Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

MAKAMBAKO TC NI MWENDO WA KUIBUA VYANZO VYA MAPATO HILI LITAKUWA SOKO KUBWA LA NAFAKA MFANO MAHINDI NA WANA ENEO LA KUTOSHA KM 10 KUTOKA CBD SONGEA ROAD ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡Kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe, yapongeza utekelezaji wa mradi wa maghala 112 Makambako.

Na. Lina Sanga

Kamati ya siasa Wilaya ya Njombe imepongeza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa maghala 112 ya kuhifadhia nafaka unaogharimu takribani bil. 2.24,katika Mtaa wa Makatani,Kata ya Lyamkena, Halmashauri ya Mji Makambako.

Pongezi hizo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo,katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Mji Makambako katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Mhe. Justin Nusupila Sanga,Mwenyekiti Kamati ya siasa Wilaya ya Njombe amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo una tija kubwa kwa wananchi na Serikali,kwani ni mradi mzuri wa uwekezaji unaowaweka wafanyabiashara pamoja kwenye mazingira rasmi na kupata soko la uhakika.

"Nipongeze utekelezaji wa mradi huu kwani una tija kwa wananchi na Serikali,na ni uwekezaji mzuri unaoenda sambamba na jitihada za Serikali kutenga maeneo rasmi ya biashara mbalimbali",alisema Mhe. Sanga.

Ametoa rai kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako,kuendelea kufanya maboresho na kukamilisha mahitaji mbalimbali ambayo yanatakiwa kufanywa na Halmashauri ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma muhimu zinazojitajika eneo la mradi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma ya Umeme inapatikana pamoja na huduma ya Maji.

Aidha,ametoa rai kwa Ofisi ya Meneja wa TARURA Wilaya ya Njombe, kutenga bajeti ya matengenezo ya barabara kwenye eneo la mradi ambayo ina uwezo wa kuhimili magari mazito ya mizigo.

Leo Sanga,mbeba mizigo katika maghala hayo,ameishukuru Serikali kwa kubuni mradi huo kwani umeongeza uhakika wa watu mbalimbali kufanya kazi na kupata fedha kwa ajili ya kuendesha maisha yao.
1693018671685.jpg
1693018671685.jpg
1693018681706.jpg
1693018695992.jpg
 
WAZIRI MKUMBO ALIVYOSHANGAZWA NA UWEKEZAJI MKUBWA SEKTA YA KILIMO WILAYANI SONGEA
Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo ameshangazwa na uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo ambapo katika Halmashauri ya Madaba na Songea mkoani Ruvuma wawekezaji toka nje wamewekeza katika mashamba yenye ukubwa wa hekta zaidi ya 2500.
Akiwa katika Halmashauri ya Madaba,Waziri Mkumbo alishuhudia uwekezaji mkubwa wa Kampuni ya kigeni ya Silver Ndolela iliyowekeza katika shamba lenye ukubwa wa hekta 1500 ambapo kampuni hiyo inazalisha mbegu za aina nne kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji.
Meneja wa shamba hilo alizitaja mbegu zinazozalishwa na Kampuni hiyo kuwa ni maharagwe,mahindi,ngano na viazi ambapo Waziri Mkumbo alisisitiza uwekezaji katika mbegu bora ni muhimu hapa nchini kwa kuwa moja ya changamoto katika kilimo ni upatikanaji wa mbegu bora.
โ€œWakulima wetu wanatumia mbegu hafifu wanalima eneo kubwa na kupata mavuno kidogo,hivyo uwepo wa shamba hili la mbegu bora itasaidia kuboresha kilimo hapa nchini โ€™โ€™,alisisitiza Waziri Mkumbo.
Waziri wa Mipango na Uwekezaji pia alikagua shamba kubwa la kilimo cha umwagiliaji la Kampuni ya AVIV katika Kijiji cha Lipokela Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Prof.Mkumbo amefurahishwa na uwekezaji mkubwa katika shamba kahawa uliofanywa na Kampuni ya AVIV TANZANIA LTD ambapo Kampuni hiyo inalima na kuchakata kahawa kwa mwaka tani zaidi ya 2000 katika shamba la kahawa lenye ukubwa wa hekta zaidi ya 1000.
Waziri Mkumbo amesisitiza kuwa kulima na kuchakata kahawa ni uwekezaji mkubwa ambao umefanywa kwa kuwezeshwa na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ambapo amesema uwekezaji huo unashughulikia sekta ya kilimo ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Ameipongeza Kampuni ya AVIV kwa kutekeleza mambo matatu kwa wakati mmoja ikiwemo kilimo cha kahawa,kuchakata mazao ya kilimo hivyo kutoa ajira kwa watanzania na kuongeza mauzo nje ya nchi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile akizungumza baada ya Waziri kutembelea maeneo ya uwekezaji katika shamba la Madaba na Lipokela,ameutaja Mkoa wa Ruvuma kwa miaka 13 sasa unaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula nchini.
Amesema katika kutambua mchango wa Mkoa wa Ruvuma kwenye uzalishaji chakula ,mwaka huu kwenye maadhimisho ya Nanenane Kitaifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alitoa chetu maalum kwa Mkoa wa Ruvuma kwa kushika nafasi ya kwanza kwa uzalishaji nafaka.
Awali akitoa taarifa ya Kampuni ya AVIV, Meneja Msaidizi wa Kampuni ya AVIV TANZANIA Muthana Namb amesema asilimia 80 ya kahawa inayochakatwa na Kampuni hiyo inauzwa katika nchi mbalimbali Duniani zikiwemo Marekani,Saudi Arabia,India, Japan, Jordan na Afrika ya Kusini.
Naye Mwakilishi wa Kampuni hiyo anayesimamia kilimo Johson Kishumba amesema Kampuni ya AVIV TANZANIA imekuwa kampuni ya kwanza katika bara la Afrika kupewa Tuzo ya Water Stewardship inayotolewa na SGS ya nchini Afrika ya Kusini kwa kufanya vizuri kwenye kilimo na mazingira.
Hata hivyo amesema kampuni hiyo inashirikiana na wananchi wanaozunguka shamba hilo ambao wamekuwa wanasaidiwa katika sekta za afya,maji na mazingira na kwamba baadhi ya wananchi wanapata ajira kwenye shamba la kahawa.
Waziri wa Mipango na Uwekezaji alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Ruvuma kwa lengo la kukutana na wawekezaji,kusikiliza mafanikio na changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi hatimaye kuimarisha zaidi eneo la uwekezaji
1693028248818.jpg
1693028242172.jpg
 
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Mji makambako na Benki ya NMB tawi la makambako, leo wamefanya utalii wa ndani katika hifadhi ya Mpanga Kipengere ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutangaza Utalii kusini mwa Tanzania na nje ya Mipaka ya Tanzania.

#utaliiwandani
#utaliikaribukusini
1693094908879.jpg
1693094879937.jpg
1693094888649.jpg
 
Project zinaendelea baada ya kuanza kuweka Lami Barabara inayozunguka mji wa makambako watu wanatumia fursa hichi ni kipande Cha ilembula hadi mtwango Wacha kazi iendelee naona maono ya aliyekuwa mbunge wa zaman Njombe kaskazin yanatumika kuwa tarafa ya makambako na wangingombe ziwe mji mmoja
IMG_20230903_104741_526.jpg
IMG_20230903_104459_658.jpg
IMG_20230903_131338_920.jpg

Ilembula.10.jpg
 
Kazi inaendelea tulisha sema around makambako sub town zinakuwa kwa speed Sana Kama mtwango, ilembula Na kipagamo kilichobaki ni kuweka miundombinu ya maana ili mkoa wa njombe uwe na mji mkubwa wa biashara naona wabunge now wapo kulifanyia kazi Na hii itaenda kuunganisha na iliyo toka ifakara ko mtu wa makambako atakuwa hazungukii Tena kibena kwenda lupembe๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mkoani Njombe Edwin Enosy Swalle amehoji Bungeni juu ya Ni Lini Serikali itaanza Ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Mtwango kwenda Ikuna ili kurahisisha Shughuli za Kiuchumi kwa Wananchi wa Kata ya Mtwango na Kata za Karibu ambapo majibu ya Serikali Bungeni yametolewa na Waziri wa Tamisemi Festo Dugange.

Akihoji Bungeni Mbunge wa Lupembe Edwin Enossy Swalle Amesema

"Mh Spika Nakushukuru kwa Kunipa nafasi Hii Mhimu kwaajiri ya kuwakilisha Wananchi wangu wa Jimbo la Lupembe, Mh Spika Mji wa Mtwango Jimbo la Lupembe ni Mji ambao unakua kwa kasi Sana je Serikali inampango gani wa Kujenga Barabara ya Lami kutoka Mtwango Kwenda Ikuna?Asante"

Majibu ya Serikali Bungeni yakatolewa na Waziri wa Tamisemi Mh Festo Dugange ambae amesema.

"Asante sana Mh Spika Naomba Kujibu Swali la Mh Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Enosy Swalle juu ya Uhitaji wa Barabara ya Lami katika Mji wa Mtwango ambayo inaunganisha kata ya Ikuna na kata ya Mtwango ni kweli Mji wa Mtwango unakua kwa kasi sana lakini Tulishaelekeza Meneja wa Tarura kuweka Vipaombele vya Ujenzi wa Barabara za Lami na katika Halmashauri zote katika Zile Fedha za Bajeti za Tarura tulielekeza kwamba angalau kuwe na Bajeti kwaajiri ya Ujenzi wa Barabara za Lami,Kwa hiyo naomba ni Sisitize kwa Meneja wa Tarura Wilaya ya Njombe asimamie Maelekezo hayo lakini kama Fedha ile ya Bajeti haitoshelezi afanye Tathimini na kuleta Ofisi ya Rais Tamisema ili tuweze kuona uwezekano wa Kupata Fedha nyingine ili kuongeza nguvu ya Utekelezaji wa Mradi huo"

View: https://www.instagram.com/p/CwyNtYUNWYj/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
Ilembula.10.jpg
 
Miji mingi inatakiwa kwenda kuji funza dodoma mji umepangiliwa ila Kuna miji itagoma kutokana na jiografia yake ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Wapo Mkoani Dodoma kwa ziara ya Kujifunza.
Wakiwa Mkoani humo wamefanikiwa kutembelea maeneo ya Uwekezaji na kubadilishana uzoefu wa namna ya kukuza Mapato yatokanayo na Makusanyo ya Vyanzo vya ndani.
Maeneo yaliyotembelewa ni Pamoja na Eneo maalumu la Machinga "Machinga Complex, Eneo la Ujenzi wa Hotel na Ukumbi wa Mikutano, Stendi kuubya Mabasi, Soko kuubla Ndugai na eneo lililojengwa Shule ya Awali na Msingi inayoendeshwa kama Shule Binafsi kwa lengo la kukuza kipato cha Jiji hilo.
Hapo kesho waheshimiwa Madiwani hao watapata fursa ya Kujionea uendeshwaji wa Shughuli za Bunge.
 
Huu mradi duuh wanasogeza mbele tuuu ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡โ™จ๏ธ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡MAMENEJA WA TARURA WAAGIZWA KUSIMAMIA KIKAMILIFU MRADI WA TACTIC.

OR TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais โ€“ TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) amewaagiza Mameneja TARURA wa Mikoa na Wilaya zote nchini zinazotekeleza Mradi wa kuboresha miundombinu katika Majiji, Manispaa na Miji (TACTIC) kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu hatua zote za manunuzi na kuhakikisha Wakandarasa wanafika katika maeneo ya kazi kuanza utekelezaji wa miradi hiyo.

Amesema hayo leo tarehe 04 Septemba 2023 Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Mashaka Gambo aliyetaka kujua Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Stendi ya Kisasa kwenye eneo la Bondeni City Jijini Arusha kupitia Mradi wa TACTIC.

Dkt. Dugange amesema Serikali kupitia Mradi wa TACTIC itatekeleza ujenzi wa stendi kuu ya kisasa ya mabasi, Masoko mawili pamoja na Bustani moja ya mapumziko kwenye eneo la Bondeni City kwa lengo la kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Jiji la Arusha na maeneo jirani.

Dkt. Dugange ameeleza kuwa Utekelezaji wa mradi wa TACTIC, kazi ya usanifu imekamilika na taratibu za ununuzi kwa ajili ya kumpata mzabuni inatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2023, baada ya taratibu hizo kukamilika, utekelezaji wa ujenzi kwenye maeneo yaliyoainishwa utaanza.
 
Huu mradi duuh wanasogeza mbele tuuu ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡โ™จ๏ธ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡MAMENEJA WA TARURA WAAGIZWA KUSIMAMIA KIKAMILIFU MRADI WA TACTIC.

OR TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais โ€“ TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) amewaagiza Mameneja TARURA wa Mikoa na Wilaya zote nchini zinazotekeleza Mradi wa kuboresha miundombinu katika Majiji, Manispaa na Miji (TACTIC) kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu hatua zote za manunuzi na kuhakikisha Wakandarasa wanafika katika maeneo ya kazi kuanza utekelezaji wa miradi hiyo.

Amesema hayo leo tarehe 04 Septemba 2023 Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Mashaka Gambo aliyetaka kujua Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Stendi ya Kisasa kwenye eneo la Bondeni City Jijini Arusha kupitia Mradi wa TACTIC.

Dkt. Dugange amesema Serikali kupitia Mradi wa TACTIC itatekeleza ujenzi wa stendi kuu ya kisasa ya mabasi, Masoko mawili pamoja na Bustani moja ya mapumziko kwenye eneo la Bondeni City kwa lengo la kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Jiji la Arusha na maeneo jirani.

Dkt. Dugange ameeleza kuwa Utekelezaji wa mradi wa TACTIC, kazi ya usanifu imekamilika na taratibu za ununuzi kwa ajili ya kumpata mzabuni inatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2023, baada ya taratibu hizo kukamilika, utekelezaji wa ujenzi kwenye maeneo yaliyoainishwa utaanza.
Hapo ni Kwa Arusha Kwa hiyo miradi ya Stand na soko.

Ila Kwa maeneo mengine Chief wa Tarura alisema miradi inaanza mwezi huu but sio zaidi ya October 2023.
 
Back
Top Bottom