipo maeneo ya nchi ya Iraq, ili kusoma na kufahamu zaidi historia yao fungua hapa >>>> Mto frati na Hidekeli Na hiyo imewafanya masomi wengi wa biblia kudhania kuwa Edeni ilikuwa maeneo ya nchi ya Iraq au kando kando yake.

Lakini vile vingine viwili (yaani Pishoni na Gihoni) havijajulikana bado. Na iyo imewafanya wengine kudhani bustani ya Edeni ilikuwa nchi ya Uturuki ya sasa n.k.

Hivyo, hakuna uthibitisho wa moja kwa moja wa kudhania kuwa Edeni ilikuwa Iraq, au Uturuki au sehemu nyingine yoyote. Na hiyo ni kwasababu ya mabadiliko makubwa ya nchi yaliyokuwa yanatokea wakati wa gharika na ule wakati wa kugawanyika kwa nchi (Mwanzo 10:25). Historia inaonyesha kuwa dunia ilibadilika mwonekano wake kwa sehemu kubwa sana.

Lakini ni wazi kuwa Edeni haikuwa pengine zaidi ya mashariki ya kati, na sio Afrika kama wanasayansi wanavyoamini, nami naamini ilikuwa katika nchi Kaanani (Yaani Israeli ya sasa).
 
Back
Top Bottom