Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

Mumeongoza sababu ya mauzo ya dhahabu ya mzungu

Mungekuwa ni nyie wenyewe msingekuwa maskini Wala kuzidiwa na Arusha kwenye financial inclusion
Unaumia ..bado sijamaliza ...wale mliokuwa mnatamba na utajiri wa makadirio kugawa Kwa idadi ya watu
Hao kaskazin wametuzidi wapi hapa
Screenshot_20230706-101502.jpg
 
Hiv inakuwaje watu maskini wa kitupwa wasioweza kupata hata 1500 kwa siku kuwa na transaction za hela namna hio?

Serikali yetu ina ujinga mwingi ndo maana wanashindwa kuongoza chochote
Wanatumiwa diaspora walioko kwenye Mikoa yetu.
 
Ulinzi zaidi kuimarishwa bomba la TAZAMA
-
TANZANIA na Zambia kwa pamoja zinatarajia kuimarisha ulinzi katika maeneo yanayopitiwa na bomba la mafuta la TAZAMA ambalo kwa sasa linasafirisha dizeli badala ya mafuta ghafi.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam Ijumaa Julai 7, 2023 na Waziri wa Nishati, January Makamba, kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ikiwa ni muda mfupi tangu kufanyika kwa kikao kilichokutanishwa mawaziri sita wa sekta za nishati na ulinzi kutoka Tanzania na Zambia.

Kwa mujibu wa Waziri Makamba, maeneo mengine ambayo wamekubaliana ni kuongeza idadi ya askari watakaolinda bomba hilo, kushirikiana jamii zinazozunguka bomba hilo, ulinzi utaohusisha ndege zisizo na rubani maarufu kama ‘drone’ sambamba na kuongeza wigo wa bomba hilo ili kuliwezesha kusafirisha mafuta kwa kiwango kinachotakiwa tofauti na ilivyo hivi sasa.

“Katika mkutano wetu, tumekubaliana kuimarisha kamati za ulinzi na usalama ambapo bomba linapita, matumizi ya ndege zisizo na rubani na ushirikishaji wa wananchi katika vijiji vinavyopitiwa na bomba hilo.

“Smbamba na hayo tumekubalina kuimarisha miundombinu ikiwemo kambi na vituo vya polisi vinaongezeka katika maeneo yale ambayo bomba hilo linapita,” amesema Makamba na kuongeza kuwa kando ya eneo la ulinzi pia wamejadili juu ya upanuzi wa bomba hilo ili kusafirisha kwa ufanisi mafuta.

“Lakini pia tumejadili juu ya ujenzi wa bomba jipya la gesi,” amesema Makamba ambaye aliongoza kikao hicho.

Akitaja sababu za kuimarishwa zaidi kwa bomba hilo, Makamba amesema kuwa lilijengwa miaka 60 ambapo lilikuwa likisafirisha mafuta ghafi, lakini kuanzia Machi, mwaka huu limeanza kusafirisha dizeli na siyo mafuta ghafi na kwamba kwa sababu hiyo lazima kuimarisha ulinzi.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi, Ambrose Lufuma, amesema wamekubaliana kuimarisha ulinzi katika bomba hilo, huku akisisitiza kuwa hivi sasa miundombinu hiyo inasafirisha bidhaa iliyochakatwa kwa ajili ya matumizi ya mwisho.

“Ifahamike tu kwamba hii ni bidhaa ambayo ipo tayari kwa matumizi hivyo inahitaji ulinzi wa kutosha. Hivyo tutahakikisha kuwa kunajengwa vituo vya polisi pembezoni mwa bomba hilo ili kuimarisha ulinzi,” amesema.
#MtanzaniaDigital
1688774129539.jpg
1688774564030.jpg
 
Napenda maghorofa mafupi mafupi ( ghorofa 1 Hadi 3) yanayojengwa kwa Kasi Bukoba...huku mnara wa kanisa ukiwa mrefu zaidi mjini bukoba....
Inakuwa simple Paris...

Nimeitoka Bukoba 2021...lakin kwa hii picha Tu ya kisehemu kidogo cha mitaa ya miembeni naona maghorofa Saba mapya....
Bukoba inahitaji miundombinu Tu ya stend na Barbara zake kupanuliwa vzr...



dfg%20(1).JPG
 
Napenda maghorofa mafupi mafupi ( ghorofa 1 Hadi 3) yanayojengwa kwa Kasi Bukoba...huku mnara wa kanisa ukiwa mrefu zaidi mjini bukoba....
Inakuwa simple Paris...

Nimeitoka Bukoba 2021...lakin kwa hii picha Tu ya kisehemu kidogo cha mitaa ya miembeni naona maghorofa Saba mapya....
Bukoba inahitaji miundombinu Tu ya stend na Barbara zake kupanuliwa vzr...



View attachment 2681864
Usitake kudanganya watu,sema hamna pesa za kujenga nyumba ndefu 😁😁
 
Ni dwarf buildings, Kagera na Mbeya wapi ni njia ya Earthquake? Acha visingizio
Mbeya mlishawahi pata earthquake gan nyie...
Unafikiri kile kitu kinatokea tu...
Linaweza kuwa eneo lake lakin kuna miamba migumu...so haizuii kujengwa maghorofa...

Bukoba tetemeko la 6 scale liliangusha nyumba zaidi ya 2000...so kuna mambo ya kuzingatia katika ujenzi ukiwa Bukoba...lakin hawajazuia kujenga majengo marefu...wanajenga with needs
 
Vibasi vya kimaskini hivi ndio ulinganishe na Benz au Marcopolo za Sauli? Kuwa serious kidogo..

Sauli hajawahi pata ajali ya kuia Toka aanze biashara
Hio Marcopolo Ya Sauli ina muda gani haipo barabarani ba hio Benz ambayo ukipanda kufika ni panapo majaaliwa maana sehem yyt inataga

Speaking of Benz unaifahamu T 910 DNH?
 
SERIKALI KUJENGA CHUO KIKUU WILAYANI SENGEREMA
Waziri wa elimu Prof Adolph Mkenda akikagua eneo la eka 378 Karumo kata ya Nyamatongo wilayani Sengerema kitakapojengwa Chuo Kikuu cha Ardhi Kampasi ya Mwanza ambacho kitajengwa ndani ya miezi 15 na kinatarajiwa kukamilika kujengwa mwezi October mwakani kwa fedha za mkopo nafuu kutoka benki ya dunia (WD).
Mratibu wa ujenzi wa miundombinu wa mradi huo kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Dk Fredrick Salukele amesema zaidi ya Sh18 bilioni zitatumika kujenga majengo matano ya kampasi ya Mwanza ya chuo hicho na pia zitatumika kuanzisha mitaala na kuweka vifaa vya kujifunzia na kufundishia ikiwa ni awamu ya kwanza ya mradi wa HEET.
”Asilimia 70 ya fedha hiyo itatumika kwenye ujenzi wa majengo hayo ambayo ni studio, jengo la utawala, ofisi za walimu, maktaba, bweni na zahanati itakayohudumia wanachuo na wanakijiji wanaozunguka chuo hicho, asilimia zinazobakia zitatumika kwenye samani, uandaaji wa mitaala kwa awamu ya kwanza ya mradi.
Amesema majengo hayo yatakapokamilika wanatarajia kuanza na wanafunzi 414 huku mpango wao nikuwa na wanafunzi 10,000 kutoka Kanda ya Ziwa katika kozi za wasanifu majengo, wajenzi, migogoro na usimamizi wa ardhi,kozi zinazoendana na shuguli za matumizi ya ziwa, ufundishaji wa namna ya upimani ndani ya maji, uhifadhi mazingira pamoja na kozi mama za chuo hicho.
 
Watasema wanaongoza kwenye utajiri wa pesa lakini takwimu zinawakataa ..mikoa iliyoongoza Kwa miamala ya fedha kuweka na kutoa pesa
1.dar es salaam
2 Mwanza
3.arusha

Wapi iringa, mbeya mnaojikuta per Capita income
Tushawaaambia utajiri wenu wa makadirio hauna loloteView attachment 2681296
Hapa ndio sehemu ya kupanga mikoa kumi masikini kwa haki bila chuki
Na hizi ndio mikoa masikini zaidi nchini na mingine inabebwa na viwanda vingi lakini bado imetopea kwenye lindi la umaskini wa mtu mmoja mmoja Tanzania
1.katavi
2.Simiyu
3.Rukwa
4.Lindi
5.Singida
6.Mtwara
7.Manyara
8.Tabora
9.Kigoma
10.Pwani.
 
Hapa ndio sehemu ya kupanga mikoa kumi masikini kwa haki bila chuki
Na hizi ndio mikoa masikini zaidi nchini na mingine inabebwa na viwanda vingi lakini bado imetopea kwenye lindi la umaskini wa mtu mmoja mmoja Tanzania
1.katavi
2.Simiyu
3.Rukwa
4.Lindi
5.Singida
6.Mtwara
7.Manyara
8.Tabora
9.Kigoma
10.Pwani.
Simiyu inatuangusha sana ....huo mkoa haukujiandaa urudishwe Mwanza
 
Napenda maghorofa mafupi mafupi ( ghorofa 1 Hadi 3) yanayojengwa kwa Kasi Bukoba...huku mnara wa kanisa ukiwa mrefu zaidi mjini bukoba....
Inakuwa simple Paris...

Nimeitoka Bukoba 2021...lakin kwa hii picha Tu ya kisehemu kidogo cha mitaa ya miembeni naona maghorofa Saba mapya....
Bukoba inahitaji miundombinu Tu ya stend na Barbara zake kupanuliwa vzr...



View attachment 2681864
Hapa hata Mbeya inatakiwa ikajifinze namna miji inavyopangwa na majengo yanavyopaswa kuwa, hongereni sana wakina nshomile waitu.
 
Back
Top Bottom